nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,862
- 5,797
| ||
|
| ||
|
Mi naona PM hana jipya... Mbona wao hawahamii Dodoma? Kila siku makelele tu na mikwala mingiiiii......Unaona TATIZO la kuchaguana KIURAFIKI bila kuangalia PROFESSION ya MTU na hamu ya kufanya kazi kama MKUU wa WILAYA? Hawataki Kuishi VIJIJINI - WILAYA zisizo na TAA na CLUBING...
Haya Ndio Matatizo yatakotupata na UTAWALA wa KIKWETE kulazimisha VIJANA MARAFIKI wa PRINCE kupewa VYEO
Mi naona PM hana jipya... Mbona wao hawahamii Dodoma? Kila siku makelele tu na mikwala mingiiiii......
Alitegemea nini, kama hata mawaziri hawawi mfano wa kuigwa kuhamia makao makuu ya nchi Dodoma, motivation kwa hawa wakuu wa wilaya, wengi wao ambao waliteuliwa kwa mujibu wa ukaribu na wakubwa waliokataa kwenda dodoma, itakuwa ni ipi hasa; hii ni sawa na kuanika mpunga nje halafu unashangaa kukuta njiwa kwenye mkeka;
Alitegemea nini, kama hata mawaziri hawawi mfano wa kuigwa kuhamia makao makuu ya nchi Dodoma, motivation kwa hawa wakuu wa wilaya, wengi wao ambao waliteuliwa kwa mujibu wa ukaribu na wakubwa waliokataa kwenda dodoma, itakuwa ni ipi hasa; hii ni sawa na kuanika mpunga nje halafu unashangaa kukuta njiwa kwenye mkeka;
Kwani wakuu wa wilaya wana kazi gani? Shughuli zote za maendeleo zinasimamiwa na wakurugenzi wa halmashauri!
• PINDA ABAINI ATISHIA KUWATIMUA KAZI
Na Walter Mguluchuma, Mpanda
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda amewaagiza wakuu wa wilaya mpya zote nchini waishi kwenye maeneo ya makao makuu ya wilaya zao vinginevyo atawachukuliwa hatua za kuachishwa kazi.
Agizo hilo alilitoa jana wakati akiwahutubia wananchi kwenye sherehe ya uzinduzi wa mkoa mpya wa Katavi iliyofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Kashaulili.
Pinda alisema wako baadhi ya wakuu wa wilaya mpya ambao toka wachaguliwe wamekuwa wakiishi nje ya wilaya zao.
Alisema wakuu wa wilaya ambao wanaona hawawezi kukaa kwenye wilaya zao ni vizuri wakawapisha watu wengine kwani wapo Watanzania wengi wanazihitaji nafasi hizo.
Waziri Mkuu alifafanua kuwa kitendo cha wakuu wa wilaya mpya kutoishi kwenye maeneo yao kinasababisha washindwe kusimamia ipasavyo maendeleo ya wilaya zao.
"Kama hamuishi kwenye wilaya zenu mnategemea nani atakayesimamia maendeleo ya wilaya zenu?" alihoji.
Aliwataka wakuu wa mikoa kuhakikisha wakuu wa wilaya wote wanaishi kwenye wilaya zao na si vinginevyo.
Pinda aliwaagiza wakuu wa mikoa kutoa taarifa kwake kama kutakuwa na mkuu wa wilaya ambaye anaishi nje ya wilaya yake ili aweze kumchukulia hatua.