Wale Tuliosoma sana O-level tukapelekwa shule za Vipaji, Huko Nature ikatuchagua

Mbaya zaidi pale unapoanza form 5 unakutana na mtu unamuuliza umefikia wapi kusoma anakuambia yote nime_cover mpk form six ninachosubiri necta tu wakati wewe hata topic wala vitabu vya kusoma hauvijui, hapo utajua kuwa dunia haina huruma .
 
Nimecheka sana! Pole yako, lakini nafuu yako wewe uliyesumbuka kwa wakati mmoja tu wa "advance".

Kiuhalisia, hizi shule (sijui kwa sasa) zilikuwa zinawakutanisha miamba hasa. Ukifika ulitakiwa kujiwekea wastani wako utakaokuwa unatambaa nao, na sio kushindana.

Anyway, kinachonisumbua ni namna Serikali imetenga hizi shule pasipo muendelezo wa hawa vijana. Wanaishia mulemule tu...
 
Daahhh, ur such a modaf.... good story teller. Umenikumbusha kitabu cha Shoe Dog cha Phil Knight. Kipindi kile ameenda Japan mara ya kwanza kufanya dili la biashara na Masamurai wa Kijapani. Funny sana.

Ila km ni story yako mwenyewe, hongera sana, ulikaza kinoma. Mi nlishindwa kabisa, nikakimbia Mock kukwepa fedheha, sikuwahi kufanya zile pepa za wanafunzi kutungiana (wenyewe wanaita FITNESS).

Pepa nyingi za shule nilikwepa. Mwisho kabisa nikaambulia 3 ya mwisho mwisho... Nikaenda zangu diploma...
 
Utoto raha sana. Yaani secondary unawaza nimekuwa wa ngapi, chuo unawaza kufaulu ichukue Gamba. Nature inaanza selection baada ya chuo. Pale ambapo mwanafunzi Bora (convocator) anaenda kuwa mratibh wa elimu, anavaa shati la kitenge limepaukaaa, halafu wazee wa makarai wanapeta tu na maisha.

Hapo ndio utajua tofauti ya IQ na EQ.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzee acha tu kuna jombaa alikuwa coet kapiga ilboru alituwashia moto first year kagonga 4.9 sijawai ona mimi uwezo wangu darasani haujawai kuwa na mashaka ila huyu jamaa ni noma ogopa mtu mnasoma wote darasani ila yeye ni kama mwalimu wenu anajua kila kitu ni balaa nashukuru tu mungu chuo sijawai kupenda kushindana kama seko dari uko ningekufa kwa presha. Kuna watu wamebarikiwa nyie

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyu ni invo bila shaka au

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeisahau Ilboru, nilikiwa na mjuba pale aiseeh ukiacha mistari aliyokiwa ananiimbisha, kipindi hicho yeye alikuwa anacheza na 90 kwenda juu, mwenyewe alikiwa anaita bouncing life yaani ananesanesa kati ya 100 na 90.

Sina hamu na wa kaskazini...

Alikiwa anajua Mahaba hatarii ila hakufanikiwa kuniambukiza ujiniasi wake mie nikaishia kidato cha pili... Poor Kasie.
Ilboru ndio Umenyeni, msuli wa huko ulikuwa waitwa "Ilboriasis Bundiata"...

Sijui kama wanafunzi wa sasa wangali wanalijua hilo jina...
 
Ma PCB ni magumu nyie ! Acheni kabisa. Biology kwangu ilikua ni mzigo, nikiwaza Ile biological science naishiwa na nguvu.

Nashukuru Mungu sikupata div.1 maana ingenilazimu kusoma Kada ya afya ambayo ni ngumu.
 
Ilboru ndio Umenyeni, msuli wa huko ulikuwa waitwa "Ilboriasis Bundiata"...

Sijui kama wanafunzi wa sasa wangali wanalijua hilo jina...

Sugar usipotee sana banaaa ona thathaa mpaka najikuta navaa barakoa mahala pasipo pake kwa kuona maandishi yako aahahahaha.

"Ilboriasis Bundiata".. sijui kwanini ila hilo jina nikilisikia huwa akili inatafsiri kile kiungo chenu pekee maalum bin mahsusi kwa kusonga....

Kumbe Sukari nawe ulipotia pale kitivo,..itakuwa mlisoma mwaka mmoja na aliyekuwa majuba wa Kasie nini eheheheheee...

K' Matata.
 
Ma PCB ni magumu nyie ! Acheni kabisa. Biology kwangu ilikua ni mzigo, nikiwaza Ile biological science naishiwa na nguvu.
Nashukuru Mungu sikupata div.1 maana ingenilazimu kusoma Kada ya afya ambayo ni ngumu.
Achen unafki jaman..yan mungu huyu anatabu sana..yan mtu et anashukuru hakupata div1....?kweel?...kwel? Broo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Achen unafki jaman..yan mungu huyu anatabu sana..yan mtu et anashukuru hakupata div1....?kweel?...kwel? Broo

Sent using Jamii Forums mobile app
Kaka najua uwamini , lakini kwa ninachofanya sasa hivi, nisingeweza kufanya kama ningepata division 1 maana ningeendeshwa na presha za watu pamoja na mikumbo kwenye fani ambayo isingenipa furaha kama ninayoipata sasa.

Nimeshuhudia washkaji zangu wengi jinsi presha za matokeo zilivyowapeleka kwenye fani wanazozijutia.
 
umesoma nin mwenzetu ambacho hakina presha?
 
Back
Top Bottom