Wakuu wa mabenki inafaa wafikishwe mahakamani kwa uhaini!

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
35,034
28,201
Kitendo cha wakuu wa mabenki kujaribu kupotosha umma na kuutishia umma kuwa serikali imeongeza gharama katika kufanya mihamala ya fedha ni kitendo cha UHAINI

Mabenki na wazalendo wote walielewa vizuri kusudi la serikali kuchukua kodi kwenye makato ya ATM na yanayofanania vizuri sana lakini wakuu wa mabenki wamejiorganise na kuamua kupotosha umma kwa makusudi lengo lao ikiwa ni kuichafua serikali ya Magufuli...
Nikiwa kama mzalendo ninawiwa kuitaka serikali ichukue hatua kali sana dhidi ya hawa wakuu wa mabenki walioamua kupotosha au kuhujumu nchi.

Mpaka ninavyoowasilisha hoja hii hakuna benki yoyote iliyotuma ujumbe kwa wananchi kama walivyotuma jana juu ya ufafanuzi wa TRA.

Tangazo lililotolewa jana na mabenki haya lingeweza kumpindua Rais Magufuli kwa kuwa lilikuwa no Tangazo hatari na linalotengeneza ugomvi mkubwa wa wananchi dhidi ya serikali.

Kinachoniuma zaidi ni matangazo yaliyotoka kwenye mabenki ambayo ni taasisi za umma mfano NMB!!!!!

WAKUU HAWA WA MABENKI HASWA YALE YA UMMA ni lazima wawajibishwe ikiwa ni pamoja na kukamatwa na kuhojiwa juu ya malengo yao.
 
Hivi jana wananchi wenye akiba zao banki ambazo mabenki wanazitengenezea faida wangeaamua kuzitoa zote mabenki yangekuaje leo?
 
ujinga ni janga! hata serikali icheze kiduku gani, hiyo kodi atalipa mwananchi tu. btw hongera kwa kuanzisha mada!
Hata mabenki yafanye figisu yoyote Jamhuri ina mikono mipana ya kuyashughulikia.kwa mfano serikali ina uwezo wa kuweka regulation kwamba standard charge ya kutoa fedha kupitia ATM isizidi 500 VAT inclusive
 
M
ujinga ni janga! hata serikali icheze kiduku gani, hiyo kodi atalipa mwananchi tu. btw hongera kwa kuanzisha mada!
Mabenki ndiyo yanayocheza kiduku kwa sababu serikali ina uwezo wa kutoa miongozo!
 
hakuna kitu kama hicho. biashara ya benki sio mafuta au sukari.
Hakuna kitu kama hicho sasa lakini kinaweza kuwepo kuanzia sasa kupitia BOT...msijidai mnajua kuliko serikali
 
NmB ni benki au taasisi ya umma...serikali ina mandate ya kusema kuwa mishahara yote ipitie hazina na kuwanyang'anya mwanya wa kuneemeka na mihamala ya kifedha...
 
Benki zikileta marosoroso na serikali ina uwezo wa kufyatuka .....!
 
Mkono wa serikali ni mrefu kuliko unavyoweza kufikiria...huwezi kupambana na serikali kamwe!
 
NmB ni benki au taasisi ya umma...serikali ina mandate ya kusema kuwa mishahara yote ipitie hazina na kuwanyang'anya mwanya wa kuneemeka na mihamala ya kifedha...

serikali haiwezi kutoa maelekezo kwa nmb, banki ina wenyewe. serikali ana hisa tu kama yule mwananchi aliyenunua dse. angalia safu ya uongozi. serikali kama mwanahisa inaweza kutoa pendekezo na likapingwa na majority, that's plc! endelea kuota!
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom