Trouton
JF-Expert Member
- Jul 3, 2018
- 1,194
- 1,362
nikua mwenyewe natoka Dar kwenda mbeya kipindi hicho.hahaha ni kweli mkuu. Ushawahi kusafiri upo na kampani ya washkaji? Nayi huwa ni nzuri sana.
nikua mwenyewe natoka Dar kwenda mbeya kipindi hicho.hahaha ni kweli mkuu. Ushawahi kusafiri upo na kampani ya washkaji? Nayi huwa ni nzuri sana.
Kabisa mkuu,mimi nina uchu lakini nikifika kisaki uwa nafunga mdomo.Ila stimela ni usafiri poa sana.Wazambia wanapenda sana pombe! Kuhusu suala la kuku wa Kisaki ni sawa na wale kuku wa Salanda kwa reli ya kati. Unakutana na kuku mkubwa kama mwewe afu bei chee hadi mwenyewe unaweza tamaa inakuisha.
Nakumba madaraja makubwa , treni ikiwa inapita kwenye mahandaki ,na good view hasa ukiwa buffet unafanya mambo yakoBila kupoteza muda, mliowahi kupanda Treni ya Tazara, Dar, Mbeya, Kapirimposhi. Ni kitu gani unakikumbuka katika safari zako ndani ya treni hiyo? Vipi yale mahandaki na kona za hatari?
Karibuni kwa mjadala...
Kwa hiyo katika hiyo vita ya ujenzi wa reli ya Tazara walikufa wajenzi wengi zaidi ya wale askari waliokufa kwenye vita halisi ya Kagera kati ya Tanzania na Uganda?Kuna siku niliona kwenye documentary moja tbc kuhusu ujenzi wa Reli hii, ambapo wachina takribani 300 walipoteza maisha, wabongo na wazambia 400. Hiyo ni kutokana na ujenzi huo kupita sehemu zenye wanyama wakali hivyo ikahatarisha maisha ya wajenzi.
Ni reli ambayo imegharimu maisha ya watu wengi sana.
Umenikumbusha mbali sana nakumbuka tulikuwa tunatoka Mbeya kwenda dar kuna jamaa yangu alikunywa pombe aina ya amarula akaanza fujo na tulipofika makambako walimshusha askari wakampeleka kituoniBila kupoteza muda, mliowahi kupanda Treni ya Tazara, Dar, Mbeya, Kapirimposhi. Ni kitu gani unakikumbuka katika safari zako ndani ya treni hiyo? Vipi yale mahandaki na kona za hatari?
Karibuni kwa mjadala...
Huyo mdada Sasahivi anaendesha Treni la TAZARA to MWAKANGAOooh aise ilikuwa hatariii, yule dada Ni shida sanaaaa mwaka huo huo km sijakosea alipewa kipande Cha mlimba to mang'ula aise alikuwa anakimbiza hatariiiii...kufika mngeta 1km Kabla kufika stesheni ngoma ikahama Reli ikapasua katikati ikakata taluma nyingi Sana, vumbi likilotokea ilikuwa si mchezo behewa 2 za mwisho zikalala chini bahat nzuri Hakuna aliyekufa, dada yule noma sana
Umenikumbusha mbali kuna safari moja nilipanda treni, vituo kama 2 kabla ya kufika Mlimba kichwa cha tren kikataka kuwaka moto hivyo ikabidi wakitenganishe na mabehewa hivyo watu wote walishuka chini kwa mshtuko. Kusolve ikabidi waende kufuata kichwa kingine Mlimba basi tulikaa muda mrefu sana mpaka watu wakawa wameishiwa pesa, Sasa kuna watu walibeba zawadi za machungwa wakaanza kuuza Mia Mia mpaka muda yakafikia sh 700 nilishangaa sana maana kabla ya hiyo shida ata bure mtu anakupa.Bila kupoteza muda, mliowahi kupanda Treni ya Tazara, Dar, Mbeya, Kapirimposhi. Ni kitu gani unakikumbuka katika safari zako ndani ya treni hiyo? Vipi yale mahandaki na kona za hatari?
Karibuni kwa mjadala...