Wakuu, njoo tujielimishe kuhusu hisa za Vodacom

Quoted "
CDS au "Central Depository System" ni mfumo wa kompyuta unaotomiwa na CDSC kuweka akaunti za hisa kwa njia ya kielectroniki. Akaunti hizi huwa zimefunguliwa na wamiliki hisa kwa hivyo, mara kwa mara, CDS hutumika kubadilisha hisa kutoka akaunti moja hadi nyingine wakati hisa zinaponunuliwa na kuuzwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam.

Hivyo basi, kila mmiliki hisa katika kampuni zilizosajiliwa katika DSE ni lazima awe na akaunti ya CDS illi kuweza kushiriki katika kununua na kuuza hisa."
Kwa mfano nimenunua hisa za 85,000.baada ya kugawana naweza kupata hata 500,000 ikiwa tumepata faida?
 
Huwezi kadiria, hiyo ni biashara unawekeza Vodacom hivyo gawio lako litategemea wa(m)mepata faida kiasi gani, juzi kuna benk moja wanahisa wamepata gawio la shilingi tano:mad::mad:
kweli bahati nasibu mkuu.ndo maana wanajishtukia wana kwambia uwe na mshauri was masuala ya kifedha.usije ukawashika mashati.
 
Mi naomba kufahamishwa.

1;Gawio la faida ligawanywa kila baada ya muda gani.

2;Hasara inapotokea (kulingana na idadi ya hisa ulizonunua) inamaana pesa yako inaweza ikaliwa mpk ukakosa umiliki kwamba account yako ikasoma sifuri?.
Mwisho kama ndo nataka kuuza hisa zangu kwa bei ya faida...unaruhusiwa kuuza zote ama chache jinsi upendavyo ww mmliki?

Na kama unataka kununua zaidi inakubidi ununue kwa mwana hisa mwenzio au la?

#Naendelea_kujifunza
 
Je ni sahihi kufanya uwekezaji wa hisa katika kipnd kigumu cha uchumi kama hiki
Au wizi tu maana watanzania tunapenda kuibiwa
 
Kuna suala najiuliza ambalo liko kiimani kidogo,hivi naponunua hisa za voda inamaana nananua hisa za voda inamaana nanunua umiliki wa voda kama cellular netwek pekee ama kampuni ya vodacom nzima pamoja na huduma zake kama m pesa na m bet?
 
Faida ya voda inashuka kila mwaka sana sana mwaka juzi iliporomoka sana kutokana na halotel kuingia kazini, na Airtel Money na Tigopesa kuwa na huduma sawa na za voda.
Kampuni ya Mtandao inayoingiza faida kila nwaka kwa kukua ni Halotel Pekeake.

Hizo nyingne huwezi tabiri kama zitapata mauzo.

Alafu pia ukicheki kua serikali inelazimisha kampuni za mitandao wauze shares zao.

Sio kua Voda walihitaji mtaji. Hapana.
Usidanganye watu mwaka Jana faida ilishuka sio kwa sababu ya market share still Vodacom ndio leading kila eneo kuanzia uuzaji wa data service,mpesa mpaka muda wa maongezi na Wateja wengi,kilichopunguza faida ni gaovement policy kulikua na introduction ya kodi mbalimbali katika HUDUMA wanazotoza makampuni ya Simu kutoka kwa serikali na TCRA mfano utaona hata sasa ukiweka vocha utaona serikali inachukua asilimia 18 kabla ya hapo hiyo asilimia 18 ilikua inabaki kwa makampuni ya Simu na hivyo kutengeneza super profit miaka ya nyuma
 
Dividend policy ya Vodacom ni kutoa asilimia 50 ya faida kama gawiwo kwa wanahisa....sote tunajua faida inapatikana baada ya kua tumetoa gharama zote za uendeshaji na Kodi, mfano Vodacom wakitengeneza faida ya bilioni 40 maana yake bilioni ishirini zitagawiwa kwa wanahisa kama dividend kulingana na uwekezaji wako uliofanya yaani hisa....kama mnataka maelezo zaidi mnaweza kupata Vodacom IPO Prospectur IPO mtandaoni unaweza kuidownload ama utaipata DSE na ofisi za Vodacom
 
Faida ya voda inashuka kila mwaka sana sana mwaka juzi iliporomoka sana kutokana na halotel kuingia kazini, na Airtel Money na Tigopesa kuwa na huduma sawa na za voda.
Kampuni ya Mtandao inayoingiza faida kila nwaka kwa kukua ni Halotel Pekeake.

Hizo nyingne huwezi tabiri kama zitapata mauzo.

Alafu pia ukicheki kua serikali inelazimisha kampuni za mitandao wauze shares zao.

Sio kua Voda walihitaji mtaji. Hapana.
Yaani Halotel ulinganishe na Vodacom??kwa lipi??we jamaa bhana sijui hata kama unauelewa kidogo na mambo ya financial security, Vodacom still ndio leading company kuanzia kwenye uuzaji wa data ,Wateja,HUDUMA za mpesa pia HUDUMA za uuzaji muda wa mazungumzo yaani Halotel hii ndio unasema ni kampuni inakua??kampuni ambayo hata haijawai kurudisha fedha walizowekeza ulinganishe na Vodacom??in which aspect ambayo Halotel wanaizidi Vodacom??
 
Du haya mambo ni kwa watu wenye hela jamn apo unaweza kuta ukinunua izo hisa mia laki nane na nusu faida ni 5000 kwa mwaka kama biashara za mabenki fixed account na wengine hela kubwa ndo upata faida inayoonekana
 
Faida hutolewa baada ya muda gani
Kila baada ya mwaka mmoja means report ya fedha ya mwaka hutoka ambayo huonyesha kama kampuni imetengeneza faida,makampuni mengine mwaka wao wa fedha uanza January to December wengine kama serikali june up to may
 
NI uchambuzi mzuri. Hata hivyo haujadadavua zaidi juu ya
1: Mchakato mzima wa kununua his ulivo
2: Huaujaeleza changamoto za soko la hisa haswa katika mazingira tuliyonayo kwa sasa hapa nchini.
 
Kuna suala najiuliza ambalo liko kiimani kidogo,hivi naponunua hisa za voda inamaana nananua hisa za voda inamaana nanunua umiliki wa voda kama cellular netwek pekee ama kampuni ya vodacom nzima pamoja na huduma zake kama m pesa na m bet?

Unanunua hisa kwenye Vodacom kama kampuni inayoendesha huduma zote ulizozitaja.Nakushauri upitie prospectus yao iliyo tolewa kwenye mtandao.
 
Unanunua hisa kwenye Vodacom kama kampuni inayoendesha huduma zote ulizozitaja.Nakushauri upitie prospectus yao iliyo tolewa kwenye mtandao.
Kama ni hivyo hii dili hainuhusu,ni haramu kwangu kushiriki kwa namna yoyote ile kwenye kamari ama kuwekeza kwayo.
 
Hisa mil560 ?? Nani ana mamlaka ya kuweka idadi ya hisa zinazouzwa mfano voda wakisema wanauza hisa mil 8000 = bil8 kwa sh850 kila hisa huo utakuwa ufisadi kwa pesa za wananchi nisawa mm niwe na biashara ya genge niuze hisa mil 4 kila hisa sh 500 ??? Mm namashaka sana na biashara ya hisa kama siyo ufisadi wa kimataifa na kuzidi kuyanufaisha makampuni kwa kuwanyonya wananchi
Mkuu hii statement ako ina maana gan?
 
Ipi ni njia nzuri kulingana na hali ya uchumi tuliyonayo kati ya kununua hisa na kufungua fixed account?
 
Back
Top Bottom