Wale tunaoanza Ujenzi 2022, Tupeane Start up Dondoo

Nas Jr

JF-Expert Member
May 15, 2018
5,356
2,000
Kaka sina pakuwekasite haina hata uzio.. unataka nikarundike hapo ziibiwe?? nyumba inataka nondo 130 kwako unataka nikanunue zote nijaze site?? kwani zinasukwa zote kwa siku moja??

Kwani mkuu una ID mbili?
 

jaxonjaxon

JF-Expert Member
Nov 21, 2014
215
250
Hongera mkuu, ukifika kwenye gypsum, kama utaweka gypsum nicheck 0713744842

Nina kiwanda cha mikanda, Kona na Maua ya Gypsum utapata Kwa bei ya kiwandani na tunakuletea ulipo.
Tupo Kibamba
 

alubati

JF-Expert Member
May 29, 2016
4,298
2,000
Wanasema asiye kujua akikuona barabarani anakujaji kwa muonekano wako.. ila natamani ungejua maish niliyo kulia nahata sasa una weza niona nina kazania kitu ambacho labda wewe huna ila kumbe wewe una mengi ambayo mimi sina.. mafano hapo una gusia ada za januari wakati mimi naumri huu sina mtoto na sinafuraha kwenye eneo hilo na umri huu.

Kama una baraka ya watoto na mke wwngine hatuna natuna 33yrs ila hatuna mke wala mtoto na kwenye eneo hilo hakukai sawa kabisa kumeshindikana.. sasa nikuulize ikiwa una mtoto na mke uambiwe unipe mimi hiyo mke na mtoto alafu mimi nikuachie nyumba hii ninayo jenga utakubali?
Aiseeee.....
 

AMADOGO

Senior Member
Jul 1, 2015
104
225
Nahisi mwenzangu Huna stress mimi ni ujenzi wa kwanza ramani yangu na yako hazitofautiani ila kuna pahala nime doubt fundi anasema foundation nitahitaji mifuko 400 eneo langu sio slope ni hapa shule ya msingi Ali hapi karibu na Moga primary school naomba nipe uzoefu mwenzangu foundation fundi kasema mifuko mingapi...maana mimi ukubwa wa jengo ni mita 21 kwa 21. Tafadhali nahisi anataka kunipiga...material zote nimeshakusanya kama wewe kasoro sementi nasita nahisi hakuna uhalisia...Tafadhali share uzoefu.
Mkuu tafuta fundi mwingine pia akupe hesabu pia. Mimi mwenyewe nilikuwa najenga maeneo hayo ya mbweni mpiji, fundi alinipa hesabu ya mifuko 405 ya cement nikawaza sana kama wewe. maana hakukuwa na uhalisia wowote. Nikapewa fundi mmoja hivi ni babu mtu mzima hiv akanipigia hasabu ya mifuko 245. Mungu saidia niliwapata mafundi wazuri NIKAWABANA na ikabaki mifuko 7.
 

kokudo

JF-Expert Member
Oct 26, 2010
2,001
2,000
2022
Mchanga wa tofari trip 6
Cement 25bags
target msingi tofari 900
 

Busara Kali

Member
Jan 7, 2021
48
125
Nina ramani inafanana na yako kwa maana ya chumba kimoja delux juu. Tathmini ya msingi nje ya tofali,kokoto na mchanga nimeambiwa ni 10m.
Kwako tathmini yako ikoje?
Na pesa ya ufundi imegawanyikaje ??
Nipe tips inisaidie kubargain
 

Nile_house_designs

Senior Member
Nov 13, 2020
112
250
Habarini wakuu, mukihitaji ramani nzuri msisite kututafuta kwa 0715477041, pia mwaweza tembelea link hii kujionea baadhi ya kazi zetu

 

The Sunk Cost Fallacy

JF-Expert Member
Dec 1, 2021
2,380
2,000
Uwanja wa futi 50 kwa 40 ambao ni square meter 200 unaonekana mdogo ila unapata kitu kama icho na ardhi yetu ni mchanga sio lazima sana kuweka mkanda chini ujenz wa gharama nafuu

Uwanja 2,500,000
Tofar 2700@900 = 2,430,000
cement 42@15000 =630000
nondo 18@2400 ni 432000
Komoto qubic moja 180000
maji 100000
fundi 1,200,000
kukod mbao za lint 75000
mbao za sahab 5@6000 = 30000
misumar 12000
usafir wa 40000

mchanga sijapigia hapo unajichimbia tu kwenye eneo lako dada alikuja na 12ml kesho kutwa tunapauaTotal ni kama 7,629,000/=

kupaua

mbao 2*2 ni 90*2800=252000
mbao 2*4 ni 90*4500=405000
fundi 1000,000
bati pc 87*22000=1,914,000
misumar ya bati & kench = 200000
kench waya 4@4000= 16000

total 3,762,000/=

jumla kuu 11,391,000/=

uharisia wa kweli ambao nauishi

hii ni kwa hesabu ya kisemvule mkuranga mchanga upo tu vifaa vya ujenz viwanda vipo mtaan nk 0744576060 View attachment 2070400 View attachment 2070399 View attachment 2070402

Sent from my SM-G965U using JamiiForums mobile app
Bati gani unatumia? Nyeupe au? Mbona gharama za kuezeka ndogo sana.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom