Wale tuliowahi kuishiwa nauli katika mishemishe tukutane hapa tuelezee tulifanyaje tukapata nauli

Mdau hiyo yako simple sana, Mnazi Mmoja to Mbezi Chamdoli, nimewahi kutoka Morogoro to Unguja dah ilikua noma sana, sitaki kukumbukaga kabisa konda wa Abood alinichukulia saa yangu na kwenye boat nilikamatwa Sina tiketi
Daa wee cha mtoto mimi nilikuwa natoka WEllingtone kwenda Amsterdam, sina hata shillingi wala visa! na mageti geti yao ile ya Umeme utakoma tu! nikaona isiwe tabu, kama nikifanikiwa kutoka Wellingtone nikifika Sydney tu nadai ukimbizi,

cha ajabu kwenye mageti ya ukaguzi yote nilipita km mtu mwema na salama nikafika Amsterdam kiulainiiii, na chakula nikala vizuri tu! na story za kujiamini za kumwaga !!

Kitu kimoja niligundua kama wewe unajua ni mtu wa kufa tu unakuwa na confidence za ajabu sana!!
 
Nawapenda sana wanaume maishani mwangu mmebalikiwa na mungu toka mbinguni katika pita pita zangu niliishiw nauli Mara nyingi nikapew nauli na wanaume kwa wakati tofauti bila kuombwa chochote kwenye mwili wangu wala no nilisaidiwa tu na bado naendelea kusaidiwa na wanaume
Umenikumbusha mbali mpaka nimelia hakuna watu wema hapa Duniani kama wanawake hasa wadada walinisaidia siyo nauli tu, mpaka kazi shule karo! Nyapu nisingekuwa nje ya nchi bila wao!!! ndo maana sitaki kabisa kumnyanyasa mwanamke! niko tayari nipigane na mumeo kama anakupiga mbelel yangu!

Basi nione in box ili tutengeneze kamuungano ketu kakusaidiana au unaonaje Duduke mwana JF hata kuoana kabisa siyo mbaya! tuna fitiana kwa kadri utakavo chagua nimesha pata watano hapa!
 
Daa wee cha mtoto mimi nilikuwa natoka WEllingtone kwenda Amsterdam, sina hata shillingi wala visa! na mageti geti yao ile ya Umeme utakoma tu! nikaona isiwe tabu, kama nikifanikiwa kutoka Wellingtone nikifika Sydney tu nadai ukimbizi,

cha ajabu kwenye mageti ya ukaguzi yote nilipita km mtu mwema na salama nikafika Amsterdam kiulainiiii, na chakula nikala vizuri tu! na story za kujiamini za kumwaga !!

Kitu kimoja niligundua kama wewe unajua ni mtu wa kufa tu unakuwa na confidence za ajabu sana!!
Wewe si ndo mkuu wa wachawi?
 
Wewe si ndo mkuu wa wachawi?
Jamani! jamani hee! mmeni QUOTE vibaya nilikuwa niko kwenye kundi la wachawi mkuu baba! sasa nimeacha! yaani huko ni full muziki na nilikuwa mchawi ambae sina umaarufu ila nilishiriki kuna watu huko wana usafiri hatari mbaya! aki pack hapo nje kibuyu chake cha usafiri hugusi!! kirahisi ni kama vx Prado,
 
Ilikuwa ni mwezi wa 12 tumefunga shule, Moshi Kilimanjaro, midterm, terminal zote sikwenda likizo maskani(Mbeya)..na annual nisiende haiwezekani...ile tumemaliza pepa ya mwisho ilikuwa civics, tumefika bwenini masela wanabeba matranka na mabegi yao mi nimekaa kitandani nawaza nafikaje Mbeya...Ghafla akili ikanijia nikakope kwa muweka hazina wa zone(hii unakuta kuna Lake Zone-hii ni zone ya wanafunzi wote wanaotoka kanda ya ziwa, Centra zone hii ni kanda ya kati yote, mimi nilikuwa mwana Southern Zone), kufika yule bro anasema hela zote zimekopwa amebakisha elfu 10. Na Moshi Mbeya ni elf 30(tulikuwa tunapanda Hood Bus), kipindi hiyo hela tunatumiwa kwa bus au posta, hakuna cha m-pesa wala tigo-pesa. Nikaona isiwe shida nikachukua ile elf 10 chap hadi dorm. Nikawaza ntafikaje hom, Nikalala asubuhi na mapema nikawahi Moshi mjini, sasa akili ya fasta na ile 10 mkononi nikaona nipite Dar kwa kaka..nikakata ticket Ngorika bus (Ngorika na Buffalo zilikuwa basi shindani sana) huyoo ndani ya basi...watu wanashuka Mombo kula mimi nimebaki kwenye basi napiga miayo tu.Tukafika Ubungo njaa inauma kinoma na sina hata cha simu na bro yuko Mabibo...nikachukua begi langu hadi Bigbrother, Big brother na hiace hadi Mabibo mahakama ya ndizi, nikaanza kumsakua mwenyeji wangu hadi saa 12 jioni ndo nakuja kumpata...sintosahau ule msoto
 
Mimi kutembea kwa mguu nilishazoea niashawahi tembea toka muhimbili Hadi ubungo way back Nika Nasoma shule moja hapo muhimbili
 
kaka acha tuu mm mwenyewe yasha nikuta niko nimepiga pamba kali nimetoka morogolo nafika ubungo sina ata mia sijui ata ilikuwaje akati nlikuwa na elf ishilini kwenye begi na natakiwa kwenda bunju
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom