Cliffhanger
JF-Expert Member
- May 22, 2018
- 721
- 1,292
Wakuu, ni kwa nini kizazi hiki cha sasa kinaona ugumu kutumia herufi H kiusahihi? Neno Habari linaandikwa Abari, Hujambo inaandikwa Ujambo, Hayupo inaandikwa Ayupo. Mengine mtaongezea.
Mwanzoni nilifikiri kuwa ni uvivu wa kuandika maneno mengi, kilichonishangaza ni kuwa hata sehemu ambayo inatakiwa itumike A tupu panaandikwa Ha, Kwa mfano neno Amekubali linaandikwa Hamekubali.
Je tufanyeje kama wana Jamii kurekebisha tatizo hil?