Walah tungeathirika leo endapo tungepoteza hazina hii!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Walah tungeathirika leo endapo tungepoteza hazina hii!!!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Eiyer, Aug 23, 2012.

 1. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #1
  Aug 23, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,675
  Trophy Points: 280
  Huyu mama ni mama wa watoto wa4,mwanae wa mwisho amemaliza chuo mwaka juzi na ameanzisha mradi wake wa kuku wa mayai.Mume wa mama huyu alistaafu kazi mwaka 2007.Lakini maisha yake hayajabadilika kutokana na miradi ya familia iliyoanzishwa na mkewe.Mama huyu hakuwahi kusoma utotoni,hii inamaana wakati anaoelewa na mumewe alikua hajui kusoma wala kuandika.Ni mwaka 92 ndipo alipojifunza kusoma na kuandika na alikua na umri wa miaka 35!

  Aliolewa akiwa na miaka 14! Mumewe mama hupenda kumuita huyu mama kiongozi,humuita hivyo kutokana na mama huyu huwa kiongozi hasa. Mumewe mama huyu anasema,"maduka yote matatu,mashamba ya mpunga kule Bariadi,nyuma tano tulizopangisha pamoja na dispensary vyote ni mawazo na usimamizi wa mke wangu.Unajua wakati nafanya kazi sikua napata muda wa kutulia,nilipokua narud nyumbani kutoka safari mke wangu alikua ananiweka kitako na kuniuliza kama kuna hela nimeibakisha kutokana na malipo ya safari ofisini baada ya matumizi safarini,na nilipofanya ubishi alikua mkali kwelikweli.

  Kutokana na mabaki hayo ya safari na akiba ya mshahara ambayo yeye ndo alilazimisha iwepo aliweza kufanya hayo niliyokueleza,na pia ameanzisha mradi wa kuwasaidia akina mama wenzake kwa kujikwamua kiuchumi kwa kuwakopesha pesa,anasema ndoto zake ni kuja kuanzisha benki".Hayo ni baadhi tu ya ushuhuda wa anayoyafanya mwanamama huyu ambae kafanya mazuri na hakuwahi kwenda shule tofauti na kujifunza kusoma na kuandika tena ukubwani.Hivi ingekua leo mama huyu angeolewa?Kwa jinsi tunavyopimana kwa elimu,rangi na pesa sidhani kama kuna kijana yoyote anaweza kuwa na mke/mume wa aina hii.Tunadhani elimu ndo inamfanya yoyote awe na ubinadamu tunaishia kujuta maishani,sisemi watu wasisome au shule haina maana,hapana,ila kuamini kwamba ukishasoma,au ukawa na hela haimaanishi una uelewa wa yote.

  Au ukioa/olewa na "msomi" basi ndoa yako itakua na furaha na mafanikio la hasha.Huyu mama amekua msaada kwa familia yake na jamii inayomzunguka,ingekua leo si angeonekana sio binadamu na hastahili kuolewa na msomi kama mumewe?Binadamu wote ni binadamu,vitu vya nje haviwezi kubadili ukweli huu!
   
 2. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #2
  Aug 23, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  huyo mama kafika hapo si tu kwa juhudi zake binafsi bali pia kwa sababu ya mume mwelewa aliye nae....
  tena hii wanaume waichukulie kama changamoto, wanaume wangapi ambao wana mali hawataki wake zao wajue?
  wanaume wangapi ambao mnawaficha wake zenu kipato?
  wanaume wangapi ambao mna akaunti a siri?
  wanaume wangapi ambao mnaachisha wake zenu kazi kwa ajili ya inferiority zenu au wivu usiokuwa na maana?
  wanaume wangapi wanaokubali wake zao kujishughulisha? unakuta wanaume wengine mke kaanzisha kibiashara kikikua wateja wakija asiwachangamkie(hususan wa kiume)

  familia inayoshirikiana na kufanya kazi pamoja ndiyo inayofanikiwa......
   
 3. V

  Von Mo JF-Expert Member

  #3
  Aug 23, 2012
  Joined: May 7, 2012
  Messages: 1,830
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana na hili, kuwa kujua kusoma na kuandika ni shule tosha kabisa, kama mtu anawaza maendeleo na si fasheni lazima mfike mbali
   
 4. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #4
  Aug 23, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,675
  Trophy Points: 280
  BADILI TABIA,nimefurahi kwa kuuona mchango wa mume pia,lakini uliyosema ni kweli,tatizo wanaume wengi hawajiamini,na kama hujiamini ni vigumu sana kumuamini mtu yoyote!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #5
  Aug 23, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,675
  Trophy Points: 280
  Point ya msingi hapa binadamu hafanywi bora na elimu kwani hata kabla ya elimu binadamu alikua hajapungukiwa chochote!
   
 6. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #6
  Aug 23, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Biashara saa nyingine ni Kipaji na bahati na elimu huja kusaidia kuboresha zaidi na kucontrol mapato na matumizi. Naamini angekuwa na ka-elimu zaidi kidogo, yumkini huyo mama tayari angekuwa amefungua bank na kuwa hata na mahoteli makubwa au mabasi ya kwenda mikoani kama siyo kuwa na kampuni yake kubwa! Nilikuwa najaribu kufikiria, kusoma na kuandika kajifunza mwaka 92, which means kabla ya hapo alikuwa anafanyiwa mahesabu na watu, Je, hakuwa anaibiwa kweli? Hakuwa anapewa ripoti za uongo za mapato na matumizi?

  Kwa upande mwingine wa shilingi, nakubaliana na wewe Eiyer kuwa saa nyingine tusikubali kupoteza wapenzi wetu tunaowapenda kwa dhati kwa sababu ya elimu duni walizonazo au kutokana na katabia fulani ambacho hakana madhara sana na kanarekebishika. Ni vyema kujitahidi kumuondoa mpenzi wako kwenye udhaifu wake (kama elimu ndogo, mpe moyo ajiendeleze!), badala ya kutafuta kitu "ready made" mara nyingi mahusiano haya huwa hayana unyenyekevu na upendo wa kweli.

  Ni mtazamo wangu tu ....

  HP
   
 7. Billie

  Billie JF-Expert Member

  #7
  Aug 23, 2012
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 5,341
  Likes Received: 2,351
  Trophy Points: 280
  Elimu kubwa siku hizi inaua nguvu kazi ya Taifa.Mi nilikuwa mlimaji mzuri wa jembe la mkono ila nilivyochaguliwa boarding skul o-level n A-level na kwenda chuoni nimejikuta siwezi tena kulima hata kupalilia maua ya nyumbani siwezi na hata nikifanya hivyo naona najitafutia ugonjwa tu.KWELI ELIMU YETU INATUFUNDISHA KUWA WAVIVU WA KAZI ZA VITENDO NA KUWA WAONGEAJI NA WALALAMIKAJI WAZURI KUTOKANA KUWA NA MAARIFA MENGI YASIYOAMBATANA NA NGUVU KAZI.
   
 8. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #8
  Aug 23, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,788
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  DUU mke wangu ana digrii hata kuku hajui kufuga!lol!wanawake wa dot com tabu tupu wapo busy na facebook
   
 9. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #9
  Aug 23, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,675
  Trophy Points: 280
  HorsePower,kwanza niambie bahati ni nini,halafu inakuwaje unadhani kuwa kama angekua na elimu angekua zaidi ya hapo?Kwanini unadhani aliibiwa.Kuna mzee mmoja,mpaka anafariki alikuwa hajui kusoma wala kuandika lakini alikuwa na utajiri wa mifugo,majumba,magari n.k,lakini kwenye "kalkuleta" humuibii na aliendesha utajiri wake vyema.Kama elimu iko kama unavema mbona wapo wenye eilimu ambao hata nusu ya mama huyu mama wameshindwa?Kufanikiwa maishani(kujitambua na kupata unachohitaji) hakuhusiani na sayansi wala "jogo"!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #10
  Aug 23, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,675
  Trophy Points: 280
  Hili nalo neno mkuu . . . . . .!!
   
 11. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #11
  Aug 23, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,675
  Trophy Points: 280
  Ukweli wa aina hii utatusaidia kujitazama na kutambua tulipokosea,na kujua ulipokosea ni moja ya hatua ya kwenda kwenye mafanikio maishani!
   
 12. Mnama

  Mnama JF-Expert Member

  #12
  Aug 23, 2012
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 1,651
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Ha haaaa zaidi zaidi wanajua tu kupanga matumizi ya hela zetu sio kuzalisha zaidi.
   
 13. The Bleiz

  The Bleiz JF-Expert Member

  #13
  Aug 23, 2012
  Joined: Jan 7, 2012
  Messages: 3,643
  Likes Received: 2,113
  Trophy Points: 280
  Huyo Bi mdachi atakua ni mchaga.
   
 14. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #14
  Aug 23, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Wa mama wa aina hiyo hawapo tena katika dunia hii ya leo.. Umesema mwenyewe mama alikua akipata hela zake au za mumewe basi anafikiria kuziweka kwa ajili ya shuhuli ya maendeleo... Wanawake wa leo hii ukimpa hela cha kwanza kwenye akili yake ni shoppin salon ili apendeze kama wanawake wenziwe huko makazini au mtaani akiwa holiday anataka umpeleke south africa mara atakuambia mbona flani kanunuliwa gari zuri na yeye anataka kama hilo sasa mwanamke wa namna hiyo utaweza kweli kumweleza mali zako au una pesa kiasi gani si atazinyonya zote...
   
 15. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #15
  Aug 23, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Nimejifunza kitu na najivunia uwepo wangu hapa jf
   
 16. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #16
  Aug 23, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,675
  Trophy Points: 280
  Unahusishaje hili na kabila????
   
 17. The Bleiz

  The Bleiz JF-Expert Member

  #17
  Aug 23, 2012
  Joined: Jan 7, 2012
  Messages: 3,643
  Likes Received: 2,113
  Trophy Points: 280
  Bz wamama wengi wa kichaga hawana kisomo kiviile lakani wao ndio nguzo kuu katika familia haswa kwenye swala la usimamizi wa biashara.
   
 18. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #18
  Aug 23, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,675
  Trophy Points: 280
  Dada yangu King'asti akisikia umesema haya mi simo,yeye anasemaga eti mwanaume bila hela na elimu ni kama bajaji bila matairi . .Lol!!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #19
  Aug 23, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,675
  Trophy Points: 280
  Na hili ndio lengo kuu!!!!
   
 20. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #20
  Aug 23, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,675
  Trophy Points: 280
  Niambie uzoefu wako kuhusu wamama wa makabila mengine!
   
Loading...