Elections 2010 Wakuu wa JF, tunaweza kupeana matoke ya uchaguzi huu kisayansi?

Dark City

JF-Expert Member
Oct 18, 2008
16,253
11,598
Nimefuatilia thread ya matokeo ya uchaguzi wa kura za maoni ndani ya CCM, nikagundua kama alivyodokeza ndugu Kasheshe kuwa uletaji wa matokeo hauko user friendly. Hii ni kwenye uchaguzi ndani ya Vyama, kwa hiyo ikifika Oct 31 watu watapata shida kupata matokeo. Kwa kuwa vyama na wadau wenye jukumu hilo wameshindwa au hawaoni umuhimu wa kufanya kitu kama hicho, je JF inaweza kuchukua kazi hiyo kwa maslahi ya Watanzania? Yaani kuanzisha kitu kama database ambayo itaonesha wagombea kwa kila jimbo na kwa kila chama kitakachosimamisha mgombea. Na mwishowe kunakuwa na matokeo ya mwisho. Hapa ina maana member yeyote mwenye matokeo kamili (ya jumla) ama anabadika mwenyewe au anatuma kwa wataalamu wanayabandika. Naamini hii itasaidia wafuatiliaji kupunguza upotevu wa muda.

Naomba kuwasilisha!:clap2::clap2:
 
Back
Top Bottom