Wale ambao tukisema kitu kinatokea kweli tujuane hapa

chongoe

JF-Expert Member
Mar 22, 2019
1,128
2,717
Nakusudia sisi ambao tukiongea jambo Mara nyingi huwa linatokea mpaka mda mwingine watu wanahisi labda mchawi naleta Kisa changu wakati nipo mdogo nikiwa nasoma shule darasa tatu nakumbuka hio siku ilikuwa naitaj daftari mbili na pesa bibi hakuwa nayo kwakuwa wazazi wangu wamefariki kwa ajali kuzama baharini wakaniacha nikiwa na miaka miwili kwaiyo ilikuwa naishi na bibi tu.

Sasa wakati naelekea shule nikakutana na jamaa mmoja ambae tuna udugu nae alafu maisha yake sio mabaya baada ya salamu Mimi nikamuomba pesa nikanunue madaftari mawili yule jamaa akanambia pesa anayo Ila hanipi nikimuuliza sababu akasema sikupi tu basi jamaa kwa kuniringishia akatoa pesa zile ili nizione makusudi tu baaada kutoa pesa japo sio zangu ila nilihuzunika mno nikajikuta naropoka tu zitapotea hizo maana alikuwa nazo shilingi laki na nusu baada hapo mi nikaondoka zangu.

Sasa yule jamaa Akaelekea zake pwani kununua samaki baada ya mda ilichukua kama SAA moja akaja maeneo ya nyumbani kuniulizia alipoulizwa imekuaje ndio akatoa mkasa mzima kuwa pesa zake zipotea na wala hakuna hata sehem aliyokaa baada kutoka ongea na Mimi ikabidi jamaa anivumishe mj mzima kuwa Mimi mwanga ila ilimpa tabu sana bibi ile hali ila mi niliona kawaida.

Kisa cha Pili kilimkuta mwalim wangu wa shule alisingiziwa anazini na mwanafunzi wake ila ilikuwa uongo tu wanamzushia sasa mida ya jioni kuna siku nilienda kumsalimia Mimi maisha yangu unga unga mwana kama nilivyosema naishi na bibi tu hali zake ngumu kwaiyo mda mwingine napiga msosi kwa mwalimu nilipofika kwake alikuwa mtu wa huzuni tu kwakuwa lile jambo lina muharibia Kusingiziwa basi pale pale nikasema kumwambia mwalimu kama umesingiziwa Mungu awaangamize waliozusha huu uzushi mwalimu aliitikia ameen.

Nikapiga msosi nikarudi home sasa kufika usiku nakuja kuamshwa kuna watu wamekufa wa familia moja baada ya samaki aina ya kasa na ile familia ndio iliozusha uongo kwa mwalim. Nakumbuka baada kupata ile habari ya msiba haikuchukua mda mwalim alikuja nyumbani akiwa na mkewe usiku ule ule tulikaa nje watu wa nne Mimi nikiwa na bibi yeye akiwa na mkewe alikuja kuniambia nisisimulie Yale maneno na wala nisiwe na tabia ya kuongea nikiwa na hasira kwakuwa nilikuwa mdogo niliona kawaida tu , ninavy visa vingi tena vya watu wadoria walivyo potea siku nne baharini letenu na nyie wenzangu wenye midomo mibaya.
 
Nakumbuka tulikuwa na msichana wa kazi pale nyumbani wakati tu wadogo.
Sasa alikuwa akiota kitu anahadithia halafu vinatokea kweli. Bi mkubwa akampiga marufuku kuhadithia vitu anavyoota maana aliota matukio mawili na yote yanatokea ndani ya wiki baada ya kuota.

Tukio la kwanza aliota tumeibiwa, ndani ya siku nne wezi wakaja wakavunja kioo cha gari na kuiba vifaa vya gari kama redio, betri, taa, bumper n.k. Yaani kwa kifupi gari lilibaki kopo tu hamna hata tairi japo injini waliiacha.

Kisa cha pili aliota kuna mtu kafariki. Yaani ndani ya siku tatu taarifa zikaja shangazi yetu kavuta. Bi mkubwa akaona huyu dada anatuweka roho juu juu na ndoto zake, akamwambie akiota vitu akaenavyo moyoni tu.
 
Darasa la 3 unaijua laki nanusu? kisa kizuri Mimi pia nimhanga lkn saiv kidogo. Natabir kwa shida shida naweza nikaona kabisa lkn nikashindwa kumwambia mtu upesi mpaka Jambo linatokea. Nabakia naumia moyoni mwenyewe kwann sikusema
 
Zamani kidogo nilikuwa secondary mawazo yalinijia tu kichwani kuwa Kuna ajali mbaya ya basi imetokea, na kweli jioni yake basi likauwa watu zaidi ya 32.
Mwaka 2006 kwa mara ya kwanza na mwisho nilimwona sehemu JPM nikajisemea moyoni huyu Bwana Kuna siku atakuja kuwa Rais na kweli amekuwa.
Sikumbuki pia mwaka gani nilimwona Jk anatoka bank crdb ilikuwa mkoani nikajisemea moyoni pia huyu Bwana Kuna siku atakuwa Rais na kweli akawa na sijawahi kumwona tena katika maisha yangu.
Matukio ni mengi tu lakini ya nakuja kwa hisia tu. Kuna siku nilihisi ndege imeanguka asubuhi kuamka nasikia Malaysia Air imetunguliwa Ukraine.
Nawaachia wengine waendelee
Kila ukimwona mtu once and for all, lazima awe Rais --- dah tunamleta Majaliwa & Silinde this time from 2055 baada ya Chuma
 
Ndugu sio mdomo tu, hata uandishi wako ni tatizo. Hakuna nukta wala mkato wala paragraph? chongoe
Kuwa makini mkuu, asije sema Jambo kuhusu wewe pia

Anyway Mimi shemeji yangu akiota usiku mtu flani amechimba, Basi kesho mtu wa karbu na huyo mtu alieota tunamzika
 
Katika habari ya kuota na kutokea au kusema na Jambo kutokea kuna mambo mawili.Nguvu kutoka kwa Mungu au Shetani.Nguvu hiyo kutoka kwa Mungu inaitwa Kipawa au inaitwa Karama kwa yule aliyeokoka ila kipawa mtu anazaliwa nacho but karama mtu anapewa na Roho Mtakatifu (1Wakor 12).

Lengo la Mungu kutupa kipawa au karama lengo ni kufaidiana na kukamilisha watakatifu.Ukiona unatumia hivyo vitu kwa ubaya au nia ovu ujue unatumika na shetani.Pia ukioneshwa mabaya unatakiwa ukemee ili yasitokee na kama mema kuyaombea yatokee pia jifunze kunena mema yatokee tumia ulimi wako kubariki na si kulaani.

Barikiwa.
 
Back
Top Bottom