Walaaniwe wote wanaoupotosha umma wa Tanzania - Mhariri, Mwananchi

M TZ 1

Member
Oct 12, 2010
34
3
Ndugu watanzania wenzangu,katika kupitia magazeti mbalimbali yanyoaminika na kuheshimika mbele ya umma wa tanzania nimekutana na makala katika gazeti la mwananchi,nimeona niwaonjeshe utamu wa hii mada,sasa nimeanza kugundua kwanini serikali inalikandamiza hili gazeti.nawasilisha

Tumesikitishwa na jinsi baadhi ya watu na vyombo vyenye mamlaka na ushawishi katika jamii yetu vilivyopindisha hoja zilizotolewa na Chadema kuhusu kitendo cha wabunge wake kutoka nje ya Ukumbi wa Bunge wakati Rais Jakaya Kikwete alipokuwa akilihutubia mwishoni mwa wiki. Wapo watu waliokiona kitendo hicho kama uhaini na wapo waliokiita usaliti wa hali ya juu.

Wote hao walitaka wabunge wa chama hicho wafukuzwe bungeni, kwa madai kwamba wamekataa kumtambua rais aliye madarakani na ambaye pia ni sehemu ya Bunge. Walisema kitendo hicho walichokiita cha udhalilishaji wa Rais lazima kijibiwe kwa nguvu zote. Chama tawala kilitoa tamko kwamba kilikuwa katika mchakato wa kuhakikisha kuwa wabunge wa Chadema wanatiwa adabu.

Lakini wapo pia waliokiona kitendo hicho kama cha kawaida na cha kidemokrasia kabisa kilichokuwa na lengo la kufikisha ujumbe kwa chama tawala na serikali yake kuhusu umuhimu wa kuandika katiba mpya na kusimika tume huru ya uchaguzi baada ya matokeo ya chaguzi nyingi tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992 kuacha maswali mengi yasiyokuwa na majibu. Chadema kilisema kuwa hoja yake hiyo ilikuwa imepindishwa na kupotoshwa makusudi, lakini kilifafanua tena na tena kwamba sio kweli kwamba kilikuwa hakimtambui Rais, bali mfumo uliomuweka madarakani.

Moja ya sauti muhimu katika jamii iliyozungumzia kitendo hicho cha wabunge wa Chadema ni aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa, Samuel Sitta aliyesema kuwa kitendo cha wabunge hao kilikuwa cha kawaida ambacho hakizuiwi na kanuni yoyote ya Bunge pia hakina adhabu yoyote. Alisema wabunge wanaruhusiwa kuonyesha hisia zao kwa kutoka nje ya ukumbi pale wanapotofautiana na jambo fulani. Alikumbushia mwaka 2000 wabunge wa upinzani walipotoka nje kwa kupinga kupitishwa kwa bajeti ya serikali.

Tumeorodhesha mlolongo mzima wa matukio hayo ili kuyaweka katika muktadha wa mgogoro huo na kuwakumbusha wadau wa demokrasia katika nchi yetu kuwa mgogoro uliopo hivi sasa sio kati ya Rais Kikwete na Chadema, bali mfumo uliobuniwa na kulelewa na chama tawala ambao ni katiba ambayo pia ilizaa tume ya uchaguzi. Katika hali hiyo, chama hicho kimetangaza madai matatu ya msingi ambayo ni katiba mpya, tume huru ya uchaguzi na tume huru ya kuchunguza yaliyotokea katika uchaguzi uliopita.

Tunapenda kuamini kuwa madai ya Chadema ni ya msingi katika kutafuta mustakabali wa nchi yetu. Tunaamini pia kuwa madai hayo sio ya Chadema pekee bali Watanzania wote bila kujali dini, kabila au chama cha siasa. Umoja wa kitaifa na amani ambayo imekuwa ikihubiriwa haitakuwapo bila katiba inayokidhi matakwa ya watu wote. Ni katiba mpya tu itakayofuta sheria mbovu kama ile ya uchaguzi ya 1985, inayoipa tume ya uchaguzi madaraka ya kumtangaza rais na kuwanyima wananchi fursa ya kupinga matokeo hayo mahakamani.

Ni katika kupima hali hiyo tunadhani kuwa tume huru ya kuchunguza yaliyotokea katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu pia ni muhimu. Watanzania watahitaji kujua, kwa mfano, kwa nini watu zaidi ya milioni 20 walijiandikisha kupiga kura lakini waliojitokeza ni milioni 8 tu? Nini kilichosababisha watu milioni 12 kutopiga kura au kuchelewa kutangazwa matokeo au katika sehemu fulani matokeo hayo kutangazwa na wakuu wa wilaya badala ya Nec?

Ni bahati mbaya kwamba Rais katika vipaumbele 13 vya serikali yake katika kipindi kijacho hakugusia masuala hayo ambayo Chadema inayadai. Baadhi ya vyombo vya habari vimefanya juhudi za makusudi kuwapotosha wananchi badala ya kuwaelimisha kuhusu suala hili linalohusu muktakabali wa nchi yetu. Sisi tunasema kuwa juhudi za Chadema na wanaharakati wengine zitashinda ili mwishowe upande huu wa Jamhuri ya Muungano nao upate maridhiano kama yaliyopiganiwa vilivyo na CUF huko Zanzibar.
 
Ni wahariri wachache sana Tanzani wenye uhuru na uwezo wa Kupembua mambo kama huyu wa Mwananchi na ningewaomba kampuni yao ianzishe Televishion kama walivyofanya Kenya, nigefurahi yule Mhariri wa Nipashe Jumapili aje hapa asome huu uchambuzi na aombe radhi kwa uharo aliotuandikia Jumapili.
 
Hata mimi nimeshangaa jinsi watu tulivyoupokea mgomo wa CHADEMA, yaani kuna watu wameapiza na kuapiza. Nafikiri kufuatana na kanuni za bunge, ni kitu ambacho kipo na hakina adhabu kama Mh Sitta alivyosema, na kwa wanaofuatilia mabunge ya wenzetu hii sio ajabu. Kuna ambao wanatamani kumbeba mheshimiwa rais kwenye mbeleko (mgongoni) kwa jinsi wanavyoona kama kaonewa mno kwa kitendo hiki.
 
Gazeti la mwananchi liko very independent. Wao kijiko wanakiita kijiko na siyo chuma kilichokunjwa. Tatizo la waandishi wetu wengi wa habari ni kusumbuliwa ama na uoga au njaa. Wanaamuliwa na wanasiasa waandike kitu gani. Ni utumwa wa aina fulani hivi unaowadhalilisha sana (ingawa wao hawajui). Hebu fikiria gazeti kama la Habari leo ambalo limepoteza heshima yake na kuwa kama magazeti ya udaku ya Shigongo. Wamesahau kuwa linaendeshwa kwa kodi zetu na si michango ya wanachama wa CCM.
Big up mwananchi, mwanahalisi na raia mwema. Ole wenu waandishi wanafiki
 
Sio tu wananchi wa kawaida wamepotoshwa, pia baadhi ya wabunge wa upinzani hawakuwaelewa Chadema, sijui ni shule ndogo?
 
Tuna media house chache sana zenye kusema hali halisi kama Mwananchi Communications. Nakereka na Habari Leo kuandika habari kishabiki zaidi kuliko mantiki. Hata hivyo watanzania tunazidi kuimarika kifikra, sasa si tu kwamba tunasoma na kuangalia taarifa mbali mbali bali tuna uwezo wa kupembua taarifa.
 
Na ulaaniwe mwenyewe na uzao wako. Chadema walipoingia kwenye uchaguzi hawakujua kuwa katiba iliyopo ina mapungufu hayo???? Baada ya kushindwa urais ndipo wanatukosea heshima tuliowatuma bungeni. Kudadadeki, walichemsha wapende, wasipende na wote mnaoshabikia upuuzi huo, ...................... ah, bora ninyamaze tu.
 
Naamini wewe mzee kibiongo ni mmoja wa wale wenye macho lakini hawaoni. Kutoka nje ya bunge ni kitendo halali na cha kistaarabu kabisa cha kuonyesha msimamo wao. Chadema hawajavunja sheria yeyote kama 6 alivyosema. Katika nchi yeyote yenye demokrasia lazima uwepo uhuru wa mtu au kikundi cha watu kutoa maoni yao, hiyo ndiyo ilikuwa njia sahihi kabisa kwa chadema kumweleza jk kuwa hayupo pale kwa ridhaa ya wananchi na wao hwatambui ushindi wake ingwa ameshaapishwa
 
Na ulaaniwe mwenyewe na uzao wako. Chadema walipoingia kwenye uchaguzi hawakujua kuwa katiba iliyopo ina mapungufu hayo???? Baada ya kushindwa urais ndipo wanatukosea heshima tuliowatuma bungeni. Kudadadeki, walichemsha wapende, wasipende na wote mnaoshabikia upuuzi huo, ...................... ah, bora ninyamaze tu.

Ee wanajamvi msameheni maana hajui alitendalo.
 
Na ulaaniwe mwenyewe na uzao wako. Chadema walipoingia kwenye uchaguzi hawakujua kuwa katiba iliyopo ina mapungufu hayo???? Baada ya kushindwa urais ndipo wanatukosea heshima tuliowatuma bungeni. Kudadadeki, walichemsha wapende, wasipende na wote mnaoshabikia upuuzi huo, ...................... ah, bora ninyamaze tu.

How old are you???
 
Dogo uwe na heshima!
CHADEMA walipoingia kwenye uchaguzi walijua kuwa KATIBA inamapungufu ndiyo maana walilielezea hilo kinagaubaga katika ILANI yao, na mgombea wa kiti cha Urais toka CHADEMA Dr.(wa ukweli) W. P. Slaa alisema mara nyingi kuwa ataanza kulishughulikia hilo katika siku 100 za kwanza atakapokuwa madarakani.

Ulikuwa unasikiliza nini wakati wa kampeni, Radio uhuru? mipasho?....

Wewe mwenyewe ndiwe unajukisea/jivunjia heshima (japokuwa sina uhakika unayo kwa kiasi gani) kwa kuwa ni mvivu wa kukumbuka na hodari wa kuropoka.

Naomba uendelee kunyamaza,
Invisible said:
Ficha upumbavu wako, usifiche hekima yako
 
Bila ushabiki wa kisiasa madai ya katiba mpya na tume huru ya uchaguzi ni ya msingi kabisa na ni kwa faida ya kila mtanzania mpenda taifa lake na kwa kizazi hiki na vizazi vijavyo. Kwa maana hiyo basi kila mtanzania mzalendo hana budi kuunga mkono madai haya.
 
Na ulaaniwe mwenyewe na uzao wako. Chadema walipoingia kwenye uchaguzi hawakujua kuwa katiba iliyopo ina mapungufu hayo???? Baada ya kushindwa urais ndipo wanatukosea heshima tuliowatuma bungeni. Kudadadeki, walichemsha wapende, wasipende na wote mnaoshabikia upuuzi huo, ...................... ah, bora ninyamaze tu.
Yawezekana ni upuuzi. Kila mtu ana namna yake ya kupima mambo. Waweza ona upuuzi lakini umefikiria huo upuuzi unavyoweza okoa shari tuendako? Unadhani watu wataendelea kuwa watulivu siku zote huku wakiamini kuwa wanadhulumiwa? Umesikia yaliyotokea Shinyanga, Karagwe, Mwanza na kwingine, je, watu wale walichochewa na nani? Kama watu wataendelea kukandamizwa amani lazima itatoweka.
Hii ni kanuni ya maisha ya mwanadamu duniani pote, rejea yaliyotokea Philipines, China, Marekani na kwingi duniani. Kunapotokea ukandamizaji, hatua ya pili ni kupingwa kwa ukandamizaji, tatu ni namna ya upingaji na mwisho ni vita. Congo wanapigana mpaka leo sababu ya Marehemu Mobutu, Burundi uasi unaendelea, na Tanzania haipo peponi. Mwaka huu 2010, mmeshuhudia watu wakipigana na kuuana na polishi kupiga mabomu ya machozi kila sehemu. Kwa mfumo huu wa kukibeba chama kilicho madarakani, naiona vita kuu siku si nyingi.
Mlio vipofu mtadhani CHADEMA wataanzisha vita, amini nawaambia vita itatokana na mfumo unaowalinda watawala. Na itakuwa vita kati ya watawala na vibaraka wao dhidi ya wananchi waliochoshwa na ukandamizwaji. Kwa taarifa tu, kuna jeshi kubwa la vijana wenye umri wa kuanzia miaka 13 ambao miaka 5 ijayo watapenda kuona mabadiliko. Kama 2005 waliandikishwa milioni 9, 2010 milioni 20, mwaka 2015 je? Wapenda amani na si madaraka tafakari, chukua hatua!!!!!!!!!
 
Nakubaliana na mhariri hapo

Wana Chadema naona mmemfagilia sana huyo mhariri lakini kesho akija na issue ya kukosoa Chadema wote mtasema amenunuliwa na mafisadi!
 
Ni wahariri wachache sana Tanzani wenye uhuru na uwezo wa Kupembua mambo kama huyu wa Mwananchi na ningewaomba kampuni yao ianzishe Televishion kama walivyofanya Kenya, nigefurahi yule Mhariri wa Nipashe Jumapili aje hapa asome huu uchambuzi na aombe radhi kwa uharo aliotuandikia Jumapili.

for sure.
 
Mod (Invisible), wawekee watu wapige kura za maoni kama watu wana support au kuto support KITENDO CHA WABUNGE WA CHADEMA KUTOKA NJE YA UKUMBI WA BUNGE WAKATI RAIS AKIHUTUBIA. Hapo tutajua mwelekeo wa wana JF
 
Na ulaaniwe mwenyewe na uzao wako. Chadema walipoingia kwenye uchaguzi hawakujua kuwa katiba iliyopo ina mapungufu hayo???? Baada ya kushindwa urais ndipo wanatukosea heshima tuliowatuma bungeni. Kudadadeki, walichemsha wapende, wasipende na wote mnaoshabikia upuuzi huo, ...................... ah, bora ninyamaze tu.

MK CHADEMA walilisema hilo toka mwanzo, kuwa endapo wangepewa ridhaa ya kuiongoza hii nchi, hivyo vingekuwa vipzumbele vyao. Naamini kabisa kama Dr. Slaa angetangazwa kuwa mshindi wa kiti cha urais, basi kwenye hotuba yake ya kufungua bunge angeyagusia yote hayo. Kwahiyo punguza jazba Mzee
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom