Wakuu nifanyeje? Mke wangu ananipenda sana

Mke wangu ghafla tu kila nikirudi home ananipa mabusu motomoto, mara aniangalie kwa jicho la kuning'inia , ananiambia maneno matamu na mazito?

Kuna mtu ameniambia mwanamke akikupenda sana ghafla basi kuna uwezekana wa kutaka kukuwekea sumu au kukumwagia maji ya moto.

Suala la maji ya moto nimenunua asali lita 5 ziko ndani tayari lkn hili la pili bado sijajua nifanyeje msaada wenu wakuu.

Duh! Aki umenichekesha Sana
 
Aiseee yani skuizi hakuna kuaminiana kabisa

Mtu unapendwa kiroho Safi ushawaza kuwekewa sumuu

Corona ndo maana imeondoka zake

#Stayhome
 
Maskini so hakuna sababu nyingine ya mwanamke kuonesha mahaba kwa waume zao?

na ajabu kuna mwanaume atabeba huu ushauri
Kwa sis wenye experience tunasema

Mwanamke mwenye furaha ya kwel na mwenye furaha ya kukupanga huwa anajulikana tuu
 
Mke wangu ghafla tu kila nikirudi home ananipa mabusu motomoto, mara aniangalie kwa jicho la kuning'inia , ananiambia maneno matamu na mazito?

Kuna mtu ameniambia mwanamke akikupenda sana ghafla basi kuna uwezekana wa kutaka kukuwekea sumu au kukumwagia maji ya moto.

Suala la maji ya moto nimenunua asali lita 5 ziko ndani tayari lkn hili la pili bado sijajua nifanyeje msaada wenu wakuu.

MSAGA SUMU wewe endelea kuimba singeli tu, mapenzi tuachie sie tuliyozoea. Naomba unipe contact za huyu mkeo maana naona kishakuwa kero kwako, hakufai kabisa.....nipe namba zake fasta nataka nikuokoe kwani mafans wako bado wanahitaji nyimbo zako.
 
Maskini so hakuna sababu nyingine ya mwanamke kuonesha mahaba kwa waume zao?

na ajabu kuna mwanaume atabeba huu ushauri

Kiukweli hata mimi kama mke wangu alikua yupo kawaida tu halafu ghafla abadilike na kuanza kuonyesha mahaba mazito kwakweli mimi ntaogopa sana! Hapo lazma kutakua kuna kitu:
1. Kuna kitu kikubwa kaharibu sasa anatafuta gia ya kukuingia
2. Kachepuka so anakuzuga ili usihisi kitu
3. Kapigwa mimba nje anataka kukubambika
4. Kakopa hela nyingi sehem kashindwa kulipa
5. Kaona meseji kwenye simu anataka kukutega akuue
6. Katembea na kaka/mdogo wako
8. Kapigwa chini na mchepuko so anajifariji
9. Anatafuta chansi ya kukuwekea dawa aliyopewa na mganga
10. Sababu nyingine zisizofikirika
 
Back
Top Bottom