ELFU-ONEIR
Senior Member
- Jun 27, 2012
- 181
- 64
Huyu mama ni mama wa watoto wa4,mwanae wa mwisho amemaliza chuo mwaka juzi na ameanzisha mradi wake wa kuku wa mayai.Mume wa mama huyu alistaafu kazi mwaka 2007.Lakini maisha yake hayajabadilika kutokana na miradi ya familia iliyoanzishwa na mkewe.Mama huyu hakuwahi kusoma utotoni,hii inamaana wakati anaoelewa na mumewe alikua hajui kusoma wala kuandika.Ni mwaka 92 ndipo alipojifunza kusoma na kuandika na alikua na umri wa miaka 35!Aliolewe akiwa na miaka 14!Mumewe mama huyu hupenda kumuita huyu mama kiongozi,humuita hivyo kutokana na mama huyu huwa kiongozi hasa.Mumewe mama huyu anasema,"maduka yote matatu,mashamba ya mpunga kule Bariadi,nyuma tano tulizopangisha pamoja na dispensary vyote ni mawazo na usimamizi wa mke wangu.Unajua wakati nafanya kazi sikua napata muda wa kutulia,nilipokua narud nyumbani kutoka safari mke wangu alikua ananiweka kitako na kuniuliza kama kuna hela nimeibakisha kutokana na malipo ya safari ofisini baada ya matumizi safarini,na nilipofanya ubishi alikua mkali kwelikweli.Kutokana na mabaki hayo ya safari na akiba ya mshahara ambayo yeye ndo alilazimisha iwepo aliweza kufanya hayo niliyokueleza,na pia ameanzisha mradi wa kuwasaidia akina mama wenzake kwa kujikwamua kiuchumi kwa kuwakopesha pesa,anasema ndoto zake ni kuja kuanzisha benki".Hayo ni baadhi tu ya ushuhuda wa anayoyafanya mwanamama huyu ambae kafanya mazuri na hakuwahi kwenda shule tofauti na kujifunza kusoma na kuandika tena ukubwani.Hivi ingekua leo mama huyu angeolewa?Kwa jinsi tunavyopimana kwa elimu,rangi na pesa sidhani kama kuna kijana yoyote anaweza kuwa na mke/mume wa aina hii.Tunadhani elimu ndo inamfanya yoyote awe na ubinadamu tunaishia kujuta maishani,sisemi watu wasisome au shule haina maana,hapana,ila kuamini kwamba ukishasoma,au ukawa na hela haimaanishi una uelewa wa yote.Au ukioa/olewa na "msomi" basi ndoa yako itakua na furaha na mafanikio la hasha.Huyu mama amekua msaada kwa familia yake na jamii inayomzunguka,ingekua leo si angeonekana sio binadamu na hastahili kuolewa na msomi kama mumewe?Binadamu wote ni binadamu,vitu vya nje haviwezi kubadili ukweli huu!
anapatikana wapi huyu bibie je naweza pata contacts zake? nadhan huyu anafaa kuwa mfano wa kuigwa duniani kote