Wala simpi pole Maxence, nampongeza sana

falcon mombasa

JF-Expert Member
Mar 5, 2015
9,158
9,239
Najua tofauti na mawazo ya wengi humu mimi ni mkristo mkatoliki tena wa itikadi kali.

Baada ya kukaa na kutafakari kwa siku kadhaa juu ya kilichompata mpendwa wetu maxence nimeamua kubadili msimamo wa kumpa pole hadi kumpongeza Maxence.

Nimeamua kumpongeza Maxence kwa kukubali kuteswa kunyanyaswa kupigwa nk kwa ajili ya wale watanzania maskin,wajinga,wanyonge,yatima,malofa,wagonjwa,vilema,wenye njaa walioko Chato, Biharamulo, Mpanda, Bahi nk.

Kwa kuwa JamiiForums imekuwa mstari wa mbele kufichua uovu dhuluma dhidi ya makundi haya. Hivyo malipo ya kipekee atakayoyapata ni toka kwa roho mtakatifu.

Maxence usikate tamaa mungu hatokuacha kwenye makao yake ya milele yaliyopangwa na yeye mwenye nguvu.

Mimi leo navunja ratiba zote nitakuwa Kisutu nimevaa shati la mikono mirefu na mistari mistari nitakunja mikono ya shati.

Hii ni hatua ya mwanzo ya kila mwenye kutaka kwenda mbinguni lazima aipitie na leo tunashuhudia Maxence akiipitia.

Na kwa kujiamini nasisitiza nitakuja na alteeza.
 
Watanzania waliopo Ngara, Chato, Geita, , Kasulu, Kahama, uvinza, Kibondo, kakonko, bahi , kondoa , manyoni, itigi, Shelui, Igunga, Nzega, Didia lohumbo, ushetu, chambo, mlele, sikonge, Urambo, Tabora, nkwenda, mubira , kaisho, Benako, ushirombo, Bukombe, tukuyu, mwakareli, , Makongorosi, chunya, kyela, chimara, Mbeya, Iringa, Makete, Mafinga, ifunda, Tosa, makambako,
 
Ilula, kilolo, Mbinga, namtumbo, Kitanda, Songea, kitai, litembo, likokola, Tunduru, Nakapanya, nanguruwe, masasi
 
Temeke, kinondoni, ilala , Kibiti, Lindi na kadhalika huko kote watanzania wanauhitaji serikali lazima ipeleke Huduma za msingi huko
 
Ni wajibu wa serikali kuwalinda na kuwahudumia wananchi viongozi waaichukulie kupeleka maendeleo sehemu kama Ni hisani Hapana na wana ccm mjue Baada ya kupigiwa kura, deni lenu kubwa Ni kupeleka maendeleo maeneo hayo kwani kura Ni kibali kimojawapo kinachowaruhusu kukusanya Kodi
 
Lazima serikali, mjenge miundombinu, muulinde Uhuru wa mtanganyika uliopatikana mwaka 1961 kwani mtanganyika alitafuta Uhuru ili aweze kuongea, kutoa maoni yake na kujipangia mambo yake mwenyewe pasipo kuvunja sheria
 
Watanzania waliopo Ngara, Chato, Geita, , Kasulu, Kahama, uvinza, Kibondo, kakonko, bahi , kondoa , manyoni, itigi, Shelui, Igunga, Nzega, Didia lohumbo, ushetu, chambo, mlele, sikonge, Urambo, Tabora, nkwenda, mubira , kaisho, Benako, ushirombo, Bukombe, tukuyu, mwakareli, , Makongorosi, chunya, kyela, chimara, Mbeya, Iringa, Makete, Mafinga, ifunda, Tosa, makambako,
Umepasahau Lusaunga na buseresere
 

Similar Discussions

38 Reactions
Reply
Back
Top Bottom