Wale Tuliosoma sana O-level tukapelekwa shule za Vipaji, Huko Nature ikatuchagua

Yeah mtoto umkimpela sentikunani olevel advance amalize huko huko ukimleta govt unampoteza

Kuna dogo mmoja akitoka na one ya 13 Senti kunani akapelekwa mzumbe advance akapata three ya 15 darasani wa mwisho dally

Sent using Jamii Forums mobile app
Jiran angu yey alisoma st flan iv o level, akatok na 1 ya 14 akaenda PCB Minaki uwiiiiiiih, et necta f6 katok na 3 ya 14, sijaamin hat kidogo, the way mzaz wake alivokuwa anajigamba mmmmh.
 
Kuna mtu aliyemaliza form six mwaka 2013 mwaka ambao JKT ilirudishwa.. Huwa nakaa najiuliza Ivi hiyo mitihani walisaisha au walifanya nini.

Maana matokeo ya mtihani wa mwaka huo yanabaki kuwa historia katika nchi hii. Ni mabaya haijawahi kutokea kabisa.

Pamoja na kuwa katika shule ya vipaji maalumu matokeo kiujumla yalikuwa mabovu sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Unasema form 6 mwaka huo kuna mwaka 2012 form 4 aisee huyu mama alifanya sijui maajabu gani aisee nakumbuka kuna jamaa alipata 4 ya 28 kwenye kubustiwa akaja kupata 3 ya 25 mimi nilie pata 4 ya 27 nikabaki hapo hapo wala siku bustiwa sijui walinisahau nyau wale sina hamu nao shwain kabisa wakati nilijua nitapanda kwenda 3 ya 24 uko
 
Mbna kuna mwingne yey alipata 4 ya 26, matokeo yalibaki vilevile post zikaja akachaguliwa advance saiv kashamaliza degree ake. Yupo tu mtaan anasubir ajira
 
nimecheka ila shule shikamoo
Haya sasa ndugu zangu na mimi tunaosoma tu hiyo mikombi na hatujawahi fika tupo..??
hizo PCB sijui HKL wengine tunazisomea humu

O level ilitosha kabisa kuniambia haya wewe kenge basi huko hupawezi utaenda kufa kibudu ishia hapa!..

Ngoja nipige na nyungu ya mwisho nivute kiti niwasome kina PCB..
 
Ni ngumu kuelewa/ kuamini ila kati ya watu waliojutia kusoma sana na kufaulu vizuri ni mimi.

Nilitumia nguvu nyingi kusoma O-level, na kweli nguvu zile hazikwenda bure, Nilichomoka na div 1.11, shule ya hovyo hovyo na hakuna aliyewahi pata hio tangu ianze.

Ilikua shangwe, kitu ambacho nilikuja kushukuru baadae sikuonesha masifa mtaani kipindi nilivyo faulu form 4 na hata watu wengi hawakujua.

Mzee baba nikapelekwa PCB shule kubwa ya vipaji maalum, nilifurahi sana nisijue kumbe nimejipeleka bucha na panga langu.

Sasa kule ndio Nature ika ni select, test ya kwanza nikala za uso, ndio nilifaulu lakini nahisi nilikua wa mwisho, maana kila unayemwona Kapasua si mchezo, ya pili ile nili confirm kabisa ile nimefunga kitasa.

Sikuamini macho na akili yangu, kama ni mimi wa kufunga dimba a.k.a kuzima taa? ingawa bado nipo juu ya wastani,

Sasa kuna Mwana nakaa naye karibu alikua na 66 yake akajua sijui ndio wa kwanza, bwana akaenda kwa vipanga wa darasa eti kuwachora sababu alisikia wakilalamikiana kuwa nimefeli, asijue kuwa ni kufeli katika next level ya battle lao wenyewe yeye alidhani ni wastani akajipeleka.

Anafika huko mwenye ndogo ana 93, alirudi taratibu kinyume nyume akakaa kwenye dawati akainama nikamwona anatafuna mtihani wake, Nilikua kila nikimwona nakufa kwa kicheko, Hakumaliza week akahama.

Nikajiuliza hawa watu ni wa namna gani? Ni kweli nilizembea sana katika usomaji zaidi hata ya vipanga wenyewe na mbaya zaidi kumbe wana walipiga twitions karibuni topic zote za form V kabla hata ya kuanza shule, lakini hili gap ni kubwaa, zikaja test nyingine nazo ni kukimbizwa tu.

Nikaona hapa nitaaibika mzee mzima, nikaanza kusoma upepo, uzuri Science hasa PCB tulikua wengi, nikagundua kuna mananga kama mimi na wengine ni zaidi yangu tuliofaulu kwa sifa.

Nikasema sasa hawa ndio guard yangu huku nyuma, nisije nikawa wa mwisho, pale ndio nikafufua ule msuli tena.

kwa kweli awamu hii Matokeo hayakuendana na Jitihada, Binafsi chemistry ndio ilinitesa zaidi kwenye mitihani, ila kwenye usomaji ni kawaida tofauti na physics iliyokua ngumu kwenye usomaji ila kwenye mtihani mambo kiasi yanashuka.

Zile njemba zilizo jaaliwa yaani kwao kila upande akishika kalamu ni kama inajiandika, unamwita mtu akuelekeze anakuja (uzuri sio wachoyo na uzuri zaidi mimi nilikua rafiki wa kila mtu) anakuelekeza speed anayoshuka nayo unaishia kuguna tu, kuna vitu unashindwa kuuliza maana unahisi atashangaa huyu jamaa amekujaje huku?..

Maisha yangu katika usomaji yalikua magumu sana, japo ya nje yalikua mazuri na ya furaha sana. Nilijitahidi sana kukaza, maajabu ambayo niliyafanyaga ni kuwa wa 8, baada ya hapo nikatupwa na sijawahi hata kuikaribia tena. Maana ile nafasi niliipata baada ya kujitesa sana.

Kwa kweli hapa nikakata tamaa, Tofauti na O-level masomo yalikua marahisi na unaokimbizana nao ni warahisi.

Huku masomo ni Jiwe, unaokimbizana nao ni Nondo, yaani huna pa kuchomokea. Nikaamua mimi ni kusoma tu na kufaulu hizi higher grades niwachie watabe, Ila hawa mananga wenzangu nihakikishe hawanipiti, basi...

Tatizo wengi walikua na roho nyepesi, wengi walihama, wengine walibadili Comb, kwahiyo kadiri wanavyopungua mimi nakaribiwa, maana anaacha nafasi moja nyuma, ikawa kila akiondoka mmoja naongeza kasi na wengi walikua wanatoka hizi St...... kuna jamaa mmoja yeye alizunguka round about kbsa, Hatukujua alipitia wapi na hatujawahi mwona tena. alituachia tu tranka lenye mazaga kama yote.

Mwisho wake nika ambulia 2 iliyochoka, wazee kama kawa ni div 1 na hata kwenye Top 10 walikuwepo, japo wengine walizingua pia.

Selection inatoka Natakiwa kwenda SUA tena, nikaona huu ni ujinga sasa, si ndio kule kule na watu wale wale, wengi sana naenda nao tena Course Moja, Yaani ilifika hatua nafikiria kuwakwepa sasa lakini wao walikua wanakubali sana kampani yangu.

Raha ya kusoma, ni kufaulu kadiri ya jitihada na mwishowe kupata kile unachotafuta...
kinyume na hapo ni msalaba, na mm elimu yangu ya advance ni niliiona kero...pale ndio niliamini kuna watu wamejaaliwa akili za darasani, sisi wengine tunasogeza tuu gurudumu..

Mwisho, ni matamanio makubwa sana kwa mzazi kua na mtoto mwenye jitihada darasani na baadae maisha kwa ujumla, na kwa kweli inaleta furaha sana, Pia nahisi uwezo wa mtoto kupambanua mambo umeunganika na mambo flani kutoka kwa wazazi na malezi labda.

Usione kila kijana mtaani akirudi likizo akakutajia shule nzuri na kubwa anayosoma ukasema kimoyomoyo huyu ni kichwa, Wengine ni wazunguka round about tuu, na wanachopitia huko wanakijua wenyewe.

Mwanao kama ni Nanga, usimlazimishe elimu unamtesa, ukimpatia ile basic ya kusoma, kuhesabu na kuandika ambayo ndio elimu kuu inatosha mtafutie njia nyingine, Narudia tena unamtesa mwanao, unamjengea hofu na dhana ya kushindwa kuanzia utoto matokeo yake anakua nayo na kujihisi yeye si chochote panapo wenzake.

Msikilize, msapoti kwa njia nzuri anayoihitaji, mfanye mshindi tangu utoto, Ushindi sio Darasani tu, mfanye Mshindi wa maisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
Special school.without proper preparation was a waste of time

Mimi ji mhanga wa sepcial school ... Ndio tulianzisha

What a waste
 
Advance shikamoo🙌, PCB shikamoo+

Nilitoka primary with a very strong foundation(though it was based on spoon feeding), nilichaguliwa kujiunga moja ya shule za vipaji maalum.
Uspecial wote uliishia form one na form two, wajuba walivokuja kujua kingereza vzr plus their hardwork, tuliotoka english medium vile tumezoea kutafuniwa, aisee tulikimbizwa vibayaa mno.
Inshaallah, form 4 nikabahatika kupata div. 1 ya mwishoni, nikachaguliwa PCB miono high school.

Niliipiga chini miono nikaamua niende private, just because nilijijua kabisaa bila spoon feeding nitapigwa K.O, besides nilihitaji kuregain foundation yangu iliyopotea.

Movie inaanza, naingia shule bila kusoma tuition halafu nimevuta week kadhaa.
Nilipitia kipindi kigumu sanaa, nimeteseka sanaa.
Nakumbuka kuna kipindi elimu ilichanganya nikawa siwezi kulala for more than two hours, ndo ile unalala saa sita, saa nane ushaamka voluntarily bila kulazimishwa na mtu.
Ilifikia kipindi roommates wangu wakaanza kudai nikiamka asubuhi huwa nanyata ili wao wasiamke, kumbe mimi naamka mida mibovu

PHYSICS: Nakumbuka paper ya kwanza nilipata 2%,nakumbuka vyema teacher aliniambia "ivi kaka katika maswali yote kumi ulishindwa kupata angalau nusu nusu atleast upate 5% mtihani mzima"
Pamoja na juhudi zote na spoon feeding yote, mpaka form five inaisha sikuwahi kupata above 40%.
Nilivoingia form six atleast nikawa napata 40+ on regular basis. Niliwah kupata above 50%( but not above 60) just twice. Mungu huwa hamtupi mja wake imekuja NECTA nikajipatia C(60% +) yangu swafii

CHEMISTRY: Nikiwa form five mwanzoni ilikuwa nzuri kiasi chake, hali ilikuwa mbaya mwishoni kiasi cha kupata F tahossa form five.
Nilivoingia form six juhudi zilizaa matunda, especially in organic chemistry and physical (Ngaiza popote ulipo agiza pepsi big) . Aisee i was obsessed with organic chemistry na niliijua haswaa, kwenye zile conversions nilikuwa mpaka naweka alternative mechanisms kwenye mitihani.
One of my teachers assured me nitapata A kwenye necta, hii ni baada ya kubutua A kwenye pre-necta.
But surprisingly niliishia kupata C ya necta.

BIOLOGY: Hili somo ni kibonde ya watu wengi, especially kama unaweza kukariri. Haijawahi kunipa tabu hata kidogo.

All in all kama wewe cyo kipanga( wale ambao wanaweza kusolve swali la physics ambalo hawajawahi kukutana nalo😅😅😅), kufaulu PCB ni bahati sanaa.. Lkn bahati inaenda kwa mtu anayedeserve
Inabidi uteseke vya kutosha so that u will deserve hako kabati
 
Mimi Nikiwa Special sjawah Pata zaidi ya 29percent ,nilivokua olevol Pepa nyingi hasa za 100. Sasa watoto wanaulizaga baba mbona Pepa za advance hatuzioni. Jibu ni moja "niliibiwa trunker kwenye train wakati nmemalza mtihani narud nyumbani " sitaki kukumbuka mchosho wa advance ni full stress..kila siku najiuliza ka one ka tisa nilikapataje form six?,,,
 
Advance shikamoo, PCB shikamoo+

Nilitoka primary with a very strong foundation(though it was based on spoon feeding), nilichaguliwa kujiunga moja ya shule za vipaji maalum.
Uspecial wote uliishia form one na form two, wajuba walivokuja kujua kingereza vzr plus their hardwork, tuliotoka english medium vile tumezoea kutafuniwa, aisee tulikimbizwa vibayaa mno.
Inshaallah, form 4 nikabahatika kupata div. 1 ya mwishoni, nikachaguliwa PCB miono high school.

Niliipiga chini miono nikaamua niende private, just because nilijijua kabisaa bila spoon feeding nitapigwa K.O, besides nilihitaji kuregain foundation yangu iliyopotea.

Movie inaanza, naingia shule bila kusoma tuition halafu nimevuta week kadhaa.
Nilipitia kipindi kigumu sanaa, nimeteseka sanaa.
Nakumbuka kuna kipindi elimu ilichanganya nikawa siwezi kulala for more than two hours, ndo ile unalala saa sita, saa nane ushaamka voluntarily bila kulazimishwa na mtu.
Ilifikia kipindi roommates wangu wakaanza kudai nikiamka asubuhi huwa nanyata ili wao wasiamke, kumbe mimi naamka mida mibovu

PHYSICS: Nakumbuka paper ya kwanza nilipata 2%,nakumbuka vyema teacher aliniambia "ivi kaka katika maswali yote kumi ulishindwa kupata angalau nusu nusu atleast upate 5% mtihani mzima"
Pamoja na juhudi zote na spoon feeding yote, mpaka form five inaisha sikuwahi kupata above 40%.
Nilivoingia form six atleast nikawa napata 40+ on regular basis. Niliwah kupata above 50%( but not above 60) just twice. Mungu huwa hamtupi mja wake imekuja NECTA nikajipatia C(60% +) yangu swafii

CHEMISTRY: Nikiwa form five mwanzoni ilikuwa nzuri kiasi chake, hali ilikuwa mbaya mwishoni kiasi cha kupata F tahossa form five.
Nilivoingia form six juhudi zilizaa matunda, especially in organic chemistry and physical (Ngaiza popote ulipo agiza pepsi big) . Aisee i was obsessed with organic chemistry na niliijua haswaa, kwenye zile conversions nilikuwa mpaka naweka alternative mechanisms kwenye mitihani.
One of my teachers assured me nitapata A kwenye necta, hii ni baada ya kubutua A kwenye pre-necta.
But surprisingly niliishia kupata C ya necta.

BIOLOGY: Hili somo ni kibonde ya watu wengi, especially kama unaweza kukariri. Haijawahi kunipa tabu hata kidogo.

All in all kama wewe cyo kipanga( wale ambao wanaweza kusolve swali la physics ambalo hawajawahi kukutana nalo), kufaulu PCB ni bahati sanaa.. Lkn bahati inaenda kwa mtu anayedeserve
Inabidi uteseke vya kutosha so that u will deserve hako kabati
poleeeeeeeeeh san lol, chezea special weyeeeeeeeeh
 
Huwa inaumiza sana.
Unajipindaaaa unafaulu kiaina lakini wa mwisho nakumbuka matokeo yalivyotoka aliniangalizia jembe letu wakati ananipa taarifa kanipa kinyonge sana wakati nimefaulu vizuri tu lakini ndo wa mwisho nwisho tena.

Kusoma na watu wenye vipaji na wale wanaoanza advance wameshamaliza topics zote za form 6 wenyewe wanaita kucover inataka moyo.

Wewe unaingia class kujifunza mwenzako alishasoma topics zote ana fanya kureview past papers.

mama wawili
Huhuhuhuh wapi hiyooooooh? Mam killey au wosooooooooh?
 
HAMNA MZEE KUNA 2007 acsee ILE PAPER HAIJAWAH TOKEA TENA
Ha ha ha.... Mkuu huu mwaka ulikua wa shetani sio bure!! Ila sio mbaya, nilidunda PCM na point 11 zangu maisha yakaendelea.

Picha linaanza hakuna mwalimu wa Physics wala Mathematics, tunaambiwa wanangojwa waliotoka Mkwawa huko tuwe na subira. Ticha wa chemistry ni msanii kufa, ilifikia mahali akatutafutia mshikaji aliyeua six apige topic ya organic ila kwa hela zetu. Teacher wa Mathematics alivyofika kwa kweli alipambana sana na alicover topic zote. Physics teacher alitutema maana aliona gari zishapoteza muelekeo
 
