Wakuu wa Wilaya kwenye Katiba mpya tuwaondoe! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakuu wa Wilaya kwenye Katiba mpya tuwaondoe!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Firigisi, Feb 15, 2012.

 1. F

  Firigisi Member

  #1
  Feb 15, 2012
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 91
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 15
  Tunaweza kuondoa wakuu wa wilaya,nchi nzima bila kuathiri shughuli za maendeleo.Watendaji waliopo wanaweza kutimiza wajibu wao bila matatizo yeyote na hawa jamaa kimsingi hamna kazi yeyote wanayofanya ya maana kutu.
  Kwanini napendekeza kwenye katiba mpya tuwaondoe.

  1.Kupunguza gharama zisizo za lazima kwenye ma VX na majumba ya kifahari ya hawa jamaa,misharara minono na kuelekeza
  hilo fungu kwenye maendelea ya sehemu husika kama maji ,nishati ,masoko bora,mikopo kwa wafanya biashara wadogo wadogo nk
  Ni mzigo kwa serikali yetu

  2.Wanasababisha migogoro kwenye maeneo husika baina ya serikali na wananchi wa maeneo yao

  3.Uteuzi wao hauna utaratibu maalumu(criteria) isipokuwa mpaka ''mkuu wa nchi anapopendezwa'' na mtu flani hii inaleta bias
  na malalamiko ya upendeleo wa vyeo na kupeana fadhila.

  4.Wameshindwa kusimamia miradi ya maendelea na kushindwa kudhibiti rushwa ,ubadhirifu wa mali za umma

  5.Wanafanya kazi za chama kimoja kwenye nchi ya vyama vingi

  6.Kuna mgongani wa kimajukumu na kuingilia kazi za wakurugenzi

  Nawasilisha
   
Loading...