maroon7
JF-Expert Member
- Nov 3, 2010
- 11,144
- 15,143
Aisee kweli hapa mjini kila kitu ni dili la mtu. Mtakumbuka wale walemavu ombaomba waliokua wanasukumwa kwenye wheelchair walisambaa kila kona ya Dar kuanzia asubuhi hadi usiku,wanaingia kwenye bar,migahawa,madukani na kwinginek.
Mpaka tukawa tunajiuliza mbona wanaowasukuma ni mabaunsa kwanini wasipige vibarua wasaidie hao walemavu kumbe baadae ikaja gundulika kuna mtu mmoja ambae alikuwa anawatoa mikoani kawalundika kwenye nyumba yake kila siku wanaleta hesabu.
Baada ya dili kuvumbuluka yule mzee alikamatwa na cha kushangaza toka kipindi hicho hadi leo sijaona hata mmoja anaetembezwa kwenye wheelchair kwa style ile. Hii inaashiria kuwa hata mkuu wa mkoa wetu Makala akiamua kuwarudisha na kuwaaondoa mitaani kwa kiasi kikubwa itafanikiwa ila pia wafanye uchunguzi kuwabaini wenye mtandao huo wa ombaomba asichukulie tu poa eti ni ombaomba mmojammoja.
Sasa imagine kama mtu mmoja aliweza kuwamwaga ombaomba jiji zima na akawapa wheelchair na kuwahost unadhani haiwezekani kuwadhibiti hawa wengine kwa style hiyo?
Uchunguzi ukifanyika amini nawaambia asilimia 90 hatutawaona mtaani.