Wakuu, njoo tujielimishe kuhusu hisa za Vodacom

Nimeona kuwa wawekezaji wa nje wataruhusiwa kununua hizi hisa kwa kupitia mlango wa nyuma fulani. Hizi brokerage firm za TZ zitanunua hisa kisha wawekezaji wa nje watanunua fungu la hizo hisa.

Hii kidogo inapoteza point nzima ya kupitishwa hii sheria ya kuwalazimisha kuuza hisa maana ilikuwa ni kuwapa watanzania chance ya kufaidika na hizi kampuni.

Lakini kwa upande mwengine inapunguza risk ya hisa hizi kudoda kutokana na kukosa wanunuzi wa ndani.
 
Usidanganye watu mwaka Jana faida ilishuka sio kwa sababu ya market share still Vodacom ndio leading kila eneo kuanzia uuzaji wa data service,mpesa mpaka muda wa maongezi na Wateja wengi,kilichopunguza faida ni gaovement policy kulikua na introduction ya kodi mbalimbali katika HUDUMA wanazotoza makampuni ya Simu kutoka kwa serikali na TCRA mfano utaona hata sasa ukiweka vocha utaona serikali inachukua asilimia 18 kabla ya hapo hiyo asilimia 18 ilikua inabaki kwa makampuni ya Simu na hivyo kutengeneza super profit miaka ya nyuma
Kama umetumwa na vods sawa. Maana nimesoma prospector zenu. Na mmepata mapungufu ya mauzo graph yenu inashuka. Wapo wengi hawajui kuzisoma wanaona nambananba tu. NIMESOMA NA MAUZO YENU YANASHUKA
 
Yaani Halotel ulinganishe na Vodacom??kwa lipi??we jamaa bhana sijui hata kama unauelewa kidogo na mambo ya financial security, Vodacom still ndio leading company kuanzia kwenye uuzaji wa data ,Wateja,HUDUMA za mpesa pia HUDUMA za uuzaji muda wa mazungumzo yaani Halotel hii ndio unasema ni kampuni inakua??kampuni ambayo hata haijawai kurudisha fedha walizowekeza ulinganishe na Vodacom??in which aspect ambayo Halotel wanaizidi Vodacom??
Sijasema HALOTEL WANAINGIZA FAIDA KULIKO VODA. nimesema HALOTEL FAIDA YAO INAPANDA KILA MWAKA. WEWE UMETUMWA NA VODA NINI ???
WAACHE WANNUE WATU VODA ILA WATANIKUMBUKA.
 
Baadhi ya watu wanapata tatizo kuelewa maana ya 'hisa'. Mada hii inachanganua. Tuanze na mfano rahisi wa biashara. Tuchukue mfano wa mradi daladala, tuuite, JF Trans, kwa madhumuni ya hoja hii.

Tuchukulie tunataka kununua minibus inayogharimu shilingi milioni hamsini, Sh 50,000,000/= Tuchukulie "hesabu" ya "tajiri" ni shilingi laki moja (100,000/=) kila siku.

Picha ya kwanza:
Mtu mmoja akifanya maamuzi magumu na kununua gari hiyo, atatoa shilingi milioni hamsini zote yeye peke yake. Na "mpunga" wa hesabu atauchukua peke yake kila siku.

Picha ya pili:
Wakiwa watu wawili waliowekeza milioni ishirini na tano kila mmoja kwenye kununua basi, kila mmoja atakuwa na umiliki nusu wa basi hili.
Swali 1.: mpunga wa "hesabu" kila siku kila mmoja atachukua kiasi gani? ___________.(Hinti: nusu bin nusu).

Picha ya hisa:
Tuchukulie kwamba yupo mtu mzoefu kuendesha madaladala. Lakini kutokana na 'ukapa' akawa hana nguvu za kununua gari hilo peke yake. Labda ameweza kukusanya mtaji wa shilingi milioni kumi tu. Kwa hiyo, lengo la kupata milioni hamsini limetimia kwa asilimia 20 tu. Ili kupata milioni arobaini zilizobaki anaamua kuuza asilimia 80 ya umiliki wa gari hilo, yaani shilingi milioni arobaini.

Kwa kujua hali ngumu iliyopo, akaamua 'kuvunja' hiyo milioni hamsini ya basi iwe vipande elfu kumi vilivyo sawa. 50,000,000 / 10,000 = 5,000.
Swali 2: Kwa vile yeye tayari ashaweka milioni kumi kwenye JF Trans, je anamiliki vipande vingapi?________ (Hinti: milioni kumi gawa kwa sh elfu tano).

Vipande vilivyobaki bila mmiliki ni 8,000. Kila kipande (hisa) sh 5,000. Thamani Jumla Milioni arobaini.

Hapo sasa inatolewa ofa kwa jamii. Tuseme hisa moja inatolewa ofa ya awali kwa umma (Initial Public Offer, IPO) ya kuuzwa sh 7,000. Jumla ya hisa ni 8,000. Kiasi cha chini kununua ni hisa kumi. Yaani Sh 70,000. Ukinunua zaidi, unaweza kuongezea hisa tano tano (elfu 35).

Swali 3. Mategemeo ya makusanyo yatakuwa shingi ngapi? _________ (Hinti: idadi ya hisa zinazouzwa x bei ya hisa.) Tuchukulie hisa zote elfu kumi zimepata wanunuzi.

Jamaa anakuwa mkononi na mtaji wa shilingi milioni 66. Ikiwa tuko wote mpaka hapa, mambo safi. Vinginevyo, fanya homework ;) hiyo hapo juu vizuri.

Jamaa anachukua milioni hamsini ananunua basi. Milioni kumi na sita anatia mfukoni kama faida / gharama za kuanzia biashara.

Swali 4: Biashara ikianza, kila siku mwenye hisa anachukua shilingi ngapi kwa kila hisa? _________________

Swali 5: Itachukua siku ngapi gawio la hesabu kurudisha gharama ya hisa? ______

Swali 6: Aliyeanzisha mradi (20% hisa) atakuwa anachukua shilingi ngapi kila siku?_______

Swali 7: Hisa hizi zingeuzwa kweli, ungenunua ngapi? :D ____________

Mfano huu umerahisishwa kupunguza 'variables'. Halafu miye si mtaalamu niliyesajiliwa wa hisa :(

Update 1: Soko la Hisa
Baada ya muda, ile ofa ya awali yenye bei moja itafikia mwisho. Baada ya hapo, hisa zitakubaliwa kuuzwa kwenye soko la hisa, ili kuwapa fursa wasiokuwa nazo kuzipata, na walionazo kuziuza.

Kwa mfano wetu, tuchukulie mtu aliyenunua hisa 100 za awali kwa bei ya shilingi 5,000 hisa moja. Akiamua kuziuza hawezi kuzipeleka sokoni kwingine, bali kwenye soko la hisa. Hapo mawakala wataanza kuzinadi, tuseme, kwa bei hiyohiyo ya sh 5,000. Wateja AMA watazigombea AU watazikacha. Wakizigombea, bei itapanda, kwa vile zinauzwa kwa mnada. Wakizikacha, bei itashuka.

Ukiwa unamiliki hisa za JF Trans, na taarifa ya habari saa mbilli usiku imefikia mahali inasema, sasa tunawaletea mauzo yalivyokuwa kwenye soko la hisa leo hii, hutabadili chaneli kwa vile kwako wewe taarifa ishaisha, bali utasikiliza vizuri ili ujue uwekezaji wako unaendaje. Bei ikipanda, mfano toka sh 5,000 kwa hisa, na kuwa sh 6,000, ukiuza hisa zako 100 utakuwa umepata faida ya sh (100 x 1000) 100,000.

Ila bei ikishuka, na kuwa sh 4,000 hisa ulizo nazo zitakuwa zimeshuka thamani, na ungeziuza kwa siku hiyo ungepata hasara ya sh 100,000 kutoka kwa bei uliyonunulia.

===

Pamoja.
 
tatizo ukinunua hisa unaambiwa wewe ni mmiliki lakini cha ajabu huna sauti kwenye kampuni ....wenye sauti ni board of directors
 
Mfanio sio mbaya ila kwenye hisa daladala inaweza ikaingiza faida lakini wenye hisa msipewe kitu, badala yake ikatumika kununua mabasi mengine au kufungu TV kwenye basi.
 
tatizo ukinunua hisa unaambiwa wewe ni mmiliki lakini cha ajabu huna sauti kwenye kampuni ....wenye sauti ni board of directors
bodi ya wakurugenzi aghalabu huundwa kutokana na idadi ya hisa. Baadhi ya makampuni wenye hisa chachechache hupewa fursa ya kupata mwakilishi wao mmoja. Nguvu nyingine uliyonayo kama mwanahisa ni kupata fursa ya kupiga kura na kuhudhuria mkutano mkuu.
 
Mfano wako ni mzuri sana mkuu, Hiyo ni understanding za mwanzo kabisa za hisa, Biashara ya Hisa sio Biashara nyepesi hivyo...Iko complicated kimtindo ndo maana hata Vodacom wanakuambia mtafute mshauri wako wa Fedha
 
Mfanio sio mbaya ila kwenye hisa daladala inaweza ikaingiza faida lakini wenye hisa msipewe kitu, badala yake ikatumika kununua mabasi mengine au kufungu TV kwenye basi.
Hii ni moja ya zile 'variables' zilizorahisishwa kwenye mfano wa hapo juu. Bodi ya Wakurugenzi / Mkutano mkuu wa wanahisa wanaweza kuamua kuwekeza upya faida kwenye biashara ili kukuza mtaji. Wengine huamua kugawa sehemu iwe gawio, na sehemu iwe uwekezaji tena (re-investment).

Kadhalika biashara inaweza kutengeneza hasara, na hivyo pasiwe na gawio kwa wenye hisa.
 
Mfano wako ni mzuri sana mkuu, Hiyo ni understanding za mwanzo kabisa za hisa, Biashara ya Hisa sio Biashara nyepesi hivyo...Iko complicated kimtindo ndo maana hata Vodacom wanakuambia mtafute mshauri wako wa Fedha
Asante sana. Hakika ushauri wa kitaalam unahusu.
 
Back
Top Bottom