Walaji wa kitimoto tujuzane kijiwe kipi kizuri kwa hapo ulipo

Zero IQ

JF-Expert Member
Dec 21, 2016
13,917
24,674
Tujuzane kijiwe kipi kizuri kwa hapo ulipo kinapika kitimoto chenye Quality yaani ukigusa utatamani kesho uje tena?

Kama mnavyojua Utamu wa kitimoto upate na ugari au Ndizi za kukaanga,nimeshapanga ratiba yangu leo lazima nikale kitimoto.

IMG_20181122_084058_797.jpeg


IMG_20181122_084115_807.jpeg


Nb:
Mashekhe na Maustadhi tafadharini sana msije kuutia shombo uzi huu,

Huu ni kwa sisi wala kitimoto tu ukiona haukufai kafanye mengine siyo kuja hapa.


Cc Zero IQ

==========

Nyama ya nguruwe ni nyama laini na yenye ladha nzuri inapopikwa vizuri, nyama hii inamapishi ya aina tofauti tofauti na leo nawaletea mapishi ya rosti. Unaweza kujiandalia nyama hii mwenyewe nyumbani na ukafurahia utamu wake.

Mahitaji
  • Nyama ya nguruwe 1/2 kilo
  • Nyanya zilizoiva 6
  • Karoti 2
  • Pilipili hoho 1
  • Ndimu 1 kubwa
  • Chumvi kiasi
  • Mafuta vijiko 2 vikubwa
  • Vitunguu saumu 2

Matayarisho

1. Safisha nyama kisha kata kata vipande vidogo kiasi kulingana na unavyopendelea na kisha weka kwenye chombo kikavu.

2. Menya vitunguu saumu na vitwange.

3. Changanya nyama yako na vitunguu saumu, kamulia ndimu na weka chumvi kiasi cha kutosha.

4. Bandika kikaango chako jikoni kisha weka mafuta kiasi kama nyama yako haina mafuta ya kutosha na yakianza kuchemka weka nyama yako.

5. Ukiwa unasubiria nyama ikauke na kuwa ya kahawia ( kumbuka kuigeuza geuza lakini usiifunikie), kwangua nyanya zako na karoti kwa kutumia grater au blender (kwangua nyanya tofauti na karoti) na kata kata pilipili hoho katika vipande vidogo vidogo.

6. Nyama ikiwa imeshabadilika rangi na kulainika vizuri weka karoti yako uliyoikwangua na koroga ichanganyike vizuri na nyama, acha iive kwa muda mfupi kisha weka na hoho zako. Vikilainika weka nyanya yako uliyoisaga na kukoroga vizuri kisha acha ichemke bila kuifunikia huku ukiwa unaigeuza geuza.

7. Ikiwa tayari epua na iandae ikiwa bado moto. Inaweza kuliwa kwa ugali, ndizi za kukaanga, viazi vya kukaanga, viazi vya kusaga n.k

Michango ya wadau:

Hii ndio nyama bora kabisa iliyobakia baada ya nyama ya mbuzi na ngombe kuingiliwa na wadudu hatari wanaoongeza uric acid, gauts na matatizo kibao ya viungo, magoti na mfumo wa damu.

Watafiti mtuambie nini kimetokea kwenye ngombe na mbuzi? nyama hizi ni hatari kubwa sasa, magoti yanavimba , yanauma, visole vinavimba na kukakamaa kuna nini?

je ni dawa wanazowatibu wanyama hawa au ni species mpya za mbuzi na ngombe ama ni GMO? mbona zamani hakukuwepo matatizo kama haya?
----
Amatolo, Nyama ya nguruwe siyo ngumu sana wala nyepesi sana, ipo katikati kwa ugumu, japo nyama ya ng'ombe ni ngumu zaidi. Kwa maana hiyo nyama inapokuwa ngumu na ina mafuta inashauriwa iliwe na kinywaji ambacho ni chachu au acidity kwa mfano wine.

Kitimoto kwa hapa Bongo, wengi hawapiki inavyotakiwa, kwa maana hiyo kienyeji kienyeji tunashauriwa ukila, basi shushia na spirit au whisky ili kuua vimelea au minyoo. Hii ni kimtaa zaidi na sio kidaktari.
 
Tujuzane kijiwe kipi kizuri kwa hapo ulipo kinapika kitimoto chenye Quality yaani ukigusa utatamani kesho uje tena?

Kama mnavyojua Utamu wa kitimoto upate na ugari au Ndizi za kukaanga,nimeshapanga ratiba yangu leo lazima nikale kitimoto.

View attachment 942375

View attachment 942377

Nb:
Mashekhe na Maustadhi tafadharini sana msije kuutia shombo uzi huu,

Huu ni kwa sisi wala kitimoto tu ukiona haukufai kafanye mengine siyo kuja hapa.


Cc Zero IQ
Kuna sehemu moja pale tanga wanatengeneza kitimoto tamu balaaa...............

nimepasahau jina ila ni jiran na round about ya kwanza ukitokea pongwe kabla hujaingia mjini
 
"Katika wanyama woote walioumbwa kitimoto kaumbika kuliko woooteeee🎶🎶,kapewa na mafuta na nywele za kizungu na kamkia kafupiii pale kwa nyumaaaa,.upate kachumbari na ndizi za kuchoma na kaserengeti baridiii pale pembeniii🎶🎶🎶🎶"
 
Back
Top Bottom