Wale mnaopenda Kukurupuka ‘ Kianaharakati ‘ Mitandaoni na Kutetea ‘ msivyovijua ‘ mbona baada ya ukweli mmepotea ghafla?

Hivi una taarifa kwamba Spika mara kwa mara alikuwa akimwambia kuwa hayo anayoyataka hayawezekani kwakuwa hayako ndani ya uwezo wake ila Mbunge Masele akawa bado analazimisha? Ina maana hukumsikia jana Spika Ndugai alivyokuwa ' akitiririka ' na ' kuserereka ' kumhusu Mbunge Masele? Sasa kwa hili kati ya Mimi na Wewe nani ndiyo ' amechemka ' zaidi hasa Kitaarifa?

Jamaaa alovyokosa akaenda kwa waziri mkuu kuomba kituko sana jamaa
 
Nakumbuka Wiki iliyopita baada ya hili ‘ Sakata ‘ Kuibuka na Kuanza kusambaa sehemu mbalimbali na hasa hasa humu ‘ Mitandaoni ‘ kuhusu Mbunge Masele ya Spika wa Bunge Ndugai nilichangia katika Uzi wa Mtu hapa na ‘ nikatahadharisha ‘ kuwa Watanzania tuache ‘ Kukurupuka ‘ na kusukumwa na Hisia za ‘ Kianaharakati ‘ kwani Siku ukweli ukija Kutolewa Kwetu wengi Wetu tuliokuwa ‘ tukilaumu ‘ tu tutatafuta wapi tufiche Sura zetu kwa Aibu.

Baada ya Mbunge Masele ‘ Kuwaaminisha ‘ Watanzania wana Mitandao wa ‘ Kukurupuka ‘ kuwa Yeye hakuwa na Kosa huko katika Bunge la PAP ambapo Yeye ni Makamu wake / wao hatimaye jana ukweli kamili umejidhihiri na kuwekwa hadharani juu ya ‘ Mapungufu / Makandokando ‘ yake na kama kawaida wale waliokuwa ‘ wakimtetea ‘ Kutwa wamepotea ghafla wakati mwanzoni ndiyo walikuwa wakifululiza Kumtetea na Kudhania kuwa ameonewa au anaonewa.

Hivi Mbunge Masele Yeye ni nani mpaka alazimishe na hadi Kushinikiza kwa Watu wa Ikulu, Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi ‘ Nyeti ‘ nchini kuwa ni lazima apatiwe Walinzi kutoka Usalama wa Taifa wa Kumlinda? Yeye ni nani hadi atake Kupewa Nyumba Kubwa ( Mansion ) na Gari za Kifahari na hadi awe na ‘ Msafara ‘ wake? Huu ‘ Ukubwa ‘ aliokuwa akiutaka Mbunge Masele unatokana na nini labda?

Bado nahoji wale wana ‘ Mtandao ‘ mliokuwa mkimtetea mpo wapi sasa? Mbona mmenyamaza?

Nawasilisha.
Inaelekea zengwe lilipikwa na kubumburuka liko juu ya uwezo wako wa kufikiri.
In short, Ndugai kasalimu amri!
 
Leo umekamatika mkuu kumbe umesoma chuo cha vilaza SAUTI. Sidhani pale kama kuna mtu alipata dvision One( labda ya dini) anapenda kwenda SAUTI pale ni vilaza na waliopata bahati mbaya wakadondokea division 3 na 4.. Hata Heslb mkopo hawatoi. Hahahaaa.

Kwahiyo Sisi tuliopata Division I Kidato cha Sita ilikuwaje tukakubalika na Kusoma hapo SAUT? Narudia tena Kusema hapa tena kwa Jeuri na Kiburi chote kuwa kama unajijua huna ' Akili ' na ' hukubarikiwa ' nazo kamwe usipoteze muda wako kwenda Kusoma Chuo Kikuu cha ' Geniuses ' watupu cha SAUT Mwanza ila kama una uhakika pasi na shaka kuwa Wewe ni ' Popoma Mwandamizi ' kabisa basi sehemu yako ya haraka ya kwenda ni Mlimani ( UDSM ) na hili halina Ubishi kwani huko ndiko kumejaa ' Wanataaluma ' wa ' hovyo hovyo ' watupu.
 
Jamaaa alovyokosa akaenda kwa waziri mkuu kuomba kituko sana jamaa

Na huko Kote unaambiwa alikuwa ' anamfitinisha ' tu Spika wa Watu Masikini ya Mungu. Na unaambiwa Mbunge Masele alifika hatua hadi ya kutaka sasa ' Kuwagombanisha ' Waziri Mkuu Majaliwa na Spika Ndugai kwa ' Maslahi ' yake ila sema tu Watu wenye ' Akili ' walimshamsoma mapema na ' Kumtonya ' Spika, Waziri Mkuu na hadi Mheshimiwa Rais juu ya huo ' Upuuzi ' wake Mbunge Masele.
 
Sasa kushinikiza kupewa ulinzi pamoja na jumba na gari la kifahari vinahusiana nini na kuchonganisha mihimili?!
 
Hivi una taarifa kwamba Spika mara kwa mara alikuwa akimwambia kuwa hayo anayoyataka hayawezekani kwakuwa hayako ndani ya uwezo wake ila Mbunge Masele akawa bado analazimisha? Ina maana hukumsikia jana Spika Ndugai alivyokuwa ' akitiririka ' na ' kuserereka ' kumhusu Mbunge Masele? Sasa kwa hili kati ya Mimi na Wewe nani ndiyo ' amechemka ' zaidi hasa Kitaarifa?
Mmmh, hayo sijui.
 
Sasa kushinikiza kupewa ulinzi pamoja na jumba na gari la kifahari vinahusiana nini na kuchonganisha mihimili?!

Alikuwa ' akivilazimisha ' wakati tayari Spika alishamwambia mara kwa mara kuwa ' haliwezekani ' ila Jamaa ( Mbunge Masele ) akawa bado amelishikilia Bango na analishinikiza huku akienda mbele zaidi kwa Waziri Mkuu na Watu wa Ikulu waliokuwa karibu na Rais ili wamfikishie matakwa yake na tena akiwaambia kuwa Spika Ndugai hamsikilizi na hata akimpiga ' Majungu ' vile vile kote alikokuwa akipita na ' Dai ' lake Kuu / Mama ni Yeye kutaka Kupewa ' Hadhi ' ya Makamu Mkuu wa Bunge la PAP kwa kupewa Ulinzi kutoka TISS ( Usalama wa Taifa ), Gari la Kifahari na awe na Msafara wake na apewe Nyumba ( Mansion / Posh House )
 
Basi kama ni hivyo acha waendelee kutoana macho.
 
Sasa kama kumbe ulikuwa huyajui au huyajui kwanini unabisha au ulitaka ufafanuzi wake wa nini? ' Moron ' mkubwa Wewe.
Hahaha, tatizo lako GENTAMYCINE, pamoja na wakati mwingine kuja na hoja zilizoshiba, hii tabia ya kujifanya conclusive siyo kabisa. Ndio maana hili ni jukwaa, sasa watu wasipochangia kama unavyotaka huna haja ya kutoa matusi. Mimi kwa maoni yangu si kosa kwa Masele kuomba alivyoviomba. Sasa usinilazimishe niamini unayoyaamini wewe.
 
Kwani Wewe ulidhani labda kulikuwa na shida gani nyingine?
Mimi nilifikiri ni kitendo cha yeye kuomba kupewa huo ulinzi tu. Lakini kama ni kweli alikuwa anawagonganisha kwa maneno ya kuhamisha huku na huku, basi na waendelee tu. Mimi wacha niendelee kufurahia mechi.
 
Duh...nchi hii ukistaajabu ya Musa hata ya Firauni nafikiri hayatishi......!
 
Na ninavyojua huwezi Kusoma au hata Kukubaliwa tu kusoma SAUT Mwanza kama Wewe siyo ' Genius ' na ' Intellectual ' wa Kutukuka. IQ yangu ya Kuzaliwa pamoja na ile niliyoongezewa na Wahadhiri wangu ' Geniuses ' watupu wa SAUT akina Padre Charles Kitima, Baba Askofu na Mhadhiri wangu Kipenzi kabisa Dkt. Bernadin Mfumbusa, Dkt. Aidan Msafiri, Dkt. Dietrick Kaijanangoma ambaye sasa ndiyo Mkuu wa SJMC ( UDSM ), Dkt. Mataba ( kama ameshamaliza PhD yake ), Dkt. Robert Mkosamali, Dkt. Barrack Otieno, Dkt. Ilkuyoni, Dkt. Xavier Ng'atigwa na wengineo wengi imenifanya GENTAMYCINE niwe na hiki Kiburi, Jeuri na Mtamu kabisa ' Upstairs ' Kwangu.
80% inahusika.
 
Nakumbuka Wiki iliyopita baada ya hili ‘ Sakata ‘ Kuibuka na Kuanza kusambaa sehemu mbalimbali na hasa hasa humu ‘ Mitandaoni ‘ kuhusu Mbunge Masele ya Spika wa Bunge Ndugai nilichangia katika Uzi wa Mtu hapa na ‘ nikatahadharisha ‘ kuwa Watanzania tuache ‘ Kukurupuka ‘ na kusukumwa na Hisia za ‘ Kianaharakati ‘ kwani Siku ukweli ukija Kutolewa Kwetu wengi Wetu tuliokuwa ‘ tukilaumu ‘ tu tutatafuta wapi tufiche Sura zetu kwa Aibu.

Baada ya Mbunge Masele ‘ Kuwaaminisha ‘ Watanzania wana Mitandao wa ‘ Kukurupuka ‘ kuwa Yeye hakuwa na Kosa huko katika Bunge la PAP ambapo Yeye ni Makamu wake / wao hatimaye jana ukweli kamili umejidhihiri na kuwekwa hadharani juu ya ‘ Mapungufu / Makandokando ‘ yake na kama kawaida wale waliokuwa ‘ wakimtetea ‘ Kutwa wamepotea ghafla wakati mwanzoni ndiyo walikuwa wakifululiza Kumtetea na Kudhania kuwa ameonewa au anaonewa.

Hivi Mbunge Masele Yeye ni nani mpaka alazimishe na hadi Kushinikiza kwa Watu wa Ikulu, Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi ‘ Nyeti ‘ nchini kuwa ni lazima apatiwe Walinzi kutoka Usalama wa Taifa wa Kumlinda? Yeye ni nani hadi atake Kupewa Nyumba Kubwa ( Mansion ) na Gari za Kifahari na hadi awe na ‘ Msafara ‘ wake? Huu ‘ Ukubwa ‘ aliokuwa akiutaka Mbunge Masele unatokana na nini labda?

Bado nahoji wale wana ‘ Mtandao ‘ mliokuwa mkimtetea mpo wapi sasa? Mbona mmenyamaza?

Nawasilisha.
Kamuulize mama ako nae ikuwa anamtetea
 
Mimi nilifikiri ni kitendo cha yeye kuomba kupewa huo ulinzi tu. Lakini kama ni kweli alikuwa anawagonganisha kwa maneno ya kuhamisha huku na huku, basi na waendelee tu. Mimi wacha niendelee kufurahia mechi.

Samahani hiyo Mechi unayosema unaendelea nayo hivi sasa ni hii hii ya ' Kibaiolojia ' au labda ni ile ya ' Runingani ' tu Mkuu?
 
Tatizo la watanzania wengi tunapenda ku- take side bila kufanya analysis ya kutosha!!

Halafu pia tukisoma ufafanuzi kwenye michango ya wengine badala ya kujitahidi kuelewa tunatetea side/maoni yetu ki unazi!!

Tushazoea ubishi na utimu wa Simba na Yanga!!

Gentamycine kwa mara ya kwanza leo naona kakamatika kwenye unazi hadi anatumia hoja ya u- genius na uzuri wa Chuo alichoma hadi kuponda chuo kikongwe cha Taifa!!!

Hivi ina maana Masele alitakiwa kuomba stahili zake wapi kama makamu wa rais wa Bunge la Afrika PAP!

Yeye kama Makamu wa Rais kuna stahili zinazoendana na cheo chake na anatakuwa apewe stahili hizo nchini kwake!!
Sasa angeimba wapi kama sio kwa Spika na Viongozi wakuu wa serikali!!

Hivi tulishawahi kama watanzania kumtambua na kumpongeza Masehe kwa hatua aliyofikia ya kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais PAP!! Au roho zilimetuuma na kumwonea wivu .

Hivi akuwa Raisi wa PAP bado tutambania stahili zake? Mbona roho za korisho hivi watz!!

Tungekuwa tunaongozwa na Upendo migogoro mingi usingetokea!!

Tukiwapigia kura CHUKI na UPENDO nahofia CHUKI anaweza kushinda!!

Watanzania tupendane!!
 
Kwasababu wewe ni mbumbumbu(hujui kitu) na huelewi ngoja nikuulize nikusaidie,

1.Wale makamu wengine wawili wanapewa vyote alivyodai Masele na nchi zao.

2.Bashite tu hapo ana walinzi wa kutoka nyumba nyeupe, yeye nani katika nchi hii? Anapewa kwa utaratibu upi?

3.Kama hujui Male ndiye anatumika kuendesha vikao vingi vya PAP kutokana na kuaminiwa kwake, huyu Rais wa PAP anagomewa na wabunge wote kwa tabia zake za hovyo.

Kwa fitina anazomfanyia Masele, ana haki ya kupewa ulinzi.
Bashite ni muajiriwa wa serikali ya tanzania. Masele ni muajiriwa wa bunge la Africa tena ni makamu wa rais. Nadhani mishahara na marupurupu yake wanaohusika ni PAP. Sasa serikali inahusikaje? Aongee na pap apeleke mapendekezo.
 
Back
Top Bottom