Unasema form 6 mwaka huo kuna mwaka 2012 form 4 aisee huyu mama alifanya sijui maajabu gani aisee nakumbuka kuna jamaa alipata 4 ya 28 kwenye kubustiwa akaja kupata 3 ya 25 mimi nilie pata 4 ya 27 nikabaki hapo hapo wala siku bustiwa sijui walinisahau nyau wale sina hamu nao shwain kabisa wakati nilijua nitapanda kwenda 3 ya 24 uko
Ila. 27 kwamwaka ule ulikuwa ufaulu mzuri tu.. Nadhani ulipata chuo mkuu...ety
 
Naona PCB na PCM zimejaa Sir tuliopiga HKL tunakomenti wapi?? Ila kwa sasa tumegeuka maHR n.k
 
Nilipata bahati ya kuwa mmoja wa wanafunzi wenye vipaji maalum, nilijiona wa kawaida mpaka nilipomaliza chuo! Kukubalika kwa Kazi ninayoifanya ndiyo inanifanya nikubali hakika Mungu alinipa kipaji!
Asante Mungu!
 
Ha ha ha.... Mkuu huu mwaka ulikua wa shetani sio bure!! Ila sio mbaya, nilidunda PCM na point 11 zangu maisha yakaendelea.
Picha linaanza hakuna mwalimu wa Physics wala Mathematics, tunaambiwa wanangojwa waliotoka Mkwawa huko tuwe na subira. Ticha wa chemistry ni msanii kufa, ilifikia mahali akatutafutia mshikaji aliyeua six apige topic ya organic ila kwa hela zetu. Teacher wa Mathematics alivyofika kwa kweli alipambana sana na alicover topic zote. Physics teacher alitutema maana aliona gari zishapoteza muelekeo
dah mkuu ulinyuka ... div 2 ya 11 kwa ile pepa mi nilisov kama past paper bado nikaona ngumu
 
Nilisoma kama wewe shule ya kata na nilikimbiza balaa, nikajiona mwamba kumbe nipo na vilaza.... o’level kwangu ilikuwa elimu rahisi na nilisoma kwa kufurahia sana.

Nikafaulu vizuri kwenda advance, japo sio ‘spesho’ ila nilikutana na watabe walionifunza kuwa mimi ni kilaza tu.... picha linaanza ile kuripoti shule tu unaambiwa watu ‘wame-cover’.

Test zote za mwanzoni nilichezea marks karibia na umri wangu, nimekuja kurudi relini form six huko na kwa ajabu zaidi nilifaulu vizuri necta nikajiunga Chuo cha ndoto ya kila mtu [PCB].... huko ndo nikagundua kuwa nilikuwa sijui nataka nini.

Eti chuo bata weee thubutu, nikapoteza mzuka wa maisha na sikuwa tena interested na nilichochagua kusomea.... nimemaliza japo kwa mbinde ila nikapiga chini ili niishi maisha yangu.

A’level ni elimu ninayoijutia ilinipeleka sana, Chuo kitu pekee nilifurahia ni boom tu.... ajira sitaki kisa nadaiwa mamilioni bodi ya mikopo.
Bila shaka we n dr
 
nilikuwa wa kwanza kiwilaya na wa 4 kimkoa, nikapangiwa ilboru aisee, skuamin nlichokikuta mana wana walikuw na moto balaa. Form one mtu kitabu cha oxford hakimtoshi anapiga BC kurwa mipawa popote ulipo heshima yako. Matkeo ya kwanza nlikuwa mtu wa 100 japo ni wastan wa two,niliumia sana bt ilivyofika form two katkat mamb ndo yakakaa level, ila nilipata tabu sana, nilitmia nguvu nyingi sana kukabiliana nao wale wadau. Askwambie mtu bhana hiz shule zina raha yake asee.
ntakumbuka mafundi nlosoma nao
ILBORU high school..
madulu lukombe popote ulipo...ww jamaa ulikuwa fundi sana na wengine kina hyera, hilmi Abdallah shaikh, .

Raha ya hiz shule unakuwa unaijua siasa sana, walosoma wanaelewa nn namaanisha..
miongoni mwa walosoma pale
1. Tundu lissu
2. Mwigulu nchemba
3. Sumaye
4. Dr Christopher cyrilo
5. Calvin marambo na wngn wengi.
 
Hu

Calvin marambo nimeona amemaliza Bachelor degree in biochemistry, mwaka jana Kama sikosei.
 
Back
Top Bottom