Wakuu wa mabenki inafaa wafikishwe mahakamani kwa uhaini!

Kwi kwi kwi!!hii ni statement ya BOT
Kwani statement maana yake ni Nini? Huo ndio ukweli wenyewe. Bank huwa wanalipa corporate tax ambayo ni kama sikosei 30% ya faida wanayoipata. Sasa itakuwaje walipe 18% VAT. Wao kazi Yao itakuwa kukusanya kama wakala wa serikali. So sie ndio tunatakiwa kulipa tu haina ujanja.
 
We mjinga hiyo 1000 Ni service charge and if serikali imehitaji VAT basi ndo hyo bank walopandisha ili buku Yao ibaki palepale cas VAT haiwahusu huwa inamuhusu mteja WA mwisho anaetumia huduma... Walipokuwa wanaongea wachumi mkawaona sio wazalendo haya sasa hayo ndo nlikuw mnataka na mkatwe Tu zaidi
 
Kitendo cha wakuu wa mabenki kujaribu kupotosha umma na kuutishia umma kuwa serikali imeongeza gharama katika kufanya mihamala ya fedha ni kitendo cha UHAINI

Mabenki na wazalendo wote walielewa vizuri kusudi la serikali kuchukua kodi kwenye makato ya ATM na yanayofanania vizuri sana lakini wakuu wa mabenki wamejiorganise na kuamua kupotosha umma kwa makusudi lengo lao ikiwa ni kuichafua serikali ya Magufuli...
Nikiwa kama mzalendo ninawiwa kuitaka serikali ichukue hatua kali sana dhidi ya hawa wakuu wa mabenki walioamua kupotosha au kuhujumu nchi.

Mpaka ninavyoowasilisha hoja hii hakuna benki yoyote iliyotuma ujumbe kwa wananchi kama walivyotuma jana juu ya ufafanuzi wa TRA.

Tangazo lililotolewa jana na mabenki haya lingeweza kumpindua Rais Magufuli kwa kuwa lilikuwa no Tangazo hatari na linalotengeneza ugomvi mkubwa wa wananchi dhidi ya serikali.

Kinachoniuma zaidi ni matangazo yaliyotoka kwenye mabenki ambayo ni taasisi za umma mfano NMB!!!!!

WAKUU HAWA WA MABENKI HASWA YALE YA UMMA ni lazima wawajibishwe ikiwa ni pamoja na kukamatwa na kuhojiwa juu ya malengo yao.
Kweli wee jinga lao,muwadanganye akina lusinde hao hao,wenye akili kama akina benno ndulu washasema acha lopolopo utaja olewa halafu ukahojiwe na zamaradi kwenye (take1)
 
TRA hawajui maana ya VAT...hiyo ni kodi inalipwa na mlaji benk ni wakusanyaji tuu...kama wasomi hawajui maana ya VAT wanajua nini sasa...
 
Jadili hoja sii mtoa hoja
Wewe hujui mambo tulia ueleweshwe. Hoja inayotoka kwa mtoa hoja bomu inaangaliwa kwa umakini isije ikawa bomu kama mtoaji wake. hata mahakamani katika mahakama ambazo huendesha kesi kikweli-kweli, shahidi akishamaliza kutoa ushahidi wake, cross-examination huanza kwa kumdiscredit shahidi mwenyewe kwanza. hata wakili anayemleta shahidi anaanza kwa kujenga credibility ya shahidi wake. Kwa hiyo wewe kama ni jingalao, lazima watu waanze kwanza kuangalia kama hoja uliyoleta inaakisi sifa ya jina lako...yaani "kubwa la majinga=jingalao"...(si mimi ninayekuita hivyo, ni wewe mwenyewe umejiita jina hilo..usijelalama kwamba nimekutukana)
 
Hawa TRA wanaelewa ila wanatufanya watu wote kama hatujaenda shule, kuelewa hii kitu huitaji kuwa na diploma, always, mwisho Wa siku VAT anaelipa ni final consumer, ndio scenario ya indirect tax, Kwa hivyo mabank yapo sawa. To the bank will be double taxation which is not allowed.
 
Kwa akili yako ya special diploma unaweza kuona jambo hili lilikuwa dogo
Subiri uone hatua zitakazochukuliwa na wenye akili ndio utajua ulienda mbali sana kulinganisha na uhaini(pengine kwa uelewa wako mdogo)!Napinga mabank kuongeza tozo ila sikubaliani na mihemko kama yako!
Una hoja,ijenge bila jazba na utaeleweka!
 
Kitendo cha wakuu wa mabenki kujaribu kupotosha umma na kuutishia umma kuwa serikali imeongeza gharama katika kufanya mihamala ya fedha ni kitendo cha UHAINI

Mabenki na wazalendo wote walielewa vizuri kusudi la serikali kuchukua kodi kwenye makato ya ATM na yanayofanania vizuri sana lakini wakuu wa mabenki wamejiorganise na kuamua kupotosha umma kwa makusudi lengo lao ikiwa ni kuichafua serikali ya Magufuli...
Nikiwa kama mzalendo ninawiwa kuitaka serikali ichukue hatua kali sana dhidi ya hawa wakuu wa mabenki walioamua kupotosha au kuhujumu nchi.

Mpaka ninavyoowasilisha hoja hii hakuna benki yoyote iliyotuma ujumbe kwa wananchi kama walivyotuma jana juu ya ufafanuzi wa TRA.

Tangazo lililotolewa jana na mabenki haya lingeweza kumpindua Rais Magufuli kwa kuwa lilikuwa no Tangazo hatari na linalotengeneza ugomvi mkubwa wa wananchi dhidi ya serikali.

Kinachoniuma zaidi ni matangazo yaliyotoka kwenye mabenki ambayo ni taasisi za umma mfano NMB!!!!!

WAKUU HAWA WA MABENKI HASWA YALE YA UMMA ni lazima wawajibishwe ikiwa ni pamoja na kukamatwa na kuhojiwa juu ya malengo yao.
Komredi kwa hili tusubiri kwanza kwani kunamchanganyano. Mabenki yapo sawa na TRA wamejichanganya kutoa taarifa yao. Ukiisema VAT hii ni kodo anatozwa mlaji. Kodi ya mapato anatozwa mtoa huduma. Hivyo basi Mfano benki inauza huduma ya kutoa pesa bila VAT ni tsh 900. Hii tsh 900 huwa benki inailipia kodi ya mapato kati ya 30%. Sasa serikali imemuomba mtoa huduma huyu amtoze mlaji 18% pale anapotumia huduma husika. Mtoa huduma hawezi kuongeza kwenye 30% nakuwa 48% Kwani hii haimuhusu yeye bali inamuhusu mlaji. Kama inamuhusu mlaji kitakachofanyika ni 18/100x900+900=1062. Hivyo ili serikali ipate VAT kutoka kwa mlaji kwa hii bidhaa ya kutoa pesa, inabidi iuzwe tsh 1052. Huu ndio ukweli ingawa ni mchungu.
Kama kila huduma na bidhaa hulipwa kodi ya VAT na wananchi tunahitaji maendeleo wacha tulipe kodi. TRA wamechemka kwa tamko lao wao ndio waziombe radhi hizi taasisi za fedha. Huu ndio uungwana kwani tunajua lengo lake ni kuwapenda wananchi inaowahudumia. Pia naamini watakuwa wakali kuhakikisha tozo hii inakuwa na tija. Hata kama wasipoomba radhi hadharani wawaandikie barua ya kuwaelewa kusudio lao.
 
Back
Top Bottom