Wale tunaopenda vacation, sehemu gani ya utalii Tanzania uliyofika au unatamani kufika?

Kwenda naona sio shida...shida kubwa ni hotels na mutu ya kukuonjesha maendeo...hahhahaha ni majanga lkn kama huna mwenyeji wa kukutembeza...ACHa nianze kutafuta muarabu mwenyeji
Hotels mbona kawaida sana. Kuanzia $50 hotel zinaridhisha kabisa. Kutembea huna haja ya mwenyeji. Google sehemu za kutembelea ukiwa Dubai then unaenda mwenyewe tu tena usitumie taxi bei mbaya,tumia dubai metro iko straightfoward unafika sehemu nyingi sana kwa bei chee.
 
Hotels mbona kawaida sana. Kuanzia $50 hotel zinaridhisha kabisa. Kutembea huna haja ya mwenyeji. Google sehemu za kutembelea ukiwa Dubai then unaenda mwenyewe tu tena usitumie taxi bei mbaya,tumia dubai metro iko straightfoward unafika sehemu nyingi sana kwa bei chee.
hapo pazuri, asante mnooo
 
Mkuu nimekukubali.
Nakazia vacation ni muda wa ku-rejuvenate. Tunahitaji sana mapumziko kutokana na purukushani za maisha.
Tafuta mahali tulivu nje ya mazingira ya kila siku na pumzika/fanya vitu tofauti.
Mfano kwa aliyeleta mada: Gibbs from/to Ngorongoro crater ukapitia view ya Lake Manyara.
Stone town ukaenda spice farm (utajifunza mengi) ukamalizia na sunset view.
Jaribu a day trip kati ya routes za mlima Kilimanjaro dhumuni ni kufika kituo au camp moja kwenda nyingine. Furahia mazingira, nyoosha miguu.
Lushoto tips umeshapewa na wadau.
 
Morogoro unaweza kufikia mjini kuna lodge nzuri na hotel affordable kabisa,unaweza fanya hiking mount uluguru kule morning site kisha kanisa la kijerumani la kwanza then ukaogelee kule China water falls,hii hiking utaenjoy kuona mji wa Moro,kujifunza kuhusu strawberry na micro spices lakini pia kwa wale wanaopenda Camp hata kule juu zipo nyingi kama China Camp, unaweza kwenda Kinole kuna waterfalls nzuri,utafanya Agritourism pia na hata Kula vyakula vya kiluruguru,ukitoka kinole kuna Mkuyuni eneo poa kwa agritourism mwisho Matombo ukajionee maajabu ya kiluguru. Hii ni day trip tu.

Ukitoka pale mjini unaweza kwenda Mikumi ukaenjoy maana hotel ni nyingi na affordable pia,ukiwa mikumi unaweza Sogea uelekeo wa kama unaenda Iringa (Ruaha mbuyuni) wale wa mamba na Agritourism kwa wannaowish.
Unaweza kumaliza route yako kwa kwenda Udzungwa na ukachagua pa kulala aidha Msolwa Ujamaa au Mang'ula, utaenjoy hiking na utalii wa miguu pia lakini unaweza Sogea mpaka Mbingu caves na huko Ulanga kuna mambo mengi (shida ya hii route barabara sio rafiki muda wote wa mwaka).

Kwa wale wapenzi wa Nyama choma kwa wale wa utalii wa misosi unaweza kusogea Kuanzia Melela mpaka Doma utaenjoy sana.

Usisahau day trip nyingine ambayo ni very simple ni kutokea Mjini mpaka soko la mlali kisha mgeta (Hii ni sehemu ya juu,mkusanyiko wa vijiji vingi) huku ni kama lushoto tu,utaenjoy vitu vingi na experience tofauti kabisa kuanzia hali ya hewa mpaka vyakula pamoja na Agritourism ndani yake.

Karibuni Moro
 
Kwa nynda za juu kusini na Kusini;

Njombe unaweza kwenda kitulo ni mbuga ya Maua na ndege,sehemu moja nzuri kwa picha na hali ya hewa,hii ni makete.
Nyumbanitu na mashamba ya parachichi unaweza kuenjoy Njombe mjini.Njombe inafikika kwa gari kutokea Dar es salaam au Ndege ushukie Songwe,route zipo ila sio nyingi kwa uwanja wa Njombe.
Kuna route unaweza kutokea Kyela kwa boat ukaenda Ludewa ukarudi Njombe,hii ni zaidi ya utalii na unaweza kuunga Ludewa mpaka mbamba bay ukarudi Songea.


Mbeya kuna Tukuyu kuna lile ziwa la Mungu, pale Tukuyu kwa wale watu wa Misosi ni sehemu nzuri na katika kubadilisha hali ya hewa. Uzuri unaweza kutokea hapa ukaenda kitulo au ukatoka kitulo ukafika hapa.
Kyela kuna Beach nzuri Sana Sana na ziko Affordable sana ni wewe uchague kuanzia Ngonga au huku mwanzo kwenye landmark hotel. Mbeya na Songwe unaweza tumia gari au ndege kwa kutumia uwanja wa Songwe.

Songwe unaweza kutembelea Kimondo na wale wa hotel Utengule Hotel huku unakunywa kahawa Murua kabisa.

Iringa sio kuzungumza kwa hotel sio haba na ziko Affordable,kuanzia Ruaha ukamalizie Isimila na Agritourism ukiienjoy vizuri. Unaweza tumia gari au Ndege kutokea Dar au Dodoma.

Ruvuma ukiwa na usafiri private utaenjoy,hotel Songea mjini zipo,unaweza kutembelea mji mdogo wa historia Peramiho utaona mengi,kuna Milima Matogoro nao Una view nzuri lakini makumbusho ya majimaji na maeneo mengi yenye historia ya nchi hii na hayajulikani kabisaa
Mbinga kuna Liparamba na mwisho ziwani,bado kuna mengi ya kuyaona hapo katikati iwe katika kilimo au mazingira ya kuvutia mengi sana.Unaweza tumia gari bus au private kutokea Dar, unaweza kupitia iringa au Lindi.

Mtwara unaweza kupumzika Masasi mjini au Mtwara kutegemea na unakotaka kwenda.
Ukiwa Masasi unaweza kupanda Ile Milima na ukapata mtulizo wa kimawazo huku unaangalia mji,unaweza kutembelea Kanisa kongwe la Anglican,unaweza kwenda Mji mdogo wa Ndanda lakini pia ukamove mpaka Newala ambako ni juu ukajionea hali ya hewa ya tofauti na mazingira pia, hii route unaweza kutembelea maeneo ya hifadhi ya Mpombe na hata mto Ruvuma pia.
Mtwara mjini unaweza kuanzia mikindani pale kuna Old boma,ukaenda mjini kuna msangaa mkuu na mwisho Msimbati,kwa sasa Msimbati kuna beach lodge ya upekee hakika utaenjoy.
Ukiwa Mtwara unaweza kufanya evening walking beach au feri na kuenjoy samaki wa aina mbali mbali. Malazi sio ghari.Mtwara unaweza kutumia bus kutokea Dar au Ndege.

Lindi kwa ukweli kuna Option moja sababu option ya Lindi mjini unaweza kutokea Mtwara mjini ukaenda Lindi,kuna beach nzuri pale na kuna Rondo natural Reserve kule Rondo plateau,ni experience nzuri sana kisha unarudi Lindi, wale wa kilimo unaweza kuenjoy mashamba ya Nazi kule Ng'apa na mashamba ya chumvi kwa wingi,unaweza kumalizia beach ya mchinga (full white sand)
Kilwa. Hakuna asiyepajua kuna mengi na wengi ukweli hawaijui vizuri, unaweza kutokea moja kwa moja kwa gari tokea Dar es salaam.
 
Hotels mbona kawaida sana. Kuanzia $50 hotel zinaridhisha kabisa. Kutembea huna haja ya mwenyeji. Google sehemu za kutembelea ukiwa Dubai then unaenda mwenyewe tu tena usitumie taxi bei mbaya,tumia dubai metro iko straightfoward unafika sehemu nyingi sana kwa bei chee.
Niliwahi kwenda dubai kwa msaada wa www.booking.com nikatafuta hotel karibu na metro train station sikutumia taxi
 
IMG_7202.jpg

Wakuu twendeni na hii

Naona ni affordable
 
Soon nitawaandalia tour mbali mbali wanaJF. Tuwe na kitu chetu kinachotuunganisha kule Twitter kuna TOT Bonanza. Ila JF tuje na tours.
ukinitag kwenye hiyo thread ya tour nitashukuru sana Chief.
 
Back
Top Bottom