Wale ambao bado tunafuatilia Kitambulisho/Namba ya NIDA tukutane hapa

vampire123

JF-Expert Member
Apr 17, 2016
1,285
820
Habari wakuu,

Kiukweli hili jambo linakera mno, mimi nilifanikisha mambo yote yaliyoitajika kama vile copy ya cheti cha kuzaliwa, cheti cha shule na baadhi ya vitu vingine ili niweze kupata namba au kitambulisho cha NIDA ambapo ilikuwa mwezi wa 9 mwaka jana yaani 2019 mpaka leo hii nishaenda zaidi ya mara 10 na kila nikienda naambiwa njoo wiki ijayo mara nyengine njoo baada ya wiki mbili hadi mwezi.

Hadi hivi sasa sijapata hata namba, yaani mpaka nachoka sasa. Kiukweli hili jambo linakera na linaumiza sana.
 
Wewe fomu yako itakuwa imepotea. Hawakwambii ukweli


Hili zoezi siku hizi ni jepesi sana.. kama unekamilisha kila kitu haizidi wiki 2 unapata namba
 
Mi' mwenyewe ni tangu mwezi wa Saba 2019. Hadi leo mpaka nishakata tamaa
 
Hapana mkulu hauko peke yako mbona ili zoezi linaonekana kama limewashinda kea ujumla....

Wamebakiza mikwala tu,
 
Mimi naomba kuuliza siku hizi ukishapewa namba ya NIDa ndiyo basi au?
nakumbuka May mwaka huu nilimcheki kachaa kuhusu izi delay, akanambia 'subiri' tunajenga kiwanda cha kutengeneza 'kadi' uko Kibaha, utataarifiwa kwa SMS 😆😆
ndio ikawaa ntolee iyo
 
~ Watu wengi hawajapata namba na vipi ID,labda kwenye kampeni watatoa tusubiri,ingekuwa ID za nida unapigia kura kila mtu angepata hata wakenya.
 
Back
Top Bottom