Jabman
JF-Expert Member
- Jul 27, 2016
- 1,005
- 1,335
Natafakari jambo la busara la wakuu wetu wa mikoa kuzuia wakulima kuuza mazao yao nnje ya mikoa yao. Je wanajua kuwa ni kwanini wanauza nje ya mikoa yao? Je wakulima wanapotafuta soko zuri nje ya mikoa yao ni dhambi? Je mfanyakazi akipata mshahara wake na azuiliwe kuupeka nje ya mkoa wake? Maana mshahara Wa mkulima ni mazao yake.
Naiomba serikali sikivu badala ya kuzuia mkulima kuuza mazao yake iyanunue hayo mazao kwa bei nzuri. Hebu fikiria kama kila mkoa utazuia mazao yake yasitoke , mikoa ambayo kila mwaka in njaa tupu si wataendelea kula viwavi? Basi mzuie pia mazao kuingia mikoani kwenu.
Najua serikali ina nia nzuri ila approach hii si nzuri. Hivi mtendaji wa kijiji naye akizuia itakuwaje?