Ngamanya Kitangalala
JF-Expert Member
- Sep 24, 2012
- 501
- 1,214
Nimejaribu kuangalia sheria na kanuni kadhaa kuhusu hili swala la KUSTAAFU kwa wakuu wa mikoa.
Nimesoma sheria ya utumishi wa umma ya mwaka 2002 (The Public Service Act,2002) pamoja na mabadiliko yake.
Pia nimesoma kanuni za utumishi wa umma za mwaka 2003 (The Public Service Regulations, 2003).
Pia nimesoma sheria ya tawala za mikoa ya mwaka 1997 (The Regional Administration Act,1997).
Mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya ni afisa wa umma (Public officer) anayeteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hawa ni wateule wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini hawana MUDA MAALUMU kisheria wa kustaafu utumishi wa umma, mwenye mamlaka ya LINI na WAKATI GANI watastaafu utumishi wao wa umma, ni Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Hivyo basi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, yeye ndio mwenye MAMLAKA ya kuamua ni LINI na WAKATI GANI mkuu wa mkoa au mkuu wa wilaya anastaafu utumishi wa umma bila kuzingatia umri wao.
Lakini Katbu mkuu kiongozi (Chief Secretary) , Katibu mkuu wa wizara (Permanent Secretary), Naibu latibu mkuu wa wizara( Deputy Permanent Secretary), Katibu tawala wa mkoa(Regional Administrative Secretary), katibu wa bunge (Cleck to the National Assembly), Wakurugenzi wa halmashauri nk, hawa wana muda rasmi wa KUSTAAFU UTUMISHI WA UMMA kwa mujibu wa sheria ya utumishi wa umma ni miaka 60, japo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayo mamlaka ya kisheria kuwaongezea muda wa utumishi endapo akiona kuna ulazima wa kufanya hiyo.
Hivyo basi wakuu wetu wa mikoa wamestaafu utumishi wa umma kwa mujibu wa mamlaka ya uteuzi wao (Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania)