Wale ambao tulikuwa hatuna hela tangu kitambo ila sasa tunasingizia Corona tukutane hapa

The Initiator huru

JF-Expert Member
Dec 4, 2017
1,530
1,733
Wakuu binafsi mm sio tajiri ila nina ndoto za kuwa tajiri, hata hivyo namshukuru mungu maisha yanasonga japo napata ka hela kakubadilisha mboga Mwenyezi Mungu apewe sifa na utukufu.

Sasa hivi corona amekuwa mtetezi wangu mkuu, yaani hata mtu akiniomba hela na nikiwa sina na singizia corona, nikipewa kadi za michango sijui ubariko harusi, nikiwa sina siogopi kusema sina na lawama zote kwa bwana corona.

Wife akiniambia ninunulie vitu kadhaa nikona gharama ni kubwa namshauri tununue vingine ili tubane matumizi, but lawama zote kwa bwana corona.

Sio mimi tuu hata baadhi ya marafiki zangu tukiwa tunachat lazima lawama kwa bwana corona japo maisha yapo vilevile , ila tuu tunamsingizia bwana corona.

Haya wadau ambao tunatumia hii mbinu kumbe hatuna fedha na maisha hayajabadilika tukutane hapa.

Enjoy the rest of the day
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom