Walaaniwe watu wote wanaowaambia vijana wajiajiri bila kuwapa mitaji

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,701
36,119
Wakuu kuna jambo linaniumiza sana.

Jambo lenyewe linaitwa UNAFIKI.

Unafiki kwa nchi za Kiafrika umekuwa mkubwa sana.

Hivi mtu anautoa wapi ujasiri wa kumwambia kijana ajiajiri huku hajampa mtaji?
Alaaniwe!!!

Hakuna kijana mvivu, hakuna kijana mwenye akili timamu anapenda kuwa tegemezi. Ila pale anapokosa ajira au mtaji ndipo ataonekana mzembe.

Binafsi ni mwajiriwa, napata kipato cha wastani cha kuweza kubadili kitoweo tu.

Pia nimejiajiri kwenye biashara ya bodaboda. Nina bodaboda kama 3 hivi vijana wanaleta hesabu per day. Niliwahi kufungua duka likafa kutokana na mtikisiko ule wa kiuchumi 2016/17.

Kilimo nimewahi kugfanya kama misimu miwili ila nako sikupata faida kwakuwa management ilikuwa finyu. Kile kilimo cha kutuma fedha kwa ndugu mikoani.

Hii biashara ya bodaboda iko poa kiasi , sasa napata 24k kwa siku.

Mtaji nilipata kazini(ajira), hakuna aliyenipa mtaji nilipokuwa kwenye kipindi kigumu cha kukosa ajira.

Kama una moyo saidia watu wawili,watatu au hata mmoja apate mtaji ajiajiri. Sio unaandika mitandaoni na kutoa michanganuo ya kiuwendawazimu ya biashara huku hutoi capital huku hujatoa mtaji.
 
Kujiajiri sio jambo jepesi..kwanza yampasa mtu (hapa namzungumzia zaidi kijana) awe na wazo la aina ya ujasiriamali anaotaka kuufanya (iwe biashara au uwekezaji ktk kilimo na ufugaji).

Jambo la pili ajue location na aina ya clients wanaomzunguka na LA Tatu ambalo ni muhimu zaidi ni MTAJI, Hapa ndipo shughuli ilipo!! Vijana wengi wana business ideas kibao ila wanakwama kwa sababu hawana mitaji.

Kumwambia ajiajiri wakati hana mtaji ni kumtia majaribuni na hasirani, bila shaka wengi hughafirika pale waambiwapo "wajiajiri".
 
Kuna ofisi moja niliingia nikakamkuta jamaa, ananiambia yeye ni kinyozi, ko' akanishauri na mie nijiajili. Nikamuuliza kwanini uliacha kunyoa? Anajibu kwa sababu ya ajira.
Hapo ndo nikaelewa shida ya walio shiba ilipo
Huyo hayawani ni mtu mbaya sana. Aliona kuwa kinyozi hakulipi zaidi ya kuajiriwa but wewe anakushauri ukanywe makohozi yake
 
Twende Sawa Sawa Na John Pombe Joseph Magufuli
Atuvushe Kutoka Uchumi Wa Kati Hadi Super Power Nation. Muda Huu Ndiyo Wenyewe 😀😁😅😄😃😃✍✍

Atake Asitake, Katiba Siyo Msahafu Tutaibadili
😐😏🤔🙄😑🤨😶😎😎
By Ally Kesi.
 
Magu na baraza lake zima la mawaziri hakuna hata mmoja kati yao aliyetoka chuo akajiajiri,wote waliajiriwa lkn eti leo wakina Jenista Mhagama wanawaambia vijana wajiajiri wkt yeye mwenyewe alikua ameajiriwa Mwl.,Kigwangala anasema think out of the box wkt yeye mwenyewe aliajiriwa WAMA akabebwa na mama Salma mpk kapata ubunge na kupata mitaji.
 
Jitafakari! Kama uliwezeshwa kupambana au ulipambana mwenyewe..

Usipende kutoa kauli za kukatisha tamaa
sijakatisha tamaa mtu, fikiri nje ya box sio kila siku kulalamika taafuta ufumbuzi,anzia hapo ulipo. kuna vitu vingi vya kufanya mfn mdog dalali wa nyumba ana mtaji wa tsh ngap?...mifano ni mingi mno.
 
Magu na baraza lake zima la mawaziri hakuna hata mmoja kati yao aliyetoka chuo akajiajiri,wote waliajiriwa lkn eti leo wakina Jenista Mhagama wanawaambia vijana wajiajiri wkt yeye mwenyewe alikua ameajiriwa Mwl.,Kigwangala anasema think out of the box wkt yeye mwenyewe aliajiriwa WAMA akabebwa na mama Salma mpk kapata ubunge na kupata mitaji.
Sasa sijui IQ zao ni ndogo au unafiki unawala
 
Back
Top Bottom