Wale tuliokutana na adhabu toka kwa wanajeshi tuambie ilikuwaje

Kuna dingi mmoja cha pombe tulikuwa tunaishi nae kota kwenye chuo kimoja. Kama kawaida ya walevi kurudi ni mida ya wanga. Sasa kuna siku kama kawaida akaenda ulevini. Sasa mida ameondoka baadae walikuja wanajeshi na mizigo yao. Walikuwa na kazi yao maalum pale ya kufanya kwa wiki moja. Kwahiyo ikabidi washike doria wenyewe hapo chuoni. Sasa kama kawaida dingi cha pombe akaamua kurudi, ila siku hiyo alirudi mapema, na alikuwa hajalewa, alionja tu! sijui kitu gani kilimgutusha! Akawa anarudi mdogo mdogo huku anasikiliza michezo(RTD enzi hizo, saa mbili kasoro). Ile anaikaribia kona ya kuingia maeneo ya kota akashtuka kusikia"hapo hapo simamaa!" We ni nani, unatoka wapi na unaenda wapi saizi?" Dingi kihoro! Pamoja na kujitambulisha ni mtumishi wa hapo chuoni, hawakumuacha! Walimrusha kichura chura, kisha wakamwambia aifiche redio yake kisha aiiibe!! Hapo kwenye kuiba redio yake ndipo alipoteseka. kila stail anayotumia, wanamkoromea, eti"mwizi gani anaiba kizembe hivyo?!" Walivyoridhika wakamwambia achukue mkulima wake atoke nduki. Mzee alifika yuko hoi na aliwatukana matusi ya kila aina. Kesho yake akaanza dozi ya metakelfin.
 
daah we acha tu hawa watu sio kuna sku niliomba lift katika gar lao basi si nikajifanya mjuaji nikadandia ki kondakta halaf nikagonga twendee kabla sjaingiz miguu yangu ndani aisee dereva akatoka akaniambia shuka nikabak nashangaa oohoo nikajua yameisha mara naskia haya shika gar isukume had itembee nilichoka hio sku kijasho kilinitoka
 
Daaahh nlikosea njia nikaongia anga za Wajeda
Nilipewa jagi la maji na Mche Mzima wa Sabuni nakuamriwa nioge hadi huo mche wa Sabuni uishe
Siku hio ndio nilijua tofauti ya Shuka na Pazia
 
Mimi niliwazidi akili MP wa lugalo nilipovuka tu ile bustani yao ya mauwa katikati ya barabara bila kujua nimevukia sehemu siyo sahihi.

Jamaa wakanishika wakanipeleka kwenye zile nyumba zao za mabati wakaanza kupanga magogo na mawe wanipe adhabu aise wakati huo nikaanza kutengeneza njia ya kuwatoka kwa akili kubwa

Kabla yakuanza mateso yake mkononi nilikuwa na bahasha ya tangazo la kuzaliwa mtoto wangu nilienda kuchukua lugalo hospital, MP mmoja nikamuita akaja nikamuambia unajua kaka Mimi naumwa tena kifua kikuu nimetoka kumeza dawa pale hospital kuna center ya wagonjwa wa kifua kikuuu, mpaka sasa sijisikii vizuri ndiyo maana nimevuka bila kuangalia pale kwenye bustani yenu.

Akaniuliza unataka nini sasa, nikamuambia unaweza kunipa mazoezi ya nguvu hapa nikafia hapa kesi itakuwa yako na hata jeshi halitakueleweni kufa mtu kisa kavuka barabara na kukanyaga bustani yenu, Mimi nachoomba msinifanyie hivyo kwasababu hapa nilipo serious naumwa na dawa inafanya kazi sijala mpaka sasa.

Wale MP kitu kiliwaingia akilini wakaniambia wewe nenda nyumbani mambo ya wagonjwa wa kifua kikuu kweli kituo kipo lugalo wanakijua, wakaniamini wakati huo nilikuwa nakooa kama kweli naumwa na natetemeka mwili mzima, nilipofika tu kituoni nikawahi kupanda Gari ya tegeta kabla hata haijasimama kituoni Mimi kama konda vile.

Hahahahahha, mimi pia pale ilinikuta, nilivuka bila kujua, kumbe pale wanapochomelea mashine za matofali na vitu vingine wanajeshi wanaotunza bustani wanakaa hapo

Nimepita vizuri kabisaaa, nafika hapo nashangaa naitwa na jamaa akaniambia kwann umekanyaga bustani wakati wao wanahangaika kumwagilia akanambia chukua ndoo kamwagilie yotee

Mm sikumwelewa akaanza kunifata nikakimbia kuelekea lugalo pale wanapokaa naona anapiga simubwanizingire mbele, niliingia chocho za mwenge pale mbioo za swalà, sikupita njia ile wiki 2
 
Hahahahahha, mimi pia pale ilinikuta, nilivuka bila kujua, kumbe pale wanapochomelea mashine za matofali na vitu vingine wanajeshi wanaotunza bustani wanakaa hapo

Nimepita vizuri kabisaaa, nafika hapo nashangaa naitwa na jamaa akaniambia kwann umekanyaga bustani wakati wao wanahangaika kumwagilia akanambia chukua ndoo kamwagilie yotee

Mm sikumwelewa akaanza kunifata nikakimbia kuelekea lugalo pale wanapokaa naona anapiga simubwanizingire mbele, niliingia chocho za mwenge pale mbioo za swalà, sikupita njia ile wiki 2
Hao jamaa wanakaa kituoni siku kituo cha kwenda tegeta na ule upande wa mwenge unadhani abiria kumbe askari wanalinda bustani
 
Hawa jamaa ni shida.
Kuna polisi mmoja yupo musoma waga ni kichomi balaa hasa kwa boda, yaani anajulikana kwa kutokiwa na mjadala na mtu aliyejipendekeza kwenye 18 zake.

Siku moja mida ya jioni jamaa aliyepiga kiraia akawa na pikipiki yake anaelekea maeneo ya bandarini alipofika maeneo ya nbc bank akakwangua kidogo gari, yule polisi kuona vile akaunga na jamaa, jamaa kavuta mpaka badarini na huko bandarini wajeda walikua wamewaka kituo, yule jamaa aliekuwa mbele anafukuzwa alipofika akafunguliwa geti akaingia, na huyu polisi nae akajichochea, jamaa zikafunga geti zikamuweka mtu kati, zilimfua kuanzia mida ile mpaka mida ya 4 usiku, kwa msaada wa rpc na mkuu wa wilaya, jamaa toka kule alilazwa almost wiki nzima.
Hizi njemba sio asee.

 
Afu hawa jamaa huwa hawatabiriki asee,
Kuna jamaa moja fundi alikuwa anawapigia bati kwenye moja ya majengo yao, mida ya kula ilipofika jamaa wakatenga jirani na alipokuwa anafanyia kazi maana kulikuwa na mti mkubwa wenye kivuli poa, wakamkaribisha jamaa, jama aakawatolea nje, wakaanza kupiga, wamepiga kidogo mara tena wakamuita, jamaa akatoa nje, wakaendelea kufinya, mida tena jamaa wakamuita,jamaa akaona isiwe taabu kishikaji na ukizingatia wamemuita mara nyingi akashukaili akafinye, kafika akanawa kisha akaanza kufinyampaka wakamaliza, baadaya kumaliza wakamwambia jamaa aoshe masufuria maana kawasumbu kumuita maranyingi afu kumbe alikuwa na njaa, asee, vililetwa vyombo, jamaa nakwambia aliosha kuanzia saa 8 mpaka saaa 2 usiku.
@Depal
 
Yes! Hapa alifundisha maadilli.
Aiseeee kipindi niko form four tulipanga tukafanye Project ziwani, mm nikiwa kama Chairman of Group.

Sasa tukiwa bado tunasubiri wahusika waje kutupa infos mimi nikaona isiwe noma ngoja nitembee tembee, Loh kule nilipokua naelekea kumbe kulikua na kambi ndogo ya Jeshi bahat nzuri niliwahi kuwaona nikarudi mbio hadi kwa jamaa yangu nikawa namuelezea.. Bahat mbaya tukawa tumesimama njiani akapita Kamanda wa ile jeshi kutufikia akasima, rafk angu alikia amevaa mkanda ambao matundu yake yapo mbalimbali akaonekana kama kavaa mlegezo. Tulikula makofi kidogo ya kuchangamsha damu then maswali yakaanza.
Kwanini umevaa mlegezo akajitetea weee mwisho akaambiwa OGELEA kiroho kikapiga Paaap maana nilijua anataka tuogelee penye Mv liemba imesima akasema namaanisha ogelea kwenye floor hapo naenda huku nikute umelowana.
Jama akajitetea mwishoni akaambiwa haya toboa mkanda vaa vizur AISEE JAMAA ALIUTOBOA MKANDA KWA MENO..!
 
Back
Top Bottom