Wakuu, njoo tujielimishe kuhusu hisa za Vodacom

Habari za Siku ya Leo wapendwa

Nimejitokeza Leo kuomba kuelekezwa kuhusu masuala ya Faida ya kununua Hisa

Napenda kutanguliza shukrani za dhati kwenu,


Huenda kuna Faida ambayo inaweza kusaidia Baadae ndo maana Mh. LOWASSA KATIKA SERA ZAKE ALITANGULIZA ELIMU ELIMU ELIMU BURE


KARIBUNI
 
Kila baada ya mwaka mmoja means report ya fedha ya mwaka hutoka ambayo huonyesha kama kampuni imetengeneza faida,makampuni mengine mwaka wao wa fedha uanza January to December wengine kama serikali june up to may
Sasa kama faida unapata baada ya mwaka si bora upeleke hizo hela vikoba?
 
Nawashukur sana Vodacom kwa kutuletea suala la uwekezaji wa hisa inalipa na nimeshanunua vipande vyangu kazaa nasubiri kupanda kwa kipande tu nifanye yangu.
 
Asante lakini kwanini vile vibinti vya pale Mliman city havitoi ushirikiano mpaka tunawaza kuna chezo, unamuuliza mtu maswali muhimu anakwambia kasome Prospectas, wangapi wanajua uelewa wa lugha ya biashara?
Anyway nitajaribu kupata kadhaa nione matokeo yake
HAWAJUI WENGIWAO,NILIMUULIZA MTTU KITU AKANIAMBIA YEYE KAAMBIWA MAMBO YA KUTUAMBIA NA KUTUSHAWISHI,NNJE YA HAPO HAJUI KITU KUHUSU HISA
 
Nawashukur sana Vodacom kwa kutuletea suala la uwekezaji wa hisa inalipa na nimeshanunua vipande vyangu kazaa nasubiri kupanda kwa kipande tu nifanye yangu.
hakikisha vinapanda zaidi ya 4% lasivyo vinaweza kupanda ukapata hasara bila kujua. chapili sio unanunua hisa tu angalia je hio fedha yako ukuweka kwenye biashara yako au ukinunua hisa ipi itakuwa na manufaa.

HISA KUSEMA KWELI KWA UPANA NI MOJA YA NJIA KUBWA KWA WAMILIKI WA KAMPUNI KUPATA MITAJI TU.USIE NA MALENGO MAKUBWA YA KUNUNUA CONTROLING INTEREST BASI ACHANA NA HII KITU ,WEKEZA KWENYE BIASHARA YAKO ZAIDI. IKIKUWA NDIO EXTRA UWEKEZE HUKO
LAZIMA UANGALIE COST VS BENEFIT
 
9771c4b2ed146e52355b74011abe6d01.jpg

Hisa za Vodacom zipo vipi?

Wengi miongoni mwetu tumekuwa tukitaka kujua kuhusu HISA za Vodacom na hii imenifanya nitupie jicho niwape ubuyu kidogo juu ya hisa hizi kwa faida ya wengi.

Kwa tafsiri rahisi HISA NI UMILIKI.
Hii inaamanisha kampuni ya Voda imetoa nafasi ya umiliki kwa wateja watakaonunua hisa za awali.

Mtu akisema nina hisa Vodacom anamaanisha anamiliki Vodacom. Umiliki huu unajionyesha wazi na bayana wakati wa kufanya maamuzi na kugawana gawio (faida inayopatikana katika kampuni). Mwenye hisa nyingi huwa na sauti au ushawishi mkubwa katika kufanya maamuzi na hupewa gawio kubwa kwa uwiano wa hisa zake lakini hakuna upendelo unatokana na upendeleo ya Idadi ya hisa unazomiliki.

Mfano Kama unamiliki hisa 100 za Vodacom Tanzania zitakufanya uwe na haki ya kuwa na kura 100 ktk Mkutano Mkuu wa Mwaka.

Kampuni ya Vodacom asilimia 65 ya hisa zinamilikiwa na Vodacom Group na asilimia 17.5 zinamilikiwa na Mirambo Limited kwa hiyo hii 25% ya hisa zilizowekwa kwenye ofa ni makubaliano Kati ya kampuni ya Vodacom na Mirambo kutoa idadi ya hisa 560Milioni sawa na hizo asilimia 25 Mwenye kuweza kununua hisa milioni 230 atakuwa amenunua hisa nyingi zaidi kuliko yeyote na anakuwa na nguvu ya maamuzi katika vikao na gawio atapata kubwa kwa sababu ndie aliechangia mtaji mkubwa.

Faida za kuwa na Hisa za Vodacom:

1. Unapata fursa ya kuwa mmoja ya wajumbe wa bodi ya wakurugenzi ama moja kwa moja au kwa kuwakilishwa.

2. Mwanahisa anapofariki shughuli za kampuni haziwezi kuyumba kwa sababu jukumu la kazi za kila siku lipo mikononi mwa menejimenti najua kuna watu wanahofia Hisa zangu ndiyo zimefika mwisho hapana suala la uendeshaji lipo mikononi mwa Menejimenti.

3. Ni rahisi zaidi kuuza HISA pindi unapoona hauhitaji kuendelea na umiliki na ukitaka kuziuza tafuta kipindi ambacho bei ipo juu ili ufaidike bei ya Ofa inaweza kuwa ndogo kulinganisha na ile ya kuingia kwenye soko pale bei inakuwa juu muda wa ofa Kama huu ndiyo mzuri kununua Hisa.

4. HISA ni dhamana (badala ya kuweka nyumba/shamba ili uweze kukopeshwa na taasisi za fedha waweza kuweka dhamana ya hisa zako).

5. Kampuni inapofanya vizuri sokoni ama kwa kutoa huduma/bidhaa bora au kwa kuwa na mipango mkakati mizuri thamani ya HISA hupanda. Unaweza kununua Leo kwa 850 then bei ikapanda hadi 2000.

Kwa maana hiyo mbali ya gawio mtu anaweza kuuza hisa kwa bei inayomlipa akilinganisha na bei ya kununulia.

Ni wakati wa kuchangamkia Fursa hii asee ofa imebaki muda mfupi kufungwa.
 
Wakuu naomba kufahamu..
Kwa ninavojua mimi kwakua Vodacom imetoa umiliki wa 25% za hisa kwa wanahisa wake, basi 25% ya ile faida wanayoipata Vodacom (Net Profit) ndio itakayo gawanywa kwa walionunua hisa, kila mmoja kwa asilimia yake....

Sasa naskia wanasema Vodacom itagawa 50% percent ya faida kwa wanahisa wake
wakati ilimilikisha kampuni kwa 25%, cjaelewa hapo
 
Kiwango cha chini cha idadi ya hisa ni 100, kiwango cha faida kitategemea na faida ya kampuni mara baada ya kuondoa tax.
tutajua kama kampuni imepata faida au hasara je watatushurikisha katika kufunga hesabu za mwaka kujua kama imepata faida au hasara
 
Naona kama bei ipo juu. Kama mtu ananunua ili aziweke mda mrefu ni investment nzuri sana. Ila mafisi kama Mimi wanaotaka kuzifanyisha biashara na kuziuza hapo bei itakapo panda basi tutasubiria kama mwaka mzima au zaidi
 
tutajua kama kampuni imepata faida au hasara je watatushurikisha katika kufunga hesabu za mwaka kujua kama imepata faida au hasara
Kila kampuni ambayo inauza hisa lazima itoe financial statements zake kila mwaka na huwa wanatoa kila robo mwaka.
 
nimefuatilia michango ya watu mbali mbali ktk hii mada na nimegundua hisa kwasasa sio kitu cha kuaminika ni sawa na kucheza kamali.

na kama mm hapa ambaye ni mwananchi wa kawaida pesa yangu nimeitafuta kwa shida kwanini nikaichezee kamali kiujumla nitakuwa nimeikosea nidhamu pesa yangu.

ila wanaotaka kucheza kamali na hisa waache wacheze. sisi wengine hata kama tutakufa maskini sio mbaya.
 
Hii biashara ya hisa sina hamu nayo kabisaaaaa nilinunua hisa bank ya crdb hisa moja ilikuwa inasimamia tshs 350 kwasasa imeanguka mpaka tshs 185/=nilipiga hesabu ya kuuza nikajikuta nitapata hasara km ya 5,800,000/=
binafsi naona kama hisa za hizi benki zetu wala hazfanyi vizuri nakushauri kama hiza zako zitapanda mpaka angalau 450 basis ziuze na uende kampuni nyingine kama vile swiss port.tbl n.k.
 
Hii biashara ya hisa sina hamu nayo kabisaaaaa nilinunua hisa bank ya crdb hisa moja ilikuwa inasimamia tshs 350 kwasasa imeanguka mpaka tshs 185/=nilipiga hesabu ya kuuza nikajikuta nitapata hasara km ya 5,800,000/=
binafsi naona kama hisa za hizi benki zetu wala hazfanyi vizuri nakushauri kama hiza zako zitapanda mpaka angalau 450 basis ziuze na uende kampuni nyingine kama vile swiss port.tbl n.k.
 
Back
Top Bottom