Wakuu wa mikoa na Wilaya shikeni hili


M

mgeni wenu

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2012
Messages
3,669
Likes
619
Points
280
M

mgeni wenu

JF-Expert Member
Joined Jan 2, 2012
3,669 619 280
Tangu serikali ya awamu ya Tano kuingia madarakani kumekuwa na Teuzi mbali mbali amabazo kila mtu amekuja na tafsiri zake kwa kadri anavyoona.

Wapo wanaoamini ni kupanga safu,wapo wanaoamini ni kuimarisha utendaji,na wengine wanaamishwa ni visasi.

Wengi waliotenguliwa nafasi zao yawezekana kabisa kabisa hawakuwa wamejiandaa kuachia nafasi zao,au tayari kwa maisha mengine ambapo kumejaa kutoridhika kabisa na kutenguliwa kwao.

Nimepitia michango kuhusu Teuzi na Tenguzi kwa muda mrefu naona kama hii ya Magesa Mulongo ni kama watu wanashangilia,sio kwamba Magesa alikuwa hafanyi kazi vizuri,la hasha alitimiza sana wajibu wake,isipokuwa kauli zake kwwa wananchi wengi wanaochangia hazikuwa nzzuri maskioni mwao.

Kwa kuwa midomo inaumba wengi walidiriki kutaka aondolewe kwenye nafasi yake...na baada ya kuondolewa wengi wanapongeza tenguzi kuliko hata Teuzi.

Niwaombe sana walio teuliwa waangalie sana matendo na ndimi zao katika utendaji kazi wao maanakikilio chako kitakuwa kicheko kwa wenzako hapo baadae.

Wekeza katika maelewano mazuri na wananchi,tumia buasara katika utekelezaji wa sheria za nchi,jali haki.Za binaadamu katika kuutekeleza majukumu yako najua mna hamu ya kufanya sana kazi wekeni akiba ya maneno na hifadhi ya vitendo Mungu awatangulie katika wajibu wenu mpya.

Karibuni Tanga (mgosi Mgeni wenu)
 
M

mgeni wenu

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2012
Messages
3,669
Likes
619
Points
280
M

mgeni wenu

JF-Expert Member
Joined Jan 2, 2012
3,669 619 280
Mkitumbuliwa na mkazomewa msije sema hamjaambiwa,maana mkuu hasomeki
 

Forum statistics

Threads 1,236,374
Members 475,106
Posts 29,255,701