Wale Tuliosoma sana O-level tukapelekwa shule za Vipaji, Huko Nature ikatuchagua

Pantomath

JF-Expert Member
Jan 4, 2019
781
3,204
Ni ngumu kuelewa/ kuamini ila kati ya watu waliojutia kusoma sana na kufaulu vizuri ni mimi.

Nilitumia nguvu nyingi kusoma O-level, na kweli nguvu zile hazikwenda bure, Nilichomoka na div 1.11, shule ya hovyo hovyo na hakuna aliyewahi pata hio tangu ianze.

Ilikua shangwe, kitu ambacho nilikuja kushukuru baadae sikuonesha masifa mtaani kipindi nilivyo faulu form 4 na hata watu wengi hawakujua.

Mzee baba nikapelekwa PCB shule kubwa ya vipaji maalum, nilifurahi sana nisijue kumbe nimejipeleka bucha na panga langu.

Sasa kule ndio Nature ika ni select, test ya kwanza nikala za uso, ndio nilifaulu lakini nahisi nilikua wa mwisho, maana kila unayemwona Kapasua si mchezo, ya pili ile nili confirm kabisa ile nimefunga kitasa.

Sikuamini macho na akili yangu, kama ni mimi wa kufunga dimba a.k.a kuzima taa? ingawa bado nipo juu ya wastani,

Sasa kuna Mwana nakaa naye karibu alikua na 66 yake akajua sijui ndio wa kwanza, bwana akaenda kwa vipanga wa darasa eti kuwachora sababu alisikia wakilalamikiana kuwa nimefeli, asijue kuwa ni kufeli katika next level ya battle lao wenyewe yeye alidhani ni wastani akajipeleka.

Anafika huko mwenye ndogo ana 93, alirudi taratibu kinyume nyume akakaa kwenye dawati akainama nikamwona anatafuna mtihani wake, Nilikua kila nikimwona nakufa kwa kicheko, Hakumaliza week akahama.

Nikajiuliza hawa watu ni wa namna gani? Ni kweli nilizembea sana katika usomaji zaidi hata ya vipanga wenyewe na mbaya zaidi kumbe wana walipiga twitions karibuni topic zote za form V kabla hata ya kuanza shule, lakini hili gap ni kubwaa, zikaja test nyingine nazo ni kukimbizwa tu.

Nikaona hapa nitaaibika mzee mzima, nikaanza kusoma upepo, uzuri Science hasa PCB tulikua wengi, nikagundua kuna mananga kama mimi na wengine ni zaidi yangu tuliofaulu kwa sifa.

Nikasema sasa hawa ndio guard yangu huku nyuma, nisije nikawa wa mwisho, pale ndio nikafufua ule msuli tena.

kwa kweli awamu hii Matokeo hayakuendana na Jitihada, Binafsi chemistry ndio ilinitesa zaidi kwenye mitihani, ila kwenye usomaji ni kawaida tofauti na physics iliyokua ngumu kwenye usomaji ila kwenye mtihani mambo kiasi yanashuka.

Zile njemba zilizo jaaliwa yaani kwao kila upande akishika kalamu ni kama inajiandika, unamwita mtu akuelekeze anakuja (uzuri sio wachoyo na uzuri zaidi mimi nilikua rafiki wa kila mtu) anakuelekeza speed anayoshuka nayo unaishia kuguna tu, kuna vitu unashindwa kuuliza maana unahisi atashangaa huyu jamaa amekujaje huku?..

Maisha yangu katika usomaji yalikua magumu sana, japo ya nje yalikua mazuri na ya furaha sana. Nilijitahidi sana kukaza, maajabu ambayo niliyafanyaga ni kuwa wa 8, baada ya hapo nikatupwa na sijawahi hata kuikaribia tena. Maana ile nafasi niliipata baada ya kujitesa sana.

Kwa kweli hapa nikakata tamaa, Tofauti na O-level masomo yalikua marahisi na unaokimbizana nao ni warahisi.

Huku masomo ni Jiwe, unaokimbizana nao ni Nondo, yaani huna pa kuchomokea. Nikaamua mimi ni kusoma tu na kufaulu hizi higher grades niwachie watabe, Ila hawa mananga wenzangu nihakikishe hawanipiti, basi...

Tatizo wengi walikua na roho nyepesi, wengi walihama, wengine walibadili Comb, kwahiyo kadiri wanavyopungua mimi nakaribiwa, maana anaacha nafasi moja nyuma, ikawa kila akiondoka mmoja naongeza kasi na wengi walikua wanatoka hizi St...... kuna jamaa mmoja yeye alizunguka round about kbsa, Hatukujua alipitia wapi na hatujawahi mwona tena. alituachia tu tranka lenye mazaga kama yote.

Mwisho wake nika ambulia 2 iliyochoka, wazee kama kawa ni div 1 na hata kwenye Top 10 walikuwepo, japo wengine walizingua pia.

Selection inatoka Natakiwa kwenda SUA tena, nikaona huu ni ujinga sasa, si ndio kule kule na watu wale wale, wengi sana naenda nao tena Course Moja, Yaani ilifika hatua nafikiria kuwakwepa sasa lakini wao walikua wanakubali sana kampani yangu.

Raha ya kusoma, ni kufaulu kadiri ya jitihada na mwishowe kupata kile unachotafuta...
kinyume na hapo ni msalaba, na mm elimu yangu ya advance ni niliiona kero...pale ndio niliamini kuna watu wamejaaliwa akili za darasani, sisi wengine tunasogeza tuu gurudumu..

Mwisho, ni matamanio makubwa sana kwa mzazi kua na mtoto mwenye jitihada darasani na baadae maisha kwa ujumla, na kwa kweli inaleta furaha sana, Pia nahisi uwezo wa mtoto kupambanua mambo umeunganika na mambo flani kutoka kwa wazazi na malezi labda.

Usione kila kijana mtaani akirudi likizo akakutajia shule nzuri na kubwa anayosoma ukasema kimoyomoyo huyu ni kichwa, Wengine ni wazunguka round about tuu, na wanachopitia huko wanakijua wenyewe.

Mwanao kama ni Nanga, usimlazimishe elimu unamtesa, ukimpatia ile basic ya kusoma, kuhesabu na kuandika ambayo ndio elimu kuu inatosha mtafutie njia nyingine, Narudia tena unamtesa mwanao, unamjengea hofu na dhana ya kushindwa kuanzia utoto matokeo yake anakua nayo na kujihisi yeye si chochote panapo wenzake.

Msikilize, msapoti kwa njia nzuri anayoihitaji, mfanye mshindi tangu utoto, Ushindi sio Darasani tu, mfanye Mshindi wa maisha.

Tusidanganyane, hakuna shule za vipaji maalum, ni shule za waliosongoka na kufaulu vizuri
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huwa inaumiza sana.
Unajipindaaaa unafaulu kiaina lakini wa mwisho nakumbuka matokeo yalivyotoka aliniangalizia jembe letu wakati ananipa taarifa kanipa kinyonge sana wakati nimefaulu vizuri tu lakini ndo wa mwisho nwisho tena.

Kusoma na watu wenye vipaji na wale wanaoanza advance wameshamaliza topics zote za form 6 wenyewe wanaita kucover inataka moyo.

Wewe unaingia class kujifunza mwenzako alishasoma topics zote ana fanya kureview past papers.

mama wawili
 
Siku zote kuna mdogo wangu(yupo o level) huwa namuambia kuwa kusoma sio kushindana na mwanafunzi mwenzio.

Kusoma unatakiwa ushirikiane na mwanafunzi mwenzio uushinde mtihani wa mwalimu.

Unapotaka kushindana na mwanafunzi mwenzio ukumbuke mtihani pia unakusubiri ushindane nao.

Namuambia sana kuwa unaposoma kwa kushindana unambweteka ikiwa tu wale uliotaka wasikupite hawajakupita.

Mwenzio kapata 40 mock wewe umepata 50 mock unafurahi kwa sababu hajakupita na unasahau kuhuzunika kuwa hiyo 50 yako bado ni ndogo sana katika ufaulu.

Namuambia sana kuwa Necta hawaangalii umempita fulani na fulani darasani,necta wanaangalia umejibu nini.

Wakati anaingia form one nilimuambia kuwa hausomi kww ajili ya mtihani wa midterm bali wewe unasoma kwa ajili ya mtihani wa necta form four,kwa hiyo elekeza nguvu zako ukifocus kwenye mtihani wa form four.

Soma sasa hivi form one kwa msuli wa maandalizi ya mtihani wa necta form four,usijowekee mindset ya kuwa unasoma kwa ajili ya mtihani wa mwezi wa sita,it is a bad mindset.

Ukisoma kwa malengo la kuushinda mtihani wa mwalimu hauta bweteka kabisa.

Dogo hashindani na mtu,hizo ni mindest mbovu huwa namuambia.

Kusoma ni katika maisha na mtihani ninchangamoto.
na maisha(kusoma) hayana ushindani unatakiwa uzishinde changamoto(mtihani)
 
Mleta mada unanikumbusha mbali sana.

Sikwenda shule ya vipaji maalum ila ni shule flani watu wake na shule yenyewe huji-grade kama vipaji maalum.

Nilipata tabu sana, narudia tena A'level nilipata tabu mnoooo

Wale wenzangu namimi walikuwa wanaji-boost kwa kwenda mchikichini kupiga kitabu kwa akina Mbuga chemistry, sijui Muddy Physics
Sasa mimi kijijin hata nikimwambia mzee nataka hela ya tuition anaona kama utapeli maana huko mwanzo sikuwahi kusoma tuition, akijitahidi sana anatuma 20K kupitia NMB (enzi hizo mpesa wala tigopesa hazijaanza) sasa ukienda kuitoa inatoka 15K hiyo utasoma sub-topic mbili za Physical chemistry hela imekata, bado nauli bado kula mihogo.


Katika kusoma kwangu sitaisahau A'level japo nilifaulu kwenda kile chuo wanaita cha Taifa lakini A'level sina hamu nayo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilisoma kama wewe shule ya kata na nilikimbiza balaa, nikajiona mwamba kumbe nipo na vilaza.... o’level kwangu ilikuwa elimu rahisi na nilisoma kwa kufurahia sana.

Nikafaulu vizuri kwenda advance, japo sio ‘spesho’ ila nilikutana na watabe walionifunza kuwa mimi ni kilaza tu.... picha linaanza ile kuripoti shule tu unaambiwa watu ‘wame-cover’.

Test zote za mwanzoni nilichezea marks karibia na umri wangu, nimekuja kurudi relini form six huko na kwa ajabu zaidi nilifaulu vizuri necta nikajiunga Chuo cha ndoto ya kila mtu [PCB].... huko ndo nikagundua kuwa nilikuwa sijui nataka nini.

Eti chuo bata weee thubutu, nikapoteza mzuka wa maisha na sikuwa tena interested na nilichochagua kusomea.... nimemaliza japo kwa mbinde ila nikapiga chini ili niishi maisha yangu.

A’level ni elimu ninayoijutia ilinipeleka sana, Chuo kitu pekee nilifurahia ni boom tu.... ajira sitaki kisa nadaiwa mamilioni bodi ya mikopo.
 
Haya sasa ndugu zangu na mimi tunaosoma tu hiyo mikombi na hatujawahi fika tupo..??
hizo PCB sijui HKL wengine tunazisomea humu😅

O level ilitosha kabisa kuniambia haya wewe kenge basi huko hupawezi utaenda kufa kibudu ishia hapa!..

Ngoja nipige na nyungu ya mwisho nivute kiti niwasome kina PCB..
 
Kuna mtu aliyemaliza form six mwaka 2013 mwaka ambao JKT ilirudishwa.. Huwa nakaa najiuliza Ivi hiyo mitihani walisaisha au walifanya nini.

Maana matokeo ya mtihani wa mwaka huo yanabaki kuwa historia katika nchi hii. Ni mabaya haijawahi kutokea kabisa.

Pamoja na kuwa katika shule ya vipaji maalumu matokeo kiujumla yalikuwa mabovu sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanafunzi wengi waliopasua O-LEVEL walifeli Advance kwa sababu ya kujiamini kupitiliza..wakifikiria maisha ni yaleyale waliyoyaacha huku chini.

Hivyohvyo na wengine wanapasua vizuri advance ila wakifika chuo wanapoteana..

Sikilizeni madogo..maisha ya shule ni MARATHON..ukimaliza level moja tunaanza upyaaa kwny level nyingine..hatujali ulipata ngapi huko ulikotoka..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom