Wakuu wa forodha wa Utaliana wanasema watu kama 40 bado wametoweka, baada ya meli ya abiria iliyobeb | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakuu wa forodha wa Utaliana wanasema watu kama 40 bado wametoweka, baada ya meli ya abiria iliyobeb

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Shine, Jan 15, 2012.

 1. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #1
  Jan 15, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Shughuli za uokozi zimeendelea kutwa, huku wazamia mbizi wakipekua upande uliozama wa meli hiyo, Costa Concordia.
  Msemaji wa walinzi wa pwani alieleza inawezekana kuwa watu wengine bado wako ndani ya meli.
  Abiria wawili kutoka Ufaransa na baharia mmoja kutoka Peru wanajulikana kuwa wamekufa.
  Mkuu wa kampuni inayomiliki meli hiyo, Gianni Onorato, alisema ushahidi wa awali unaonesha kuwa meli iligonga mwamba;
  nahodha haraka akafuata utaratibu wa kuwatoa abiria melini.
  Lakini operesheni ilizuwilika kwa sababu meli yenyewe haraka ilipindukia ubavuni na kuzusha mtafaruku.
  Taarifa za karibuni zinaeleza kuwa ofisi ya mashtaka ilimzuwia nahodha baada ya kumhoji.

  120114140339_italy_ship_304x171_reuters_nocredit.jpg
   
Loading...