Wakuu wa wilaya wakimbia vituo; PINDA ABAINI ATISHIA KUWATIMUA KAZI

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797

• PINDA ABAINI ATISHIA KUWATIMUA KAZI

Na Walter Mguluchuma, Mpanda

WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda amewaagiza wakuu wa wilaya mpya zote nchini waishi kwenye maeneo ya makao makuu ya wilaya zao vinginevyo atawachukuliwa hatua za kuachishwa kazi.

Agizo hilo alilitoa jana wakati akiwahutubia wananchi kwenye sherehe ya uzinduzi wa mkoa mpya wa Katavi iliyofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Kashaulili.

Pinda alisema wako baadhi ya wakuu wa wilaya mpya ambao toka wachaguliwe wamekuwa wakiishi nje ya wilaya zao.

Alisema wakuu wa wilaya ambao wanaona hawawezi kukaa kwenye wilaya zao ni vizuri wakawapisha watu wengine kwani wapo Watanzania wengi wanazihitaji nafasi hizo.

Waziri Mkuu alifafanua kuwa kitendo cha wakuu wa wilaya mpya kutoishi kwenye maeneo yao kinasababisha washindwe kusimamia ipasavyo maendeleo ya wilaya zao.

"Kama hamuishi kwenye wilaya zenu mnategemea nani atakayesimamia maendeleo ya wilaya zenu?" alihoji.

Aliwataka wakuu wa mikoa kuhakikisha wakuu wa wilaya wote wanaishi kwenye wilaya zao na si vinginevyo.

Pinda aliwaagiza wakuu wa mikoa kutoa taarifa kwake kama kutakuwa na mkuu wa wilaya ambaye anaishi nje ya wilaya yake ili aweze kumchukulia hatua.

Unaona TATIZO la kuchaguana KIURAFIKI bila kuangalia PROFESSION ya MTU na hamu ya kufanya kazi kama MKUU wa WILAYA? Hawataki Kuishi VIJIJINI - WILAYA zisizo na TAA na CLUBING...

Haya Ndio Matatizo yatakotupata na UTAWALA wa KIKWETE kulazimisha VIJANA MARAFIKI wa PRINCE kupewa VYEO
 
Alitegemea nini, kama hata mawaziri hawawi mfano wa kuigwa kuhamia makao makuu ya nchi Dodoma, motivation kwa hawa wakuu wa wilaya, wengi wao ambao waliteuliwa kwa mujibu wa ukaribu na wakubwa waliokataa kwenda dodoma, itakuwa ni ipi hasa; hii ni sawa na kuanika mpunga nje halafu unashangaa kukuta njiwa kwenye mkeka;
 
Mi naona PM hana jipya... Mbona wao hawahamii Dodoma? Kila siku makelele tu na mikwala mingiiiii......
 
Mi naona PM hana jipya... Mbona wao hawahamii Dodoma? Kila siku makelele tu na mikwala mingiiiii......

Badala ya wakubwa kuanza kwa kuhamia makao makuu ya serikali Dodoma wanawakamia wadogo.. Waongoze kwa mifano vinginevyo hawana haki ya kuwaonyeshea vidole wengine..
 
Alitegemea nini, kama hata mawaziri hawawi mfano wa kuigwa kuhamia makao makuu ya nchi Dodoma, motivation kwa hawa wakuu wa wilaya, wengi wao ambao waliteuliwa kwa mujibu wa ukaribu na wakubwa waliokataa kwenda dodoma, itakuwa ni ipi hasa; hii ni sawa na kuanika mpunga nje halafu unashangaa kukuta njiwa kwenye mkeka;

big up' mkuu, umenena. Kwanza yeye na JK wange amia Dodoma, ingekuwa busara yeye kutoa kauli hiyo.
 
Naamini hakuna haja ya kutangaza tishio kama hilo kwani akitaka kuwafahamu wale wote wasioishi kwenye maeneo yao hachukui hata nusu saa, hapo ndipo angetekeleza adhabu anayoitaka. Njia ndefu za kurekebisha mienendo ya watumishi hata pale pasipohitajika si lazima. Naungana pia na wale wanaoshauri kuwa hata wizara nazo ambazo miundo mbinu za kiofisi zimekamilika zionyeshe utiifu wa kuhamia Dodoma
 
Interesting. Ingekuwa vizuri tukifahamu kama wamepewa mahitaji yanayotakiwa kuwepo katika vituo vyao. Vitendea kazi si mashangingi tu, nyumba, mawasiliano, logistics zinazohusiana na kuhamishwa kwa familia zao shule za watoto wao, hostpitali kama wakiumwa na hata mahitaji ya kila siku.

Kama hayo yote PM amewaandalia, basi ni vema tuwalaani wakuu hao wa wilaya, kama hajawaandalia basi kauli ya PM ni blah blah tu.
 
Alitegemea nini, kama hata mawaziri hawawi mfano wa kuigwa kuhamia makao makuu ya nchi Dodoma, motivation kwa hawa wakuu wa wilaya, wengi wao ambao waliteuliwa kwa mujibu wa ukaribu na wakubwa waliokataa kwenda dodoma, itakuwa ni ipi hasa; hii ni sawa na kuanika mpunga nje halafu unashangaa kukuta njiwa kwenye mkeka;

Muheshimiwa hebu nieleweshe hapo kwenye red.
Ofisi kuu za wizara zote zipo Dar au Dodoma?
Kama zipo Dar, wakae Dodoma halafu kazi wafanye Dar?
Mtazamo wangu ni kwamba wangeiandaa Dodoma kuwa makao makuu ki vitendo na sio kinadharia.
 
Angetoa mifano ndio tungemuelewa zaidi,maana kuna wilaya zingine hazina nyumba za wakuu wa wilaya ila wilaya ya jirani nyumba zipo,ambapo sio mbali sana;na hizo ni arrangement za wakuu wa mikoa na tamisemi sisi wananchi hatutakiwi kuona PM analalmikia utaratibu walioupanga wasaidizi wake!!apeleke fungu nyumba zijengwe haraka maana sasa watahamia hotelini na familia nzima.....gharama inarudia pale pale!
 
Na yeye anafanya nini Dar es salaam akahamie Dodoma.... Raisi anaishi Ndege Makamu kwenye Gari na yeye anaishi Dar mawaziri na manaibu wote wanaishi Dar huyu jamaa vipi ananyooshaea watu vidole wakati yeye ana bonge la Boriti jichooni mwake... Pindaaaaaaaaaaaaaaaa.... na wewe ufukuzwe kwanza kazi sababu hujahamia Dodoma....

Hii inatokea Tanzania tu.....
 
Kwani wakuu wa wilaya wana kazi gani? Shughuli zote za maendeleo zinasimamiwa na wakurugenzi wa halmashauri!

kazi yao ni kuingia kwenye vikao vya halmashauri na dcc na kupiga posho,kuwasumbua wakurugenzi wawawekee mafuta kwenye magari wakachukulie vimada
 
pale mafia alikuwepo dc anaitwa manzie mangochie(sasa hivi ni dc geita),huyu gamba alikuwa kila weekend anaenda daslam kucheki mechi taifa na alikuwa anatumia fedha ya serikali,usafiri wa mafia ni wa ndege tu!kwenda na kurudi ni laki mbili na ishirini elfu,per diem laki na sitini..sometimes katikati ya wiki alikuwa anaenda dar kwa ishu zake binafsi,.yani hichi kijamaa kilikuwa kero kuu kwa wahasibu,jeuri yake ni sababu yeye na mama salma wana undugu..that's JK regime
 
Jamni hayo ni maneno tu, niliwahi pita wila mpya kama mbili hivi, makao makuu ya wilaya kuna ofisi tu, wafanyakazi waote wanaishi mjini, sasa kwanini DC ndio akae huko?

• PINDA ABAINI ATISHIA KUWATIMUA KAZI

Na Walter Mguluchuma, Mpanda

WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda amewaagiza wakuu wa wilaya mpya zote nchini waishi kwenye maeneo ya makao makuu ya wilaya zao vinginevyo atawachukuliwa hatua za kuachishwa kazi.

Agizo hilo alilitoa jana wakati akiwahutubia wananchi kwenye sherehe ya uzinduzi wa mkoa mpya wa Katavi iliyofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Kashaulili.

Pinda alisema wako baadhi ya wakuu wa wilaya mpya ambao toka wachaguliwe wamekuwa wakiishi nje ya wilaya zao.

Alisema wakuu wa wilaya ambao wanaona hawawezi kukaa kwenye wilaya zao ni vizuri wakawapisha watu wengine kwani wapo Watanzania wengi wanazihitaji nafasi hizo.

Waziri Mkuu alifafanua kuwa kitendo cha wakuu wa wilaya mpya kutoishi kwenye maeneo yao kinasababisha washindwe kusimamia ipasavyo maendeleo ya wilaya zao.

"Kama hamuishi kwenye wilaya zenu mnategemea nani atakayesimamia maendeleo ya wilaya zenu?" alihoji.

Aliwataka wakuu wa mikoa kuhakikisha wakuu wa wilaya wote wanaishi kwenye wilaya zao na si vinginevyo.

Pinda aliwaagiza wakuu wa mikoa kutoa taarifa kwake kama kutakuwa na mkuu wa wilaya ambaye anaishi nje ya wilaya yake ili aweze kumchukulia hatua.

sizipendi kauli zake, zimejaa kulalamika kamavile hajiamini. toa amri kuanzia sasa mkuu wa wilaya anayeishi nje ya kituo chake cha kazi ifikapo, siku fulani ajue hana kazi . wala hatutamjulisha tutateuwa mwingine, wakuu wote wa wilaya watoe taarifa wapi? wanaishi kwa ufuatiliaji.[ktk nchi makini jamaa wa usalama wa taifa, utawapenda, ] unajua kama mkuu wa wilaya haishi wilayani kwake , basi ujue viongozi wote wa wilaya baada ya saa za kazi wanatimka na kuacha wilaya wazi.
 
Back
Top Bottom