Wale Mliowahi Kupanda Treni ya Tazara Tukutane Hapa

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
5,310
2,000
Wakati nilipokua natumia usafiri wa Tazara, hakuna jambo ambalo nilikua nalikwepa kama lile la kukata tiketi ya 3rd class. Nikienda stesheni halafu wakiniambia supersitter na second kumejaa, nilikua nipo radhi kubadili usafiri na kuondoka na basi.

Kuna mwaka nilishuka Iyunga nikiwa sina kitu baada ya mpuuzi mmoja kunivizia nilipopitiwa na usingizi halafu akabeba begi yangu ya nguo. Pia msimu wa mavuno (mpunga) kuanzia mwezi wa 6 na pia kipindi cha kufunga na kufungua shule, dah! hilo dude huwa linajaza abiria mpaka mlangoni, chooni, njiani, kiasi kwamba hata pa kupita tu ni tabu.

Kiujumla ule usafiri una changamoto nyingi ingawa unawasaidia sana wakazi wa jirani na hiyo reli. Serikali ingekua siriazi, wangeweza kupata mapato mengi sana kupitia tazara! Bahati mbaya wanashindwa na sababu wanazijua wenyewe.
 

Somi

JF-Expert Member
Feb 7, 2009
1,389
2,000
1552428347785.jpeg
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom