Wale tunaosikilizia maumivu ya loan board tukutane hapa

Babafetty

Senior Member
Nov 11, 2013
107
107
Nimemaliza chuo kikuu cha Dar es Salaam mwaka 2009, ila kiukweli nilikua napokea mkopo toka HELSB 60%, ilikua ndogo ila ilivuta mpaka miaka mitatu ikaisha. Baada ya kumaliza chuo nilipata kazi mwaka Vodacom nikafanya kwa mwaka mmoja kabla ya kuingia serikali kuu, kipindi chote hicho nilikua sijaanza kukatwa, miaka ya 2013 hivi nikaenda kupiga masterz kwa mshahara na marupurupu.

Duh, balaa likaanza mkuu wa sasa aliposhika madaraka, kwanza nilipigwa beats, nikaenda mwenyewe kujisalimisha bodi ya mkopo, wakaanza kukata 8%, maisha yalienda, kwan haikuniumiza kichwa sana, baada ya miezi jamaa si akaongeza % ya makato, ikafika 15%, ndugu ile ilinifanya nitoke mchezoni, manake ukizingatia nilikua na makato mengine ya mkopo, niliona kama mwisho wa mwezi ukifika napokea salary slip pekee yake, mshahara hakuna.

Nikapata matarajio baada ya mkuu kusema kuna ongezeko si kaniongezea tsh. 13,000 kiukweli naona kama kakazia vyuma vizuri.

Sasa mkopo wenyewe unaisha 2022, ila tatizo kubwa limeanzia kwenye makato yasiyokuwa na kinga toka loan board.

Nipe expirience yako jinsi ulivyohathirika na mkopo wa chuo, baada ya kukopeshwa kidogo na kukatwa kikubwa.

Chuma kimekazwa vizuri kwakweli.
 
Ni kawaida, huyu jamaa anatuumiza kwa makato ila kiukweli wengi tutamaliza mapema, mimi binafsi nimebakiza miezi 26 tu wamalize deni lao. Ninachofurahi zaid nitamaliza muda mmoja na Mikopo mingine. Nikienda kukopa bank baada ya kwisha kwa pamoja Mikopo hiyo lazima nijenge viwanda kumsapoti jamaa, ingawa napokea hela ya madafu now.
 
Haya sio makato bali ni nikisasi cha kutoipigia ccm kura 2015.Anadhan anatukomoa kumbe anajimaliza mwenyewe maana watu wengi watamalia mapema,sijui ataanzisha makato gani tena.Labda hili linaloitwa taadhar kazini.
 
Ee Mungu Tusikie Nasisi Tusimame Kwenye Ile Foleni Ya ATM Hatutalilia Kuhusu Makato Na Nyongeza Ya Mshahara
 
Nimemaliza chuo kikuu cha Dar es Salaam mwaka 2009, ila kiukweli nilikua napokea mkopo toka HELSB 60%, ilikua ndogo ila ilivuta mpaka miaka mitatu ikaisha. Baada ya kumaliza chuo nilipata kazi mwaka Vodacom nikafanya kwa mwaka mmoja kabla ya kuingia serikali kuu, kipindi chote hicho nilikua sijaanza kukatwa, miaka ya 2013 hivi nikaenda kupiga masterz kwa mshahara na marupurupu.

Duh, balaa likaanza mkuu wa sasa aliposhika madaraka, kwanza nilipigwa beats, nikaenda mwenyewe kujisalimisha bodi ya mkopo, wakaanza kukata 8%, maisha yalienda, kwan haikuniumiza kichwa sana, baada ya miezi jamaa si akaongeza % ya makato, ikafika 15%, ndugu ile ilinifanya nitoke mchezoni, manake ukizingatia nilikua na makato mengine ya mkopo, niliona kama mwisho wa mwezi ukifika napokea salary slip pekee yake, mshahara hakuna.

Nikapata matarajio baada ya mkuu kusema kuna ongezeko si kaniongezea tsh. 13,000 kiukweli naona kama kakazia vyuma vizuri.

Sasa mkopo wenyewe unaisha 2022, ila tatizo kubwa limeanzia kwenye makato yasiyokuwa na kinga toka loan board.

Nipe expirience yako jinsi ulivyohathirika na mkopo wa chuo, baada ya kukopeshwa kidogo na kukatwa kikubwa.

Chuma kimekazwa vizuri kwakweli.
Haha eti "makato yasiyo na kinga".. Kwahiyo unakatwa bila kinga mkuu
 
Acheni utumwa hiyo pesa siyo ruzuku mrudishe, mkinyimwa mkopo mnanuna na kuandamana mkipewa kurudisha mnapaniki kuweni kifikira na si kimwili kumbuka ule ni mkataba ukihisi unaonewa ama mashariti yamekiukwa nenda mahakamani,,,
 
Poleni jamani...mungu amuweke mzee wangu mahala pazuri huko alipo.
Maana aliniambia usiombe mkopo nitalipa kila kitu.

Kuna jamaa yangu alikuwa anapewa hela ya ada kwao halaf akachukua mkopo sasa hivi anajuta
 
Acheni utumwa hiyo pesa siyo ruzuku mrudishe, mkinyimwa mkopo mnanuna na kuandamana mkipewa kurudisha mnapaniki kuweni kifikira na si kimwili kumbuka ule ni mkataba ukihisi unaonewa ama mashariti yamekiukwa nenda mahakamani,,,
jina lako tu linaonyesha ushapotea..
ha ha ha.
 
Imekaa vizuri 15% maana wengi wanamaliza deni mapema. Kama ungekata miaka 4 sasa ni miaka 2 tu umemaliza unaanza kufurahia maisha.
 
Back
Top Bottom