Wale Mashabiki wa Simba SC tunaokerwa na Uchezaji wa Clatous Chota Chama tujitokeze Kumkosoa hapa tafadhali

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,011
16,748
Sina shida na Kipaji chake Kikubwa alichonacho ila Kiufundi kwa Kocha Mweledi na ambaye haingiliwi na Uongozi wa Timu hawezi Kumuanzisha Clatous Chama katika Mechi za Ushindani hasa.

Hii ni Mechi yangu ya Saba namtizama (namfuatilia) Clatous Chama na Kugundua kuwa ndiyo Mchezaji Kinara wa Kuharibu ( Kufifisha ) Mashambulizi ya Simba SC kwenda kwa Timu pinzani.

Leo tena amerudia Kosa lile lile kama alilolifanya dhidi ya Azam FC ambapo kuna nyakati Mchezaji mwenzake Kapombe au Dilunga alikuwa katika nafasi nzuri ya Kufunga ila kama Kawaida yake akaupooza mpira na Shambulizi Kufifia.

Yapo matukio yake mengi tu ila Kwangu Mimi itoshe tu kusema Clatous Chota Chama anatakiwa awe anaingia pale tu Timu ikiwa imeshashinda tayari ila siyo ikiwa inausaka (inatafuta) Ushindi kwani anatuchelewesha na atatuchelewesha mno katika Ushindi.

Na sishangai Kumsikia Mmoja wa Waandishi wa Habari za Michezo nchini Zambia na Mchambuzi Siku moja alipohojiwa na Mtangazaji wa Clouds FM alishangaa kusikia kuwa Chama huku Tanzania ni Mchezaji Mzuri na Mkubwa wakati kule Kwao nchini Zambia ni Kawaida mno ila akasema Mchezaji mwenye Kipaji cha hali ya Juu Zambia na hata Wachezaji wenzake wanamkubali ni Larry Bwalya.

Mlio karibu pia na Chama mrekebisheni.
 
Kweli mkuu ila hayo tuyaache kwa kocha na benchi la ufundi
Asipobadilika tutampeleka kwa Mkopo Yanga SC akateseke kwa Kunyanyaswa na akina Kaseke na akishikishwa Adabu na Kutia Huruma tutamrudisha kwa Wanaojua zaidi ya Al Ahly Afrika nzima Simba Sports Club a.k.a Kiboko ya Kocha bora na tajiri Afrika Pitso Mosimane.
 
Unaweza kukuta mleta uzi hajawahi kucheza ata one touch
Ningeamua kuendelea Kucheza mpira huenda Watanzania mngekuwa kila Siku mnaniimba, mnanitizama Runingani katika Ligi Kubwa Ulaya huku wengine kila mkiniona tu mngetaka kupiga Selfie na Mimi. Zinedine Zidane 65% ya Ujuzi na Uwezo wake Kajifunzia Kwangu. Hutaki jinyonge / Hamtaki jinyongeni kabisa.
 
Kwahiyo tujadili hoja yako kwa sisi tunavyomtazama chama au wanavyomzungumzia wazambia huko kwao?
Kati ya Watanzania na Wazambia wanaojua hasa Soka na hata Viwango tu vya FIFA wako mbali kati ya Tanzania na Zambia ni nani?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom