Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki (EAC) wafanya kikao kujadili Corona. Rais Magufuli na Nkurunziza hawakushiriki

Wamekubaliana kuhamasisha raia wa nchi wanachama kuchapa kazi, hasa kilimo na uzalishaji wa bidhaa za kujikinga na Covid. Ni kitu ambacho huku bongo kilishawekewa msisitizo. Hapo wamezuga tu kwenye ubadilishanaji wa taarifa za ugonjwa. Wanataka tu kum prove wrong JPM ajifeel alichemka, wakati wao pia ndio wanafatia njia yake.

Hichi ni kipimo madhubuti kwa jiwe, sasa hapa ndio anatakiwa awe jiwe kweli kweli la sivyo akilegeza tu bhas tumepoteza pambano. Watatuchukulia poa sana mipakani, Tukaze hadi wapige magoti.
uzuri huu mwamba wa magharibi huwa nauaminia sana.
 
Acha kutisha watu hapa Raisi siyo malaika lazima atukanwe inapobidi
Rais siyo malaika, lakini amekaa kumwakilisha Mungu. Sasa Mungu mwenyewe anapotukanwa, huwa hamwachi mtukanaji(labda aombe msamaha), kwanini Rais akitukanwa, mtukanaji aachwe?
 
Vikao vya jumuia ya Africa mashariki vimeendelea leo kwa njia ya video agenda kubwa ikiwa ni COVID 19,kwenye kikao wamekwepo Paul Kagame ,Museveni ,Kenyatta na Rais wa Sudan kusini ,ambao hakwepo ni Rais wa Tanzania na Burundi.
Screenshot_20200512-154209_Twitter.jpeg
 
Tukana unavyoweza, ila kitendo cha kumtukana Rais wa nchi ni uzwazwa wa hali ya juu. Kumtukana Rais na kumuona hafai, inamaanisha unatutukana waTanzania wote.
Hakuna aliyetunakanwa labda kaambiwa ukweli....kutukana watz wote ndio nini mkuu. Kuiba aibe mmoja maovu afanye mmoja alafu wasingiziwe watz wote acha ubandidu
 
Wengine wapo kwao na mambo yao tusubil tuone tutakapo fika na aina hii ya mtu asie shaulika akikosea anatafuta mtu wa kumbebesha lawama ogopa sana mtu ni kiongozi afu ana kauli ya kusema kila kitu

"mimi nimesema"
 
Je, huo mkutano ni dawa ya Corona?
Njia za kujikinga na Corona zinaeleweka, sasa wao wamekaa kujadili nini kipya?
Hapo wamemwogopa JEMBE yeye huwa hapendi kupoteza muda kujadili masuala ambayo tayari yanaeleweka.
Huko Duniani wamekaa vikao wee lakini njia za kujikinga na Corona zinabaki ni zile zile.
 
Kuna baadhi ya nchi katika hicho kikao zinategemea bandari yetu(ni wateja) so kama tunahitaji mapato ni bora tukahudhuria tukaongea na wateja wetu..Hoja inajibiwa kwa hoja sio kwa kujificha au kutoroka. Kama ishu ni lugha kwenye kikao kuna mashine za kutafsiri pia kuna ubaya gani akienda kukuza kiswahili kama alivyo fanya S.A ,Malawi n.k.
 
Sasa unamfananisha Mungu na Magufuli kweli wewe nimzima.
Wapi nimemtaja Magufuli? Mimi namtaja Rais, na kama unamaanisha Rais Dr John Pombe Magufuli, sijamfananisha na Mungu, bali nimemtaja mamlaka aliyonayo kuwa yametoka kwa Mungu, hivyo yeyote anayemdharau mpakwa mafuta wa Mungu, sharti apate joto.
 
Hakuna aliyetunakanwa labda kaambiwa ukweli....kutukana watz wote ndio nini mkuu. Kuiba aibe mmoja maovu afanye mmoja alafu wasingiziwe watz wote acha ubandidu
Ukweli wa kipumbavu. Yaani uambiwe ukweli na vijamaa nyuma ya keyboard uufuate, uachane na ushauri wa wataalamu waliokuzunguka?
 
Wapi nimemtaja Magufuli? Mimi namtaja Rais, na kama unamaanisha Rais Dr John Pombe Magufuli, sijamfananisha na Mungu, bali nimemtaja mamlaka aliyonayo kuwa yametoka kwa Mungu, hivyo yeyote anayemdharau mpakwa mafuta wa Mungu, sharti apate joto.

Mungu awezi kumtuma shetani kuwa mwakilishi wake , mtu anayefurahia kupigwa risasi kwa my lissu labda kama katumwa na Mungu wa chato.
 
Tukana unavyoweza, ila kitendo cha kumtukana Rais wa nchi ni uzwazwa wa hali ya juu. Kumtukana Rais na kumuona hafai, inamaanisha unatutukana waTanzania wote.
Ipo hivi kama ulimchagua umetukanwa kama hujamchagua haujatukanwa ...........................Hivyo sio watanzania wote
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom