Wale polisi waliocharazwa Bakora na raia wamefukuzwa kazi ! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wale polisi waliocharazwa Bakora na raia wamefukuzwa kazi !

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutunga M, Aug 7, 2009.

 1. Rutunga M

  Rutunga M JF-Expert Member

  #1
  Aug 7, 2009
  Joined: Mar 16, 2009
  Messages: 1,556
  Likes Received: 230
  Trophy Points: 160
  Kwa wiki kadhaa zilizopita ilitolewa post hapa JF kuhususiana na polisi waliopigwa na wananchi kwa kuchoshwa na vitendo vya rushwa katika mkoa wa Kagera.

  sasa jeshi la polisi limewatumia kazi polisi 2 kati ya wanne waliohusika katika tukuio hilo.

  taarifa ya kutumiliwa kwao imetolewa na jeshi la polisi leo asubuhi na imewataja kuwa ni mwenye namba E 7107 sajini Herman Musiha(40) maarufu kwa jina la “peke peke” na mwenye namba F 7372 PC Mateso Said (26) ambao Julai,11 walitoroka kituo chao cha kazi cha Bukoba Mjini na kwenda wilayani Missenyi na kufanya kazi ya kusimamisha magari yanayovusha magendo kwa lengo la kuwashurutisha wwavushaji ili wawapatie fedha.Hata hivyo waliambulia kipigo ,kunusurika kuchomwa moto na gari walilokuwa wamekodi kuvunjwa vunjwa.

  kwa mjibu wa taarifa hiyo ni kuwa polisi hao wanakabiliwa na kesi mahakamani.

  Haijaelezwa wengine watachukuliwa hatua zipi
   
 2. Kilbark

  Kilbark JF-Expert Member

  #2
  Aug 7, 2009
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 558
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Hawa jamaa (Polisi) wamezidi halafu hii nchi yetu mambo ya zimamoto yanatuathiri sana hata mwenendo wa baadhi ya memba hapa JF mimi mmoja wao yaani tunajadili kitu baada ya tatizo na sio kabla ya tatizo. Najua mfumo wetu sio mzuri na hata hili jeshi la Polisi. Nakumbuka katika Bunge la kwanza baada ya uchaguzi mkuu wa 2005 hoja kuhusu jeshi la polisi ilizungumzwa na nadhani mheshimiwa Slaa alisema jeshi la Polisi lifanyiwe overhaul sasa sijui iliishia wapi. Leo majambazi wakianza utasikia oooh Polisi wana shida wana matatizo hawana vitendea kazi posho na porojo zisizokuwa na msingi tatizo tunalijua kwanini tusilimalize? Tunangojea mpaka linapokuwa kubwa tunaanza kutupiana lawama. Na huu utamaduni ndio tulionao.
   
Loading...