mgonga
Senior Member
- Oct 26, 2018
- 174
- 560
- Thread starter
- #21
Asante kwa niaba yao!inahuzunisha sana tu,sema ndo kazi ya Mungu haina makosa!poleni wote ..inauzunisha sana...
Sent using Jamii Forums mobile app

Njooni tuwatakie heri na baraka tele huko walipo!R.I.P Mama,we miss u mama!
View attachment 1445888
Sent using Jamii Forums mobile app
Nikikumbuka siku nakuchukua hospitali, madaktari wakisema urudi tu nyumbani hamna namna...ugonjwa(cancer) umeenea mwili mzima, ukibaki hospitali gharama zitaongezeka...Nililia sana, nawe ulilia sana....ukiniambia, "mwanangu God Heals, madokta wameshajua hali ni mbaya...sina mda wa kuendelea kuishi. Umenipambania tangu siku ya kwanza miaka 5 iliyopita....leo imefikia." Uliongea kwa uchungu sana...tukarudi nyumbani....ukanisihi mengi sana, ukanikumbusha mengi sana, na ukaniomba niendelee kuwapenda wadogo zangu.
Ukanitania....ukilazimisha furaha, "mwanangu God Heals naondoka bila kumwona mjukuu wangu...ningependa sana kumbeba mme au mke mwenzangu, ila naondoka bila kumwona mjukuu..." Tukacheka huku mioyo ikiuma sana. Lilikuwa tabasamu la mwisho....
Nakumbuka kesho ukaomba nimpigie dada aje nyumbani, aje na mjukuu wako....kweli nilifanya hivyo...nao wakafika.... Tukaongea tukiwa na hudhuni sana... ukawa unajitahidi kutabasamu huku ukilalamika moyo unakuuma, mara mbavu, mara miguu, mara kichwa, mara mikono.... Ukatuangalia wote, kila mmoja kwa wakati wake... Ukiwa mbele ya mumeo kipenzi, watoto wako watatu, mjukuu wako mmoja, ukaanguka chini... ukajilaza... na hukufumbua macho tena.
Ni miaka 6 sasa imepita, Pumzika kwa amani mama, pumzika salama...katika siku hii sina pa kushika kila nikikumbuka maneno yako, na wakati ule mgumu, wa mwisho pale hospitali. Tutakumbuka kwa nasaha zako. Hakika ulikuwa mwema kwetu.
Lala salama mama yetu kipenzi.
Jazaak allahu khairPoleni sana wote jamani
Kwa kuwaenzi watoleeni sadaka mara kwa mara ni nzuri sana
Poleni tena
Sent from my iPhone using Tapatalk
ooh pole sana, Mungu ampumzishe.PUMZIKA KWA AMANI MAMA YANGU,LEO NI WIKI TOKA ULIPOTANGULIA MBELE YA HAKI,MWENYEZI MUNGU AKUONDOLEE ADHABU YA KABURINI,AKUSAMEHE DHAMBI ZAKO,AKUPE KAULI THABITI NA ALIFANYE KABURI LAKO LIWE LENYE MWANGA WA BARAKA 🤲

Daaah pole sana nduguNikikumbuka siku nakuchukua hospitali, madaktari wakisema urudi tu nyumbani hamna namna...ugonjwa(cancer) umeenea mwili mzima, ukibaki hospitali gharama zitaongezeka...Nililia sana, nawe ulilia sana....ukiniambia, "mwanangu God Heals, madokta wameshajua hali ni mbaya...sina mda wa kuendelea kuishi. Umenipambania tangu siku ya kwanza miaka 5 iliyopita....leo imefikia." Uliongea kwa uchungu sana...tukarudi nyumbani....ukanisihi mengi sana, ukanikumbusha mengi sana, na ukaniomba niendelee kuwapenda wadogo zangu.