Wale Mlio na uzoefu katika lugha ya kiswahili tujadili maneno haya

mathsjery

JF-Expert Member
Sep 26, 2015
2,208
1,755
Nini maana ya neno kuoana?!
Nini Tofauti Kati ya kuchumbia/kuchumbiwa na kuposa/kuposwa?!
Mfano:-
Unasikia mwanamke/mwanaume(mwanamme) anasema Mimi na mke/mme(mume) wangu tumeoana.
Wanamaanisha Nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuoana ni neno lenye maana ya kupatana, wakati kuoa ni kupata na kuolewa ni kupatwa. Watu mume na mke hatusemi Fulani kapata na Fulani kapatwa kwamaana ya kuoa na kuolewa bali tunasema wamepatana kwamaana ya kuoana. TUKI 2014 wanafasili neno "oa" kuwa ni kufanya muungano na mwanamke ili kukaa pamoja naye kama mke na mime kulingana na sheria, mila, desturi au taratibu za ndoa za mahali panapohusika.

Barafu la moto
 
Lakini kuna wengine Wanasema kuoana ni kufanana, Je unalizungumziaje hili? Na Kama ni sawa, unafikiri ni sawa kwa wanandoa kulitimia neno hili na labda kuna mbadala?!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lakini kuna wengine Wanasema kuoana ni kufanana, Je unalizungumziaje hili? Na Kama ni sawa, unafikiri ni sawa kwa wanandoa kulitimia neno hili na labda kuna mbadala?!

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndio, kuoana inaweza kuwa kufanana. Muktadha ndio unaoukiria kilongo cha kutumika, kwalugha nyepesi ni sawa na kusema neno oa/ oana huwa na maana kwakutegemea na mazingira ya utumizi wake. Mfano katika mitihani ya kiswahili tunatumia neno oanisha ikiwa na maana fananisha/ linganisha/ patanisha/ n.k. lakini kwa muktadha wa ndoa sio sahihi kulifasili neno oa kwakusema ni kufanana, kwenye ndoa linaweza kufasiliwa kama kukubaliana kuishi pamoja(kupatana), kuungana, n.k. Ingawa katika jamii za kiafrika hatutumii msamiati wa kuoana bali wa kuo na kuolewa tu, hili ni kutokana na utamaduni wa mwanaume kumlipia mwanamke na kumhudumia.

Barafu la moto
 
Kwa mujibu wa uislamu na tamaduni za kiafrika tuna kuoa na kuolewa kwasababu mmoja anamchukua mwingine kwa kumlipia na kwenda kuishi pamoja. Lakini ukristo unaangalia muunganiko au mapatano yao kiroho zaidi na kuona kwamba wanakuwa ni mwili mmoja na ndio ulipo mzizi wa kuoana, kwasababu hawazingatii nani kamfuata nani na nani kalipa nini tofauti na uislamu ambao wakati wa kuoa mpaka malipo hutamkwa.
Sijui kwa taratibu nyingine lakini nijuavyo kwenye Uislamu mume anaoa na mke anaolewa sio kuoana

Barafu la moto
 
Back
Top Bottom