Wakuu wa vituo vya Polisi waitwa Mahakamani kueleza sababu za kukaa na mshtakiwa mahabusu kwa siku 14

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
09508230122bbe53bbd158623aaaf233

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewataka wakuu wa kituo cha polisi Kijitonyama na Oysterbay kufika mahakamani hapo leo Ijumaa Oktoba 25, 2019 kueleza sababu za kukaa na mtuhumiwa kwa siku 14 badala ya kumpeleka gereza la Segerea.

Mtuhumiwa huyo, Elizabeth Balali alifikishwa mahakamani hapo Oktoba 10, 2019 akikabiliwa na mashtaka ya kujipatia Sh25 milioni kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji fedha.

Elizabeth anayedaiwa kuwa msimamizi wa mali za mke wa gavana wa zamani wa Benki Kuu Tanzania (BoT), marehemu Daudi Balali, siku hiyo alisomewa mashtaka na wakili Wankyo Simon mbele ya hakimu mfawidhi, Kelvin Mhina.

Jana Alhamisi Oktoba 24, 2019 mshtakiwa huyo alifikishwa katika mahakama hiyo akitokea kituo cha polisi Kijitonyama, na Mhina ambaye alisikiliza kesi hiyo mara ya kwanza kuagiza arejeshwe kituoni na kutaka wakuu wa vituo hivyo kufika mahakamani kesho kujieleza.

“Nataka kesho waje wajieleza kwa nini wamekaa na mshtakiwa kwa siku 14 katika vituo vya polisi badala ya kumpeleka Segerea kama mahakama ilivyoagiza,” amesema Mhina.

Akimsomea mashtaka Oktoba 20, 2019 wakili wa Serikali Wankyo Simon alidai kati ya Oktoba 19 na Desemba 21, 2017 jijini Dar es Salaam, mshtakiwa alijipatia Sh25 milioni kwa ulaghai kutoka kwa Dk Roderick Kisenge kwa kumuuzia eneo la mita 900 ambalo halijapimwa lililopo Boko Dovya wilayani Kinondoni wakati akijua si lake.

Katika shtaka la utakatishaji fedha, Wankyo alidai katika kipindi hicho mshtakiwa alipokea Sh25 milioni kutoka kwa Dk Kisenge kupitia akaunti yake iliyopo Benki ya CRDB wakati akijua fedha hizo ni zao la kosa la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, Elizabeth hakuruhusiwa kuongea chochote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza makosa ya uhujumu uchumi.

Hakimu Mhina katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 109/2019 alimueleza mshtakiwa huyo kuwa licha ya mahakama kutokuwa na uwezo wa kuisikiliza, pia shtaka la utakatishaji wa fedha halina dhamana.

Siku hiyo ilielezwa mahakamani hapo kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na kuahirishwa hadi leo ambapo imebainika kuwa alikuwa katika vituo hivyo badala ya Segerea.

======
CHANZO: Mwananchi
 
Zomboko,
Unataka nini hapa na hii kipande ya gazeti?
Police ni dola hawakosi majibu na wakalindwa.
Sec 5 Cap 16 of the Penal Code inasema Afisa wa Police afanyapo upelelezi wa kesi apewe muda na asiingiliwe.
Watakapokuambia wako katika upelelezi ndio sababu walimhold huyo mama utawaambiaje?
 
Mahakama wanajua,ila wanataka jibu rasmi ili sheria ionekane imefuatwa.
 
Hii maana ya utakatishaji fedha nafikiri Serikali haijaisoma na kuielewa vizuri.

Utakatishaji fedha ni uuzaji wa mali au upokeaji wa fedha iliyo chafu na kuibadilisha matumizi ili kukwepa kosa ililozaliwa nayo hiyo fedha. Sasa kwa hii kesi ya huyu Elizabeth, sijui ni vipi hiyo milioni 25 kutoka kwa Dk. Kisenge kuonekana kuwa ni hela chafu. Kusema kuwa ni zao la ulaghai, maana yake lingeweza kuhesabika kama kosa la utakatishaji fedha ikiwa Elizabeth angezihamisha kwa mtu mwingine baada ya yeye kuzipokea kutoka kwa Kisenge. Kama hivi sasa zikiitwa pesa chafu maana yake hata Dk. Kisenge anatakiwa kuwa mshtakiwa kwa kuwa ndiye aliyetuma fedha chafu.

Nafikiri hapa Upande wa mashtaka wamejielekeza vibaya katika kufungua hiyo kesi na kutumia vibaya neno utakatishaji. Hii kesi haifai kuitwa kesi ya uhujumu uchumi.
 
Sheria za mtaani sasa sheria iliyoweka limit ya masaa 24 haina maana
Zomboko,
Unataka nini hapa na hii kipande ya gazeti?
Police ni dola hawakosi majibu na wakalindwa.
Sec 5 Cap 16 of the Penal Code inasema Afisa wa Police afanyapo upelelezi wa kesi apewe muda na asiingiliwe.
Watakapokuambia wako katika upelelezi ndio sababu walimhold huyo mama utawaambiaje?
 
Sheria za mtaani sasa sheria iliyoweka limit ya masaa 24 haina maana
Unaambiwa Sheria ni shimo refu lisilokuwa na mwisho.
Sheria ya mtaani unaijuwa wewe na ya Saa 24 unajua kuitaja tu.
Nikueleze, saa 24 kimaandishi ndani ya IR/RB wanapoivunja Sheria hiyo kwa kukutoa Lock up wanakutembeza nje wanakurudisha na kukregister upya dai hiyo Sheria kama utawatia hatiani.
Kwanza Sheria iliopo ni 48 hours 24 hours ni Sheria yako ya mtaani.
 
Huyu mama atashinda kwa kishindo. Sheria ituambie, kutakatisha pesa ni Nini?
Halafu huyu mama amefanya Nini?
Kutakatisha pesa ni kujipatia pesa kwa njia isiyokuwa ya halali na kujaribu kuipoteza njia hiyo au hizo kwa kuisambaza pesa hiyo katika taasisi za kifedha au watu kwa nia ya kuihalalisha.
Tutamfunga.
 
Mtamfunga labda kwa kosa la kwanza,la kujipatia mali kwa njia ya udanganyifu, napo hapo lazima muwe na hukumu ya Mahakama inayomtaja mmiliki halali kuwa sio Elizabeth..hilo la utakatishaji fedha hakuna hakimu atayekubali kuaibika kwa kumtia hatiani na kosa hilo lilibandikwa isivyo sahihi, halafu baadaye hukumu yake ibagazwe na jaji wa mahakama kuu na hata majaji wa rufaa
 
Ongea vitu usivyojua na wasiojua wenzako.
Sheria ni taaluma tena ngumu. Hivyo usiivamie kutoka hukumu za mtaani, nimekupa muhtasari wa utakatishaji pesa usome kwa umakini na uelewa.
Jana watu watatu wameshtakiwa kwa kupatikana na tausi 3 wa ikulu, pesa 300,000/= waliouza mmoja wametakatishwa nayo.
Shule kijana kama ulikwepa rudi!
 
Acha kusoma soma bila kuelewa. Hiyo tafsiri uliyoiweka kuhusu utakatishaji unaona inaingia kwa huyo mshtakiwa wa habari hii? Baada ya kupokea ameihamisha kokote ili kuisafisha na kuihalalisha?

Hao unaosema waiba tausi, wangekamatwa wakiwa hawajawauza wangeshtakiwa kwa utakatishaji?
 
Nasoma soma bila kuelewa, wewe unaesoma na kuelewa subiri matokeo. Utapatata majibu yako wange....au wasinge.....
 
Back
Top Bottom