Wakuu nataka kununua gari kwa Mara ya kwanza na ninaishi mazingira ambayo ni rough kiasi. Naomba kujua ni gari gani dogo linaweza kuvumilia

V
Kwa hizi sifa
-Mara ya kwanza kumiliki gari
-Rough road
-Gari ndogo
-Gari ya gharama rafiki.

Hapo unashauriwa kununua Suzuki Jimny, ama Suzuki Escudo (old model). Tofauti na hapo ni vigumu kupata gari yenye kufit sifa zote hizo kwa pamoja. Sana sana ukikwepa unaweza kuishia kwenye kumiliki pikipiki, maana inaweza kuwa msaada kuliko kung'ang'ania kumiliki gari yoyote wakati vigezo havikidhi.
Vipi Mitsubishi io au hata mini yenye 4WD kama pesa yake ni ndogo zaidi. Vina nguvu alafu viko juu juu avilambe ardhi hata barabara ikiwa ya hovyo. Shida yake spear ila hayaharibiki hovyo hovyo, body za Mitsubishi asilimia kubwa ni chuma ngumu.
 
Back
Top Bottom