Wakuu, nimekuta mil 300 kwenye Bank account yangu - sizijui!

FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
31,617
37,815
Naomba ushauri tu, leo nimekuta Mil 300 zimo kwenye account yangu ya Benki - Sijui zilikotoka sasa naomba ushauri kwenu:

1. Niripoti bank yangu kwamba kuna mzigo sijui ulikotoka
2. Nikae kimya kwanza kusikilizia
3. Nianze kuzitumbua
4. Nizihamishe fasta kwenye acc nyingine
5. Nizitoe zote nikae nazo home, sababu wanaweza ku-trace kama nikiweka kwenye acc yangu nyingine?

Wazoefu naombeni ushauri wenu - nimedata hata kazi nashindwa kufanya - Jina la Benki naliweka kapuni kwa sasa.
 
Huo muda uliotumia kutype humu ungeutumia kuuvuta huo mpunga uwe nao utajua utakapouweka,afu mambo mengine ndo yafate.

Mimi hua nawaambia washkaji zangu yaani kwenye akaunti yangu nikute hela yoyote iwe billion au trilion siiachi.Mambo mengine baadae.
 
Police Tanzania na DCEA ile Kampeni yenu ya kutokomeza Kilimo cha Bange na Matumizi yake kwa baadhi ya Watanzania imeishia wapi?
Bange tena Mkuu, wakati mi nazungumzia mzigo kwenye acc sijui ulikotokea.
 
Kama ni kweli na hukua usingizini kwamba unaota basi elewa kua hilo ni jambo la kawaida sana kutokea Bank. Kama usemavyo ni kweli basi ujue sio tu kwamba pesa hizo sio zako bali ni za moto. Utakapo zigusa kama ulivyosema mwenyewe kwa kuzitoa au kuzihamisha, kosa la UTAKATISHAJI linakuhusu

Ila ni suala ala muda mfupi tu kwenye ripoti za siku iwe Bank yako au huko zilipotoka watajua na watazirudisha zinapostahili. Ushauri wangu zitolee taarifa hapo tawini kwako au tawi la karibu la Bank yako ingawa naelewa Bank hawatakupa hata buku zaidi ya kukushukuru na kukuona muaminifu
 
Back
Top Bottom