Raisi hawazi kuweka maendeleo kwa kuchagua wakuu wa mkoa ambao wanahama kila siku na wengi wao hawajui mazingara ya mkoa wanaoongoza. Kikubwa na kibaya zaidi ni kwamba kama mkuu wa mkoa akifanya kazi nzuri anahamishwa kwenye mkoa mkubwa na wenye maendeleo zaidi na wale wabaya au ambao hawana uzoefu wanapewa mikoa yenye hali ngumu zaidi kiuchumi. Wakuu wa mikoa wengi kwenye mikoa midogo wanapiga kampeni kucha za kuhamishwa hii ni kutokana na hali ya sasa kwamba hawa wakuu wa mkoa hawachaguliwi na si wenyeji wa mikoa wanayoongioza. Mimi ningependa wakuu wa mikoa wachaguliwe kila miaka minne na wananchi wa mkoa. Hii itafanya kwanza wapiganie maendeleo ya mikoa yao na pili inaleta serikali ya watu iwe imara. Raisi wa Tanzania anateua watu wengi na serikali ni kubwa sana kwasabu wafanyakazi wengi wanafanya kazi za serikali maisha yao yote. Kama tukileta kura tutapunguza hawa wafanyakazi kufikiri kwamba kazi yao ni ya kudumu. Kwasabu hatuna ma Gavana kama nchi nyingine basi tuchague wakuu wa mkoa na wakuu wa wilaya.