Wakuu wenzangu Manaojuwa Sheria za Tanzania Nauliza swali langu hili naomba mnijibu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakuu wenzangu Manaojuwa Sheria za Tanzania Nauliza swali langu hili naomba mnijibu

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by MziziMkavu, Sep 20, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Sep 20, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,612
  Likes Received: 4,603
  Trophy Points: 280
  Habari zenu Wakuu wenzangu naomba kuuliza Swali hili je Sheria za Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, kuhusu Mtanzania kuwa na Uraia wa nchi mbili hapo kwetu imepitishwa na Serikali yetu? Na pia ningeomba kama kuna Mtu ana kitabu cha Sheria ya Jamhuri wa Muungano au Katiba ya Serikali ya Tanzania naomba anipatie Naomba hilo swali langu nijibiwe asanteni
   
 2. mayenga

  mayenga JF-Expert Member

  #2
  Sep 20, 2011
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 3,739
  Likes Received: 537
  Trophy Points: 280
  Sheria ya uraia wa nchi mbili bado haijapitishwa.Hata hivyo kwakuiwa tunayo sheria kuhusu uraia(The Citizenship Act),kuna uwezekano isiwepo sheria mpya badala yake ikliyopo itafanyiwa marekebisho.Kuhusu katiba mimi ninayo copy moja,ila kama uko Dar es Salaam,waweza kwenda duka la Serikali lililoko mtaa wa Jamhuri na kujipatia copy yako kwa bei ndogo tu.
   
 3. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #3
  Sep 20, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,612
  Likes Received: 4,603
  Trophy Points: 280
  mimi sipo Dar es-Salaam ndio maana nikataka kujuwa kuhusu hilo suala je wamelipitisha Wabunge? au ndio limewekwa kapuni? Au ndio Tungojee Serikali mpya ya mwaka 2015?
   
 4. NGOGO CHINAVACH

  NGOGO CHINAVACH Verified User

  #4
  Sep 20, 2011
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 797
  Likes Received: 145
  Trophy Points: 60
  hakuna sheria inayoruhusu uraia wa nchi mbili, kuhusu katiba tembelea website ya bunge Parliament of Tanzania.(click hapo kwenye parliamnet)
   
 5. Niezzle

  Niezzle Member

  #5
  Sep 20, 2011
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Sheria kuhusu suala la Mtanzania kuwa na uraia wa nchi mbili bado haijapitishwa....Unaweza ku download katiba ya Tanzania kupitia website ya bunge hakikisha unatafuta na Amendment bill ya constitution
   
 6. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #6
  Sep 21, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,612
  Likes Received: 4,603
  Trophy Points: 280
  Kama ndio hivyo basi bado sisi Wa Tanzania tupo nyuma sana Kimaendeleo tunazidiwa hata na majirani zetu itabidi Serikali ilifikirie kwa upya hili suala la kuumpa Mtanzania nafasi ya kuweza kumiliki Uraia wa nchi mbili kwa wakati mmoja.
   
 7. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #7
  Sep 21, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,612
  Likes Received: 4,603
  Trophy Points: 280
  Serikali inachongojea nini hili suala Bila ya kulipitisha? Au ndio mpaka tungoje tena wakati wa kampeni ya Uchaguzi mkuu mwaka 2015 ndio walizungumzie hili suala ndani ya Kampeni? mbona wamekuwa wazito namna hii hao viongozi wa Serikali?
   
 8. T

  Taso JF-Expert Member

  #8
  Sep 21, 2011
  Joined: Jun 12, 2010
  Messages: 1,648
  Likes Received: 458
  Trophy Points: 180
  Unauliza "mbona serikali wazito namna hii" kana kwamba swala hilo ni cut-and-dry na wote government, parliament and Tanzanians at large tunakubaliana tunataka uraia pacha. Sivyo.

  Kuna mgawanyiko mpana kwenye jamii juu ya swala la kugawa uraia wa Tanzania kwa watu wengine, serikalini pia kuna wide division, kumbuka Wizara ya Mambo ya Ndani na Foreign Affairs walivyotoa misimamo inayosigana mwaka jana.

  For any number of reasons. It is not very clear what benefits will be reaped by mkulima na mfanyakazi wa Tanzania kwa kuleta uraia pacha. Au, critics wamesema, watakaonufaika ni wageni, kama Wahindi na Waarabu na Wakenya, ambao watatumia mwanya huo ku exploit economic privileges za Mtanzania.

  Hoja ya wanaoomba uraia pacha ile iwawezesha kuwekeza "nyumbani" nayo inagonga gonga ukuta, wameulizwa ni kitu gani ambacho huwezi kuwekeza bila uraia? Mchina anawekeza kwenye mikokoteni ya kukusanya chuma chakavu Kariakoo, Mmarekani amewekeza kwenye kuzalisha umeme Ubungo, Mhindi amewekeza kwenye maduka na ufisadi mjini, wewe Mswahili uliyezaliwa Kariakoo ukachukua uraia wa India hapana shaka utaweza kushindana na Wachina na Wahindi kuwekeza "nyumbani" na uraia wako wa India.

  Wanaohoji uraia pacha pia wame question uzalendo wa Watanzania ambao waliutema uraia wa Tanzania walipohamia ughaibuni na sasa wanautaka tena, Rais Kikwete alisema "wanataka kula huku na kule."

  Mwisho wa siku, hata kama kuna faida lukuki, swala la uraia pacha sio priority agenda ya nchi kwa sasa and is not in the conversation. Katika immigration policy na citizenship framework kwa ujumla kuna imperatives nyingine zinazotuumiza vichwa kwa sasa, immigration dynamics za East African integration, national identity cards za Watanzania, na more pressingly, uraia wa Watanzania uchukue sura gani kama katiba mpya ita overhaul Muuungano. Hayo ndio tunayo grapple with on the nationality front, sio uraia pacha.
   
 9. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #9
  Sep 21, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,612
  Likes Received: 4,603
  Trophy Points: 280
  hao uliowataja ( Wahindi na Waarabu na Wakenya, ambao watatumia mwanya huo ku exploit economic privileges za Mtanzania. ) Wapo wangapi hapo kwetu Tanzania? Wanaweza kufika Watu Millioni moja?walishindwa kuharibu Uchumi wa Tanzania baada ya kupata Uhuru mpaka sasa Wataweza kuharibu sasa eti kwa sababu ya kuwa na Uraia wa nchi mbili kwa wakati mmoja? Mkuu

  mbona unazungumza out of point? hao
  Wahindi na Waarabu na Wakenya wapo wengi Nchini Uingereza,Ulaya na Amerika mbona hawawezi kuharibu Uchumi wa hizo Nchi nilizozitaja? Wanachi wa nchi yetu wana wivu sana hao watu weupe na wageni pia kwa sababu sisi wenyewe Wavivu kikazi WaTanzania ni wazembe kikazi na uzalishaji na hatuna Maendeleo yoyote yale. kazi yetu ni uvivu,uzururaji mijini na uzembe wa kazi.

  Kuwapa wananchi haki yao wanayoitaka yaani Uraia wa Nchi mbili hakuto sababisha Kuharibu uchumi wa nchi yetu. Amka Mkuu acha usingizi na ubaguzi wako wa Rangi huo,Nchi yoyote pasipo kuwa na Wageni hakuna maendeleo hapo , angalia Amerika karibu yote ina wageni wengi kuliko nchi yoyote ile ya Duniani je imeanguka kiuchumi kwa sababu ya Wageni? Hebu nijibu hilo swali langu. Kwa Mfano mimi huku nilipo naishi

  Ugenini na Serikali ya hapa nilipo inapata faida kutoka kwangu kila nikinunua kitu kwa mfano Laptop nitalipa Kodi ya Serikali nikinunua TV mpya lazima nilipe ushuru wa Serikali sasa Serikali inafaidika sana na wageni kuliko hao wenyeji Mkuu amka basi.
   
 10. T

  Taso JF-Expert Member

  #10
  Sep 22, 2011
  Joined: Jun 12, 2010
  Messages: 1,648
  Likes Received: 458
  Trophy Points: 180
  Na nyinyi mlioko uhamishoni mnaoomba tuwakubalie uraia pacha, mko wangapi?

  Kama Wahindi na Waarabu na nyinyi mlioko huko mko wachache sana basi hiyo inaturudisha kwenye pointi yangu ya msingi kwamba kwa sasa hatujiumizi vichwa na pendekezo la kubadilisha sera ya nchi kwa ajili ya narrow interests, tuna samaki wakubwa sana wa kukaanga katika maswala ya kitaifa. Hususan kama kigezo cha maombi yenu ya uraia pacha ni kwamba mtaleta faida za "tunalipa kodi na kununua laptop"!

  Kwanza, wewe uliyehamia au kuzamia ughaibuni hutalipa kodi wala kununua laptop Tanzania. Haupo nchini, period. Wahindi na Waarabu wanaoishi Tanzania hawanunui laptop Tanzania, wanatuuzia laptop, tena kilanguzi na hawalipi kodi: wanajibadili majina from Patel Zain to Patel Airtel. Au Albwardy Kempinski to Albwardy ASB Tanzania Limited. Sasa mtatusaidia nini tukiwapa uraia pacha? Halafu kabla hatujaamua kuwakubalia au la, tungependa kujua, haswa haswa mko wangapi huko?

  Faida ya kununua laptop!
   
Loading...