Wakuu wa Mikoa na Wilaya ziwe ceremonial posts

GALLABA

Member
Dec 19, 2016
63
119
Kutokana na kauli ya waziri kairuki kwamba mkuu wa mkoa au wilaya awe anajua kusoma na kuandika tu, napenda kushauri ziwe ni ceremonial posts yaani kazi ya kukata utepe tu na kuhudhuria sherehe na matamasha, lakini sio

1.Kufanya maamuzi mazito ndani ya halmashauri mf.Mh.Gambo na madiwani Arusha, kuamuru watendaji wawekwe ndani mf Mh.Paul Makonda,

2.Kuwa ndio mwenyekiti kamati ya ulinzi na kujipa madaraka makubwa dhidi ya Rpc mfano.makonda alipotangaza wauza unga

3.Kulipwa posho na mshahara mkubwa, na hata wasitengewe bajeti kabisa. kwasababu ni non fuctional kutokuwepo kwao hakutafanya kazi ziende , wawe kama mameya,

4.kutoingilia maamuzi yoyote dhidi ya baraza la madiwani,halmashauri zaidi ya kushauri tu

Kwasababu siku zote akili ndogo haiwezi kutawala akili kubwa,

1.RPC -professionally ni polisi, mwenye uzoefu na mafunzo ya usalama wa raia na mali zao, kwanini mtu mwenye elimu ya darasa la saba amtawale huyu. anatakiwa aripoti kwa IGP,
Mh.Adadi Rajabu aliwahi kunena wanasiasa wanaharibu ushahidi

2.Wakurugenzi wa Halmashauri/Majiji-hawa ni wazoefu na wenye elimu ya kutosha kwanini mtu wa darasa la saba amtawale huyu

3.Watendaji wa serikali, kundi hili kuna wanasheria,madaktari, wahasibu kwanini mkuu wa mkoa,wilaya awe juu yao wakati wamemzidi elimu, hivi mwanasheria akifoji mkataba inakuwaje, mhasibu akifoji malipo inakuwaje, mkaguzi akiandika ripoti tofuati inakuwaje,
darasa la saba atajua, wakati anahitajika mtu msomi zaidi yao au mwenye uzoefu kuwatawala

Ushauri tu,
 
Ajue kusoma na kuandika hii ni dharau kubwa sana ina maana kipind kile mh aliposema anafanya upembuz wa hawa watu alikua anangalia anaejua kusoma na kuandika vizur au ni vip?
 
Katiba yetu ni mbaya kama si mnafiki huwezi kupinga jambo hili. WaTz tukubali kufia tunachokiamini labda watatuelewa
 
Nakumbuka maneno ya mwenez wa sasa wa CCM,HP,kuwa cheo cha DC et al hakina tija. Leo ndo nimemuelewa alimaanisha nini!
 
Ajue kusoma na kuandika hii ni dharau kubwa sana ina maana kipind kile mh aliposema anafanya upembuz wa hawa watu alikua anangalia anaejua kusoma na kuandika vizur au ni vip?
Ina maana.ukisoma awali a.k.a chekechea ukajua.KKK basi usihangaike kuendelea kujiumiza inatosha kuwa Rais,waziri,mbunge,mkuu wa mkoa /wilaya,diwani.
 
Mimi sina tatizo hata kama ni darasa la saba, tatizo langu ni RC mwenye cheti feki ambapo ni kosa la jinai, je anaruhusiwa kufoji?
Kwa hiyo rais anataka hao vilaza anao wazid elimu yeye ndo na wao watuongoze sisi yaan ana piga auto pilot hii nchi kweli me nashauri hta urais tuwe tunachagua ma handsome na beautifuls tu ndo nchi itasonga
 
"Hiki ni kijiko unachokiona, baada ya kula kwa mkono...
neno linaloponya, lilokosa mdomo...
na huu ni bonge la ujumbe kwenu, kwangu kama somo...
HILI NDO WAZO LA AWAMU..."
 
Hii nchi imekuwa ya ajabu sana,nadhani hata DAB pia anoana kabisa kuwa analindwa kwa katiba kuvunjwa. Shame on You! Ila ajue kuwa sio wote tuliopo ikifika 2020/2025 tutakuwa tumekufa, wapo watu watamnyoosha tu tena vizuri sana. Ikiwezekana na jela wataeleweka.
 
Back
Top Bottom