Wale tuliokutana na adhabu toka kwa wanajeshi tuambie ilikuwaje

Pyepyepye

JF-Expert Member
Jan 6, 2017
1,940
3,825
Habari wana bodi.

Kama maada inavojieleza hapo, pengine kwa kuguswa moja kwa moja, kusimuliwa, au kuona kwa macho yako, namna ambavyo walinzi wetu hawa wanavyotoa adhabu dhidi ya wakosefu, walioingia kwenye anga zao, ama kwa maksudi au kwa bahati mbaya.

Mimi binafsi yalinikuta. Miaka kadha iliyopita nikiwa mwanafunzi wa wa sekondari ya Muyama, hawa jamaa (wanajeshi) walikua na kambi yao pale migongo (sijui kwa sasa kama ingalipo bado)

Siku hiyo ilikua jumamos na kwa kawaida jumamosi kwa maeneo yale ndio siku ya soko linalounganisha watu vijiji na maeneo ya mbali, yaani ndilo soko kubwa.

Ishu ilianza nikiwa na jamaa angu mmoja akiwa na demu wake, (mwanafunzi mwenzetu) wakati tukifanya manunuzi, ghafla alikuja dogo kistaarabu tu akamwambia demu wa jamaa kuwa anaitwa, na vile jamaa hakuwa na makuu akamruhusu demu aende, baada ya muda mfupi demu akarudi akiwa kama yuko off mood flan hivi, jamaa hakumuuliza.

Baada ya muda wa mizunguko na manunuzi ya hap na pale, hivi na vile, uzalendo ukanishinda nikaamua kumuuliza, shem wangu huyu, nae akafunguka, kuwa wanajeshi wanamsumbua, sa mie nikatoa wazo la kulipa kisasi na nikapendekeza tukatoe upepo kwenye tairi za gari lao.

Mchakato wa kisasi ujaanza, kwa kutafuta kijiti Cha kutolea upepo na misumari ya kutobolea tair. Baada ya zana kukamilika, tukaanza kulisogelea gari lao, wakati huo wao wanapiga urabu tu wala hawan wazo kabisa. Baada ya kulisogelea na kujiridhisha kuwa hakukuwa na mtu yeyote liyekuwa akijisumbua juu yetu, ndipo mshikaji wangu akachuchumaa kwa ajili ya kufanya yake.

Akiwa kachuchumaa kwenye tairi la pili, nilishangaa naona vumbi na mshikaji akiwa juu, ile na hamaki namuona mjeda mmoja akiwa anamtenda jeuri na nchi ile ina udongo mwekundu na vumbi lake asikuambie mtu. Wakati mjeda akiwa anmsurubu mshikaji, nikaona jamaa mwingine anakuja kwangu spidi, nikajiongeza kwa kujua ni wale wale, nililaza mshale mfano haujakuwepo.

Nimefika gheto (wakati huo tunaita camp) sina chochote, kila kitu nimetupa, hata demu (shem) mwenyewe sijui aliko, dk kama 20 baadae namuona jamaa angu kapauka na manundu ya kutosha, kababalnce (sare ya shule) kake kekundu kamechanwa, chanwa, ile namuona mshikaji tukaanza kucheka tu.

Siku chache baadae tunagundua washikaji wanamega tena kidemu kilicho tusababishia shida, tukaona hamna noma jamaa akamtema asee.

Wale ambao tunavisanga na hawa watu ebu tupeane uzoefu
 
Genye Sio Poa Aisee
Ilikuwa Kipindi Cha Mvua Mvua Kama Kawaida Nikamcheki Mtoto Wa Mjeda Kwa Simu Nikampanga Fresh Tutoke Nikamgegede Ramani Zikakubali tukapanga Fresh Tukapige Show Guest Moja Ambayo Iko Pembezoni Mwa Mji Dah !! Asalale Kumbe Pembeni Ya ile Guest Kulikuwa Na Bar Tunakatisha Hivi Kuingia Guest Naona Tunafatiliwa Nyuma Mara Papu Tunageuka Nyuma Na Muona Mzee Wake Huyu Hapa A wap Nani Adakwe Kizembe Nilikula Marathon Awards Ya Kufa Mtu Yani Alafu Kila Nikigeuka Nyuma Kipipa Hiki Hapa Duh!! Wajeda Sio Binadamu Wenzetu Kila Nikikumbuka Sina Hamu Nao
 
Kuna jamaa mmoja tunajuana kabisa alikua anatoka na mwanafunzi sasa uyo msichana ambae ni student kaka ake ni msoja na ndo anaemlipia mdogo wake schoolfees..... Mdogo wake alikanywa hajasikia sasa iyo siku jamaa alikua mtaani tuu na mambo yake gafla kaka mtu akamtokea yaan alimsulubuuu mtaa mzima walijaà hapo hakuna aliye amua...... Lkn baada ya mda mfupi student alijulikana mjàmzito na sasa iv anaishi na jamaa ake alie sulubiwaga na kaka ake
 
Siku niliingia kwenye shamba lao na kuangua embe za kutosha, mara paap jamaa huyu, aisee!! Sintosahau maana aliniambia nile embe zote na maganda yake then embe zenyewe mbichi hadi nafika home madenda tu yanatoka mdomoni na meno yote yamekufa ganzi!
 
Mimi niliwazidi akili MP wa lugalo nilipovuka tu ile bustani yao ya mauwa katikati ya barabara bila kujua nimevukia sehemu siyo sahihi.

Jamaa wakanishika wakanipeleka kwenye zile nyumba zao za mabati wakaanza kupanga magogo na mawe wanipe adhabu aise wakati huo nikaanza kutengeneza njia ya kuwatoka kwa akili kubwa

Kabla yakuanza mateso yake mkononi nilikuwa na bahasha ya tangazo la kuzaliwa mtoto wangu nilienda kuchukua lugalo hospital, MP mmoja nikamuita akaja nikamuambia unajua kaka Mimi naumwa tena kifua kikuu nimetoka kumeza dawa pale hospital kuna center ya wagonjwa wa kifua kikuuu, mpaka sasa sijisikii vizuri ndiyo maana nimevuka bila kuangalia pale kwenye bustani yenu.

Akaniuliza unataka nini sasa, nikamuambia unaweza kunipa mazoezi ya nguvu hapa nikafia hapa kesi itakuwa yako na hata jeshi halitakueleweni kufa mtu kisa kavuka barabara na kukanyaga bustani yenu, Mimi nachoomba msinifanyie hivyo kwasababu hapa nilipo serious naumwa na dawa inafanya kazi sijala mpaka sasa.

Wale MP kitu kiliwaingia akilini wakaniambia wewe nenda nyumbani mambo ya wagonjwa wa kifua kikuu kweli kituo kipo lugalo wanakijua, wakaniamini wakati huo nilikuwa nakooa kama kweli naumwa na natetemeka mwili mzima, nilipofika tu kituoni nikawahi kupanda Gari ya tegeta kabla hata haijasimama kituoni Mimi kama konda vile.
 
Sitasahau siku nilipomng'ang'ania raia abebe bodaboda yake.
Ilikuwa mwaka 2013, jkt mujibu wa sheria kambi ya 822KJ Rwamkoma. Tupo single file tumetoka pori siku tatu atujalala usingizi.
Tukiwa njiani tunarudi kambini tukakutana na mkurya mmoja anaendesha pikipiki yake, sasa sijui alikuwa hajasikia ile amri ya bodaboda zote zisimame ili siye tupite (akaharibu kazi!).
Basi tupo na afande wetu private machachari (afande wa demo) afande Ramadhani Dio si ndo tukamuona jamaa anatusogelea...! Kurutu tukaongea na afande wetu na afande akakubali..! Aisee tulipewa dakika tano (tano za nguvu) yule mura nadhani alienda kuhadithia nyumbani kwake..!
Off course sijisifii wala kujiskia vzuri kwa tulichokifanya, ila daah jeshini sio jamani..! Unaweza ukafanya kitu unajua kibaya sema ile roho mbaya (sumu uliyotemewa na makamanda ) ikasababisha ukafanya mambo ya ajabu sana...!
 
Kuna jamaa mmoja tunajuana kabisa alikua anatoka na mwanafunzi sasa uyo msichana ambae ni student kaka ake ni msoja na ndo anaemlipia mdogo wake schoolfees..... Mdogo wake alikanywa hajasikia sasa iyo siku jamaa alikua mtaani tuu na mambo yake gafla kaka mtu akamtokea yaan alimsulubuuu mtaa mzima walijaà hapo hakuna aliye amua...... Lkn baada ya mda mfupi student alijulikana mjàmzito na sasa iv anaishi na jamaa ake alie sulubiwaga
Duh sitasahau makutupora 2005

Ilikuaje mkuu??
 
Kuna jamaa mmoja tunajuana kabisa alikua anatoka na mwanafunzi sasa uyo msichana ambae ni student kaka ake ni msoja na ndo anaemlipia mdogo wake schoolfees..... Mdogo wake alikanywa hajasikia sasa iyo siku jamaa alikua mtaani tuu na mambo yake gafla kaka mtu akamtokea yaan alimsulubuuu mtaa mzima walijaà hapo hakuna aliye amua...... Lkn baada ya mda mfupi student alijulikana mjàmzito na sasa iv anaishi na jamaa ake alie sulubiwaga na kaka ake
Huyo jamaa alithibitisha penzi la kweli asee.
Ila wanaume nao ni vichwa ngumu, kweli.
 
Back
Top Bottom