Wale ambao tumekatishwa tamaa na madaktari kwamba hatuwezi kuzaa tena tukutane hapa kwa nia ya kupeana moyo

Tofauti ipo bwana,mtoto wa testtube na mtoto anaepatikana kwa natural ya Mungu alivyoumba.
Usimdharau ukajiona Wewe Ni Bora ..huyo Mungu aliona wengine watapata watoto kwa njia hiyo...Mungu ndo kawapa Karama hii binadamu ya kuweza kutatua matatizo ya Watu..

Usijione uko Bora zaidi kwa kuzaa natural eti wengine hawakufaaa...lahasha.
.Wewe umebeba miez Tisa na yeye amebeba miezi Tisa..WOTE NI WATOTO...Tena wahuyu anaweza kuwa mtoto Bora kuliko huyo wako wa natural.
 
Waongo tu hao, kaka yangu aliambiwa hawezi kutungisha mimba akakata tamaa, hivi navoandika hapa mkewe ana toto la kiume miaka 3 kopi kopi kopi kila Idara na baba yake na mkewe tyr ana mimba nyingine tumbo lishaanza kujionesha
Usijipe moyo sn shemeji yako ndiye anayejua kinachoendelea.
 
Usimdharau ukajiona Wewe Ni Bora ..huyo Mungu aliona wengine watapata watoto kwa njia hiyo...Mungu ndo kawapa Karama hii binadamu ya kuweza kutatua matatizo ya Watu..

Usijione uko Bora zaidi kwa kuzaa natural eti wengine hawakufaaa...lahasha.
.Wewe umebeba miez Tisa na yeye amebeba miezi Tisa..WOTE NI WATOTO...Tena wahuyu anaweza kuwa mtoto Bora kuliko huyo wako wa natural.
Hujanielewa. Tatizo lipo kisaikolojia zaidi. Mtoto akikua utamwambia yeye alipatikana nje ya fallopian tube ?
 
Walimwambia ukweli,unajua mimba ya kupandikizwa ni hivi, wanakupa madawa unaovulate mayai mengi then wanachukua mayai wanayakutanisha na sperms maabara. Halafu yatakayo fanikiwa kutoa embryo. Wanaichukua hiyo embryo ndo wanainject kwenye uterus.
Kwahiyo hapa anakuwa mtoto sio wa mume ni wa maabara
 
Ni kweli inauma sana lakini mwisho wa siku unatakiwa ujikubali na kuishi maisha ya furaha kama wanavyoishi watu wengine. Kuna watu wanzaa alafu watoto wote wanakufa na kuwaacha wao wakiteseka,na wengine wanazaa mabalàa tu. Muhimu ni kushukuru kwa kila like ulilopangiwa na Muumba wako.

Nilioa 2009 mpaka August 2013 tulikuwa hatujapata mtoto mke akahisi yeye ndiyo ana matatizo maana Mimi kitandani Niko zaidi ya fit yenyewe. Mke wangu akata akipime mwenyewe tu nikamuambia hapana tukapime sote hatuwezi kujua nani ana matatizo.

August 2013 tukotoka zetu mkoani mpaka Dar TMJ pale nikaweka appointment na Gynecologist wa kike, tukafanyiwa vipimo sote wawili,kutoka majibu mke wangu yupo normal na Mimi nikakutwa Obstructive Azospermia. Kwa miaka mitatu mke wangu na familia yake walikuwa wanatafuta sababu ya kuivunja ndoa tofauti na ile ya matatizo ya uzazi. Kwa miaka mitatu maisha yalikuwa magumu yaliyojaa msongo wa mawazo mpaka September 2016 mke wangu alienda kwao matembezi ya kawaida baada ya wiki moja nampigia simu ananiambia yeye hatarudi tena kwangu nimpe talaka yake tu basi. Siku hiyo hiyo nikamtumia talaka yake ndiyo ukawa mwisho wa ndoa yetu.

January 2017 nikaoa mwanamke mwingine,ninamshukuru Muumba wa Mbingu na Nchi tunaishi kwa furaha kuliko kwenye ndoa ya mwanzo kabla na baada ya kugundulika Nina tatizo. Tena mke wangu wa sasa ana umri mdogo kuliko yule aliyekimbia(QUOTE]Pole sana mkuu! Naona nami naelekea huko.
 
Kuna watu wenye uhitaji na hawapati watoto na kuna wengine ambao kiuhalisia waweza sema hawafai kuwa wazazi wanatotoa kila kukicha!

Mungu hana formula hufanya akitakacho! Ila amini nakuambia nishaona watu waliokuwa kwenye shida kama yako na Mwenye Enzi akaja kuwafuta machozi muda ambao hawakutarajia! Kukata tamaa ni mwiko....usiache mlilia Muumba wako daima!
NB: Kuna watu pia naamini Mungu anakuwa kawaweka mahususi walee watoto wenye uhitaji. Kuwa mzazi si lazima uzae wako japo najua kuna raha yake spesheli hapo.
Mungu akakupe amani yake maana ndo kitu pekee chaweza kutuliza uchungu unao upitia kwa sasa
 
Haya Mambo hayatabiliki, kuna mtu kaambiwa hawezi kuzaa Homoni haziko balance mtoto wa watu kalia mpk ndoa ikavunjika. Cha ajabu ss hv Ana mimba ya miezi 6 huko.
Mungu huwa anataka kuanzia pale wanaadam wanapishindwa
Noted.
 
Hujanielewa. Tatizo lipo kisaikolojia zaidi. Mtoto akikua utamwambia yeye alipatikana nje ya fallopian tube ?
Kwaiyo mtoto.wako akikua..hua unamwabia Mimi na baba yako tulifanya Mapenzi ukatokea....Mimi sijawai ambiwa...WEWE Mama yako alikwambia alikuapataje...labda kwa mganga?
 
Tofauti ipo bwana,mtoto wa testtube na mtoto anaepatikana kwa natural ya Mungu alivyoumba.
Sasa...WEWE unakataa huyu mtoto was test tube ambae Mama Yake anabeba mimba ya miezi Tisa na anamzaa ...je huyu a surrogate ambae Ni yai na mbegu za Mama Yake.. lakini anaebeba mimba Ni mwingine..?
 
Kuna yule mama .......Magese aliaminishwa hawezi kuzaa hadi alifanya vipindi kwa TV's kuelimisha kuhusu tatizo alilokuwa anaaminishwa kuwa ndio sababu ya yeye kutoshika mimba ( endometriosis), cha ajabu kazaa
Yule alipandikizwa zaidi ya Mara kumi
 
Wale tuliowahi kuambiwa taarifa hizi za kusitkitisha na kuvunja moyo njooni tupeane moyo na nguvu za kuendelea na maisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
Lazima ufe ukiwa unapambana.
Haiwezekani mtu kutembea juu ya maji kisayansi lakini yesu alitembea na kumuwezesha Petro kutembea.

Mwili wa binadamu unaumbika kila siku hivyo viungo vinabadilika kila siku muundo na utendaji kazi.

Via vya uzazi leo vyaweza visiwe na uwezo wa kubeba au kutungisha mimba ila kesho vikaweza kufanya kazi hiyo kwa kuwa vinakua ama kubadilika kiutendaji kutegemeana na hali uliyopitia maishani kama ajali,msongo wa mawazo,matumizi ya madawa fulani pindi unaumwa ugonjwa fulani.

Mtu aweza shindwa kubeba mimba kwa
1.matatizo ya kawaida ya viungo vya uzazi.
2.matatizo ya kishirikina
3.migogoro ya kijamii ktk kuoa na kuolewa inayosababishwa na migogoro ya wazazi au ndugu .
4.mengineyo.

Yote hayo manne yana tiba kwa njia za hospitali,njia za maombezi,njia za jadi au kwa kuisha yenyewe pasipo kutumia dawa yoyote.

Matatizo haya yanawatesa hasa wanawake.Usikubali kuambiwa haiwezekani kuzaa wakati uko hai na bread unaenda vizuri.Hivi hamjui kuwa bread ni yai lililokosa mbegu ya kutungisha hivyo linaharibika.

Wafipa tuna msemo wetu tunasema Kezyaa umulembo yaani kujaribu ni dawa.
Msivunjwe mioyo na watu ambao ni chanzo au sehemu ya shida ziwapatazo.Bado nina amini hakuna mwanamke mgumba unless otherwise mgumba ni yule ambaye hajawahi na hawezi kwenda bread kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Daaaaaa.....shemeji yenu alibahatika kupata ujauzito lakin ndan ya miezi miwili na nusu ikaharibika...na apo baada ya kusota miaka 4 bila majibu.
 
Back
Top Bottom