Wakuu natafuta hii movie ya kihindi

Pain killer

JF-Expert Member
Aug 15, 2017
6,839
2,000
Daa

Hii movie nimeiona miaka nyuma kidogo sijui inaitwa je,ipo hivi

Kuna mama alikuwa analea watoto, sasa pale kwake kuna maabara flani doctor alikuwa anafanya utafiti,

Kuna siku doctor akawa amemuonesha yule mama dawa flan ambayo ukinywa unakuwa huonekan machoni kwa watu, wakaifanyia majaribio wapo wawili maaabara na kweli ikaonekana hivo, kumbe mtoto mmoja kawachungulia, walivotoka tu maabara yule mtoto akanywa ile dawa mara akawa haonekan, vituko vikawa vinaonekana ndan, mtoto akibeba hata sahan, Mule ndan wanaona ni sahan pekee inatembea wanashangaa, akipanda baiskel wanaona baiskel pekee inajiendesha ,ile dawa ilikuwa inatumika masaa machache kulingana na kias alichokunywa


Kuna siku yule mama alitekwa na majambazi, aisee hapakuwa na masaada Wa police wala nini, yule dogo akanywa ile dawa akaenda kumsaidia, wakat anamuokoa aisee, ilikuwa inaonekana bastola pekee yake inapiga maadaui inajipiga kitu kilichowashangaza maadui, wakawa wanamimim risasi ovyo, ikamnasa dogo, mara gafla akaonekana ila mwil ukavimba na kuwa mkubwa zaidi kuzid hadi majengo ,kiufupi akaonekana lakini, sio binadamu wa kawaida tena,!

Alimaliza Wale maadui wote, kwa vile sio wakawaida hakupaswa kuishi tena kwenye jamii ya watu, akapotelea baharin movie ikawa imeisha


Wakuu anayeijua hii movie jina Lake tafadhali

Naihitaji saizi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